MM
Kwakweli nimecheka sana, swali ni rahisi lakini lina majibu tofauti kabisa. Watu wanafeli mitihani si kwa kutojua bali kwa kutoelewa swali.
Swali ni hivi, ili katiba ibadilishwe kwa kutumia sheria na utaratibu wa bunge unaosemwa ni lazima kuwepo na chanzo cha kufanya hivyo. Sasa hivi tunajua chanzo ni JK kwasababu hakuna mahali CCM au Serikali yake imejadili kuhusu kuandikwa kwa katiba.
Kwa mantiki hiyo hili ni wazo la JK. Swali wazo hili limepataje uhalali hadi liandikiwe katiba?
Kupitia taratibu za bunge ni matokeo ya wazo hilo, uhalali wa wazo umepatikana wapi.
Yupo aliyesema wazo limepitia njia halali, well hata wenye pesa chafu za damu wakiziingiza katika mzunguko zinakuwa na uhalali lakini je chanzo cha pesa hizo ni halali?
Maana ya swali hili ni kuwa kama tutaruhusu mtu aamke asubuhi na kubadili mambo mazito kama haya basi rais X ajaye naye anaweza kuamka asubuhi na kuamua iandikwe katiba nyingine. Kila baada ya maiaka 5 tutaandika tu kwasababu kuna mtu ana wazo hilo.
Mwanzo wazo lililopotolewa tulihoji kama ilikuwa ipo katika ilani ya uchaguzi au ni sera au kuna kukao chochote kilichofikia maamuzi japo kwa uchahce. Jibu ni hakuna. Tunajua ilikuwa hoja ya wananchi kupitia wapinzani.
Hata hivyo kama taifa hatujawahi kukaa na kupanga tunataka taifa la namna gani na tuliandae vipi.
Tukasema mchakato wa katiba wa kutumia wazo la JK si sawa na kuanzisha chuo cha UDOM. Hili ni suala zito linaloweza kuivuruga nchi sana. Tukaambiwa ni mafaataani sasa nadhani ukweli unaonekana.
Huu ni mwanzo tu ninachokiona ni nchi kuingia katika machafuko. Hilo ninaliona kwa mbali.
There ur....100%. What is the main objective for us 'Tanzanian' 2 write a new constitution?baada ya kujibu swali hili uhalali na sio uhalali, mchakato uendeje, na usainiwe au usisainiwe majibu ya haya yote yatapatikana kwa jibu la swali hilo.