Kikristo ni dhambi gani unakuwa umeitenda ukiamua kuwa na wake wawili au zaidi

Kikristo ni dhambi gani unakuwa umeitenda ukiamua kuwa na wake wawili au zaidi

Hado sijafika umri wa kuoa ila nikija kuwa na uwezo naoa mke zaidi ya mmoja japo mkristo, hizi sheria watu walijewekea
 
Kitu wakristo walikosea na kukataza mwanaume kuwa na wake zaidi ya mmoja, imechangia sana kuharibu muundo familia, mke lazima awe na bimdogo wa kumchallenge. Hata watoto nao wanajitahidi kuwa best versions of themselves wakishindana na watoto wa wake wengine. Ila siku hizi zero tu
Unawaza ngono sana.
 
Je ni dhambi kuoa mke zaidi ya moja ?

Kama ni dhambi, hio ni dhambi ipi waliyoitenda pia kina Musa, Lameki, Yakobo, Daudi, n.k. kwa kuoa zaidi ya mke moja ?
Busara za wamisionari tu
Babu zetu waliupokea ukristo wakiwa na mke zaidi ya mmoja na walioleta ukristo waliendelea kuheshimu jambo hilo.
 
mwanamke akijua muda wowote waweza kumletea mwenzie basi hata tangu akiwa kwao mama yake atamuasa sana na kumpa mafundisho kuishi na mume, ila akijua milango yote imefungwa hata mafundisho anaweza kupuuzia maana anajua mpo sawa tu
Acha kuwaza ngono kijana. Kwanini umtishie mwanamke utamuacha kwa kuoa mke mwingine ili ajirekebishe? Hakuna mafundisho mengine ambayo tofauti na kufanya ngono na mwanamke mwingine ajirekebishe?
 
Acha kuwaza ngono kijana. Kwanini umtishie mwanamke utamuacha kwa kuoa mke mwingine ili ajirekebishe? Hakuna mafundisho mengine ambayo tofauti na kufanya ngono na mwanamke mwingine ajirekebishe?
Wewe ndio uache kuwaza ngono kwa kudhani kuongeza mke ni kuhusu ngono pekee.

Kuoa mke zaidi ya moja unakuwa umeheshimisha wanawake wajulikane wana ndoa

Kuoa mke zaidi ya moja wanaweza kukupa watoto wengi zaidi "enendeni mkaijaze dunia"

Kuoa mke zaidi ya moja hupooza tamaa ya kuzini pale moja anapokuwa kapata kazi ulaya wewe upo Namtumbo
 
Acha kuwaza ngono kijana. Unawaza, akienda mbali utafanya ngono na nani. Haujawaza mtoto au watoto watabaki nani ila umefikiria ngono. Unaweza kukaa mwaka mmoja au miwili bila kufanya ngono?
Unaona kuwaoa wanawake wawili ndiyo unawaheshimisha?
Nendeni duniani mkaijaze dunia, basi kwa mawazo yako ya ngono ukafikiri ni kuoa wanawake wengi?
Kwanini Mungu hakumpa Adamu wake wawili akampa mmoja tu? Yeye hakuona hayo mpk ampe mke mmoja?
 
Je ni dhambi kuoa mke zaidi ya moja ?

Kama ni dhambi, hio ni dhambi ipi waliyoitenda pia kina Musa, Lameki, Yakobo, Daudi, n.k. kwa kuoa zaidi ya mke moja ?
Hakuna dhambi, kinachoenda mbinguni ni roho siyo mwili na ndiyo maana hata mbinguni hutakutana na mke wako unayemuita wa ndoa. Hivyo oa hata wake 100 as long as unaweza kuwahudumia no problem.
 
Nilichogundua hapa wengi wenu hamna uelewa na biblia au maandiko kwasababu mnajibu vitu ambavyo havipo ngoja niwaambie ipo hv kuoa mke mmoja hy sheria imewekwa na watu maalumu kama vile mapadre nk ila sio muumin wa kawaida ni viongoz wa dini
 
Je ni dhambi kuoa mke zaidi ya moja ?

Kama ni dhambi, hio ni dhambi ipi waliyoitenda pia kina Musa, Lameki, Yakobo, Daudi, n.k. kwa kuoa zaidi ya mke moja ?
Mkuu Randy Orton nakukumbushia tu huu uzi hapa chini uliuleta wewe. Inaelekea hili swala linakugusa sana.

