Kikosi cha Timu ya Taifa kufuzu AFCON Chatangazwa

Kikosi cha Timu ya Taifa kufuzu AFCON Chatangazwa

AbaMukulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2018
Posts
2,053
Reaction score
3,586
Chama cha soka nchini Tanzania kimeachia majina rasmi ya wachezaji wa Tanzania ambao watashiriki kwenye mechi za kuwania ushiriki wa mashindano ya AFCON 2023 dhidi ya Niger.

FyqDUHcWAAAsRMx.jpeg
 
Wengine wanacheza ndondo cup huko nje lakini wanaitwa na huku uwezo mdogo. Sio Kila mchezaji anayecheza nje ya nchi anastahili kuitwa Timu ya Taifa.
Ni kweli kabisa. Halafu nina wasiwasi baadhi ya hawa wachezaji wana uraia wa nje pia, au tufumbe macho kwa kuwa ni jambo la kitaifa?
 
Wengine wanacheza ndondo cup huko nje lakini wanaitwa na huku uwezo mdogo. Sio Kila mchezaji anayecheza nje ya nchi anastahili kuitwa Timu ya Taifa.
Wataje kabisa mkuu
Usipige jiwe gizani
 
Ni kweli kabisa. Halafu nina wasiwasi baadhi ya hawa wachezaji wana uraia wa nje pia, au tufumbe macho kwa kuwa ni jambo la kitaifa?
Sio una wasiwasi bali ni kweli hao wanaocheza ligi za nje ya Africa ukimuacha Samatta na Dismas wana uraia wa nchi nyingine lakini wana uwezo wa kuchezea timu ya taifa bila shida maana inaruhusiwa kwenye mpira..

Hata TFF walishatoa kibali maalumu kwa Diaspora wenye asili ya Tz kuruhusiwa kuchezea timu ya taifa hata kama wana uraia wa nchi nyingine ukweli ni kwamba tz ina diaspora wazuri sana na wanaofanya vizuri sema Scouting yetu ni hafifu sana aisee Norway kuna mtanzania mpaka kafikisha miaka 32 hakuwahi kuitwa timu ya taifa yoyote hadi leo msimu ulioisha kapiga magoli 35 katika mechi 32 ya ligi kuu Norway ila tumefumba macho hatumuoni,Austria kuna kiungo hatari anaitwa Lema ni mchaga anakimbiza ile mbaya hatujawahi kumuita,kuna dogo yupo Adelaide fc,Australia yupo mbioni kusajiliwa na Bayern munich kazaliwa kambi ya wakimbizi Nyarugusu ni mtanzania na mrundi ana option ya kuchagua hapa lakini hadi leo tupo kimya kumshawishi..Fc Nantes ya ligi kuu ufaransa kuna mtanzania Omari mvungi na anafanya poa tu sisi tunang'ang'ania simba na yanga we have to change!!

Nchi zote zinazofanya vizuri hapa Africa ni matokeo ya professional players wanaocheza nje ya bara la Africa hawa Congo DRC hawana tofauti na sisi ila wanafanya vizuri tangu zamani kwa sababu ya Diaspora wanaokipiga nje sisi tumeng'ang'ania siasa za simba na Yanga eti kwanini Kapombe hajaitwa!
 
Sio una wasiwasi bali ni kweli hao wanaocheza ligi za nje ya Africa ukimuacha Samatta na Dismas wana uraia wa nchi nyingine lakini wana uwezo wa kuchezea timu ya taifa bila shida maana inaruhusiwa kwenye mpira.l..
Nchi zinazofanya vizuri Zina mipango mizuri na uwekezaji kuanzia timu za vijana ila sisi tunaenda shortcut ndio maana tunafikiri tukitoa uraia tutafanikiwa tunasahau Taifa la watu million 60 haliwezi kutoa wachezaji bora
 
Back
Top Bottom