Kikwete Alipata Wapi Madaraka ya Kuanzisha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya ya JMT?



There ur....100%. What is the main objective for us 'Tanzanian' 2 write a new constitution?baada ya kujibu swali hili uhalali na sio uhalali, mchakato uendeje, na usainiwe au usisainiwe majibu ya haya yote yatapatikana kwa jibu la swali hilo.
 
Debe Tupu Haliachi Kuvuma.

Mwanzilishi wa thread hii ni Debe Tupu, linavuma...
 


Mwanzilishi wa hii thread ni mtu ambaye anaombe Tanzania iwe nchi ya vurugu. Sasa hivi roho inamuuma sana anapoona mchakato wa katiba unaendelea kwa utulivu.

Tumeshamzoe na harakati zake za kuchochea vurugu na chuki. Watu wameshaanza kumshtukia, ndio maana mgomo wake wa simu ulifeli.
 
Kama huu mchakato ni haramu, kwa ushauri wako ni kuendelea na katiba tuliyonayo?

Chombo halali ni kipi?
Mkuu,

Usiumize kichwa chako bure.

Wapo watu ambao katika kila jambo lazima watafute jinsi ya kuchafua hali ya hewa. Mchakato uko hatua za mwisho, anatoke mtu kuuliza kama mchakato una uhalali wa kuanzishwa!!!

Kwa vile mleta thread anajulikana historia yake ya kuchochea vurugu baina ya watanzania, basi msipate shida kushughulisha vichwa vyenu kwa hoja zake mfu...
 
Nina mashaka na hoja kama hizi iwapo wanaozishupalia hajabeba ajenda ya makundi ya mafisadi ambao tunasikia wasingependa katiba mpya ipite kwa vile itawakwamisha malengo yao ya 2015. Tafakari.

Aliyeleta mada haitakii mema Tanzania. Ni mtu ambaye kila siku yuko mstari wa mbele kuchochea vurugu na kupinga harakati za maendeleo ya watanzania. Mtu wa namna hiyo hawezi kutoa ushauri mzuri kwa ajili ya taifa la Tanzania.
 

Nguruvi3

Wewe ukiwa miongoni mwa wanaoipigania agenda ya serikali tatu inabidi uanzekujiuliza kwa kina ni nani mwenye mamlaka ya kusimamia mchakato wa kuandika katiba ya Tanganyika? This is what people should be discussing now because unlike Tanzania, Tanganyika has no organ at all. Mambo ya Tanzania yanaweza kusimamiwa na Bunge la Tanzania, je ya Tanganyika?

Haya maswali ya kitoto ya mwanakijiji amnbayo yanawachanganya zaidi watu badala ya kuonyesha way forward at this time mngeyapuuza tu. Watu wafikirie mbele badala ya kukaa chini na kuzogoana!!!
 

Upinzani tu usingekuwa sababu ya kufanya kitu kikubwa na nyeti hivi. Kumbuka alishinda na kuapa kulinda na kuhifadhi Katiba anayotaka kuibadilisha. Nafikiri factor ya Zanzibar ilikuwa msingi mkubwa wa mchakato huu. Zanzibar kwa Katiba yao walishakinzana na Katiba ya Muungano. Hakuna njia ingine isipokuwa kutengeneza Katiba mpya ili kuondoa msigano huu.
 
Wewe mwanakijiji sometimes you make yourself look stupid, ulitaka Huo mchakato auanzishe kilaza mbowe? Zamani ulikua na hoja, sasa hivi uko Kama dada powa
 

Tanzania kazi yetu ni kuiga nini Kenya wamefanya na sisi tufanye. Kwenye vyama vingi mambo yalikuwa hivi hivi. CCM wanajaribu kufanya kitu wasichokita...........hivyo hakufanikiwa mpaka pale wananchi watakapoamua kwa dhati kuwa kweli wanaitaka katiba mpya.
 

wewe ndio ume nielewesha....huyu jamaa sijaelewa alicho kua anaongea.
 
"Chombo halali" kitapatikanaje?Kuuliza si ujinga...

chombo halali kinapatikana kwa njia halali. Chukulia kwa mfano; Rais Kikwete akiamua kesho kuwa anaanzisha Mahakama ya Wanawake - je itakuwa ni halali kwa yeye kufanya hivyo kwa sababu tu anaamini kesi zinazohusiana na wanawake zinahitaji mahakama maalum; na wakatokea wanawake wengi wakamuunga mkono... sisi wengine tutapinga kwa sababu hana madaraka ya kuanzisha mahakama!
 
Haya maswali ya kitoto ya mwanakijiji amnbayo yanawachanganya zaidi watu badala ya kuonyesha way forward at this time mngeyapuuza tu. Watu wafikirie mbele badala ya kukaa chini na kuzogoana!!!

Tuchukulie kuwa ni swali la kitoto lijibu basi; maana hata mtoto akiuliza swali anapewa jibu. Ukiona mtu mzima anashindwa kujibu swali la mtoto ni kwa sababu mtoto kauliza swali gumu. Wewe unaamini Kikwete (Rais wa Tanzania) ana madaraka ya kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya.
 
wewe ndio ume nielewesha....huyu jamaa sijaelewa alicho kua anaongea.

Usipoelewa ni vizuri ukauliza usichoelewa; kwani kila mtu ana uelewa wake. Wakati mwingine ni matatizo ya mwelewa au ya mweleweshaji. Ningejaribu kukufafanulia; lakin ikwa vile wengine wanaelewa vizuri - kama alivyofanya Nguruvi basi ni vizuri kuwasoma wengine uone wameelewa vipi na wao wakakuelewesha.
 
mwanakijiji tulipaswa tufuate njia ipi!?

Incredible and very intelligent question:

a. Kwanza na zaidi kabisa walitakiwa kuangalia Katiba ya sasa inasemaje kuhusiana na kuandika Katiba Mpya.
b. Kwa vile Katiba ya sasa hairuhusu kuandika Katiba Mpya (chini ya Ibara ya 98) basi walitakiwa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa (hasa kwa watu wanaosema wanafuata utawala wa Katiba na Sheria)
c. Katika mabadiliko hayo ya Katiba walitakiwa kuweka utaratibu wa kuandika Katiba Mpya kama ulivyo utaratibu wa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa.

Kutoka hayo matatu ndio tungezungumzia kuandika Katiba Mpya.

Sasa hivi wote hawa wanaweza kuitwa wahaini tu!
 
Nadhani alifanya hiyo sababu ya uwoga wa Vyama vya upinzani.Kwa sababu hata kwenye ilani ya CCM mchakato wa katiba haukuwepo.Pili labda baada ya kuona wenzetu Kenya wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuandika katiba mpya,ila hakufahamu kuwa wakenya walikuwa na nia ya dhati ya kuandika katiba.
 
kwahiyo mnasemaje wadau , tuuchinjie baharini au ? Maana uwezo tunao !
 
WE mzee umefulia huna jipya uwe unanyamaza kama huna ya kusema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…