Mkuu Randy Orton nakukumbushia tu huu uzi hapa chini uliuleta wewe. Inaelekea hili swala linakugusa sana.

Ndo ukweli huo, wanawake wanatafuta ndoa ila wanaume wa kuwaoa wapo wachache, matokeo yake wanashinda makanisani kusubiria miujiza ambayo kwa hesabu za uchache wa wanaume haiwezekani
 
Ndo ukweli huo, wanawake wanatafuta ndoa ila wanaume wa kuwaoa wapo wachache, matokeo yake wanashinda makanisani kusubiria miujiza ambayo kwa hesabu za uchache wa wanaume haiwezekani
Hakuna mwanamke anayeona heshima ni kuolewa mke wa pili unajidanganya, kila mwanamke anapenda mume wake mwenyewe...
 
Hakuna mwanamke anayeona heshima ni kuolewa mke wa pili unajidanganya, kila mwanamke anapenda mume wake mwenyewe...
kuna utofauti wa unchopenda na unachostahili. Unaweza kupenda uwe unakula peke yako lakini ni vema ukileta chakula nyumbani ule na wenzako.

Hata Rais wetu ni mke wa tatu na imelinda heshima yake kwamba ana ndoa.

kila mwanamke awe na mme wake haiwezekani maana wanaume ni wachache kuzidi wanawake na wapo wanaume wachache zaidi wanaoweza kuoa.
 
kuna utofauti wa unchopenda na unachostahili.

Hata Rais wetu ni mke wa tatu na imelinda heshima yake kwamba ana ndoa.

kila mwanamke awe na mme wake haiwezekani maana wanaume ni wachache kuzidi wanawake na wapo wanaume wachache zaidi wanaoweza kuoa.
Sio heshima kuolewa mke wa pili...

Inachukuliwa ni unyanyasaji fulani wa kijinsia...

HAKUNA mwanamke anayependa kuolewa mke wa pili, hata huyo Rais hujui kama angekua na option ya kuwa na mume mmoja wa peke yake kama angechagua kuwa mke wa tatu??!

Nani kakwambia kila mwanamke ni lazima aolewe au kila mwanaume lazima aoe ???
 
unyanyasaji wa kijinsia ni mambo ya feminists hao waliochochea mambo ya usagaji.

Kama kina Musa walioaminiwa kufanya mission kibao za Mungu walikuwa na wake wawili na Mungu hakukemea sehemu yoyote ni kwamba haina tatizo.

Kama mwanamke hataki hayo maamuzi yake, anaweza kufuga paka ampe kampani.
 
Ni mambo ya feminists, kwa mtazamo wako, ila mwanamke ni kiumbe mwenye hisia, kugawana/kushare mtu unayempenda ni jambo gumu,..... kama wewe huwezi kumuona mkeo akizalishwa na mwanaume mwingine ndivyo na wanawake wanavyofeel, sasa ukiheshimu hisia hizi za wanawake huwezi kuja na ishu za kuoa wake wengine ndio maana tunasema ni unyanyasaji wa kijinsia....

Kama unafuata vitabu Mungu hajakemea, ila pia hajaruhusu kwa maneno yake...sasa ni jukumu lako kujifanya wewe ni Musa uoe wake wengi...

Kuna wanawake wengi tu hawana kampani, hawana paka ila swala la kuolewa mke wa pili haliwaingii...
 
Amri za Mungu zinasema.
'Mpende Mungu wako kwa akili zako zote, kwa nguvu zako zote na kwa moyo wako wote. Mpende jirani yako Kama nafsi yako.'
Halafu Kuna zile amri kumi kutoka kitabu Cha kutoka.
 
Marko 10:7-9
[7]Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;

[8]na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.

[9]Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
 
Je ni dhambi kuoa mke zaidi ya moja ?

Kama ni dhambi, hio ni dhambi ipi waliyoitenda pia kina Musa, Lameki, Yakobo, Daudi, n.k. kwa kuoa zaidi ya mke moja ?
Kabla hujauliza hilo swali,,

Ungejiuliza kwmba YESU hakuwa na mke wala hakuwahi kufunga ndoa,

Zile sheria za ndoa kaweka nani kwenye biblia?
 
Dini ya Kiislamu ni bora sana kwa mwanaume alie kamilika na dini ya kikristo ni bora sana kwa mwanamke wa sasa.
 
Back
Top Bottom