Kikwete ana ubia gani kwenye serikali ya sasa?

Wanasahau kuwa hata magufuli mara kibao alimtumia kikwete kwenye safari za nje.
 
Kwa nini kwa uzoefu huo hatumiki ndani ya nchi kusaidia reforms za election na democracy?
Unachanganya diplomasia za kimataifa ambazo Watanzania wengi wanaungana na siasa za ndani ambazo Watanzania wengi wanapingana.
 
Unachanganya diplomasia za kimataifa ambazo Watanzania wengi wanaungana na siasa za ndani ambazo Watanzania wengi wanapingana.
Nilifikiri diplomasia za kimataifa zinajengwa na msingi wa siasa za ndani!
 
ajabu kupinga uzoefu wa jk
Ni vigumu sana kumchukia mtu kwa sababu ya siasa zake halafu kukubali vipaji vyake vingine au hata uwezo alioupata kwa sababu ya kushika viti fulani.

Mimi nimeweza kumkosoa Kikwete kwenye mambo mengi lakini siwezi kushangaa akitumiwa kwenye hili.
 
George Bush aliwahi kumpa Bill Clinton majukumu gani?
Obama aliwahi kumpa Bush majukumu gani?
Nyerere aliteuliwa na viongozi wa maziwa makuu kuwa mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, sio Mkapa.
Bush kampa Clinton majukumu mengi moja wapo ni kwenye misaada ya Tsunami Asia mwaka 2004 na kimbunga Katrina

Obama pia kampa Bush majukumu mengi tu moja wapo ni kusimamia misaada ya tetemeko la Ardhi la Hait mwaka 2010 .

Au ulikua haujazaliwa?
 
Taifa letu likijankupata ukombozi wa kweli kabisa, huyu mzee atatajwa kama adui wa taifa! Wanaompenda hawataamini jinsi alivyo sumu mbaya kwa taifa.
 
Bush kampa Clinton majukumu mengi moja wapo ni kwenye misaada ya Tsunami Asia mwaka 2004 na kimbunga Katrina

Obama pia kampa Bush majukumu mengi tu moja wapo ni kusimamia misaada ya tetemeko la Ardhi la Hait mwaka 2010 .

Au ulikua haujazaliwa?
Sidhani kama unaelewa unachosema
 
Acha uzwazwa. Mbona hatukumuona Mwinyi akitumiwa na kumtumikia Mkapa au mbona hatukumuona wakati wa jiwe ambaye alimbana vilivyo? Kikwete ana tabia za kupenda kuzuruura ndo maana akaitwa vaso da gama. Hukumbuki!!!
Hukumuona wapi, wakati ulikua kinda unaetoka kamasi na kulamba.
 
Ndiyo dalali no 1 wa rasilimali za nchi
 
Acha uzwazwa. Mbona hatukumuona Mwinyi akitumiwa na kumtumikia Mkapa au mbona hatukumuona wakati wa jiwe ambaye alimbana vilivyo? Kikwete ana tabia za kupenda kuzuruura ndo maana akaitwa vaso da gama. Hukumbuki!!!
Ni dalali wa mali za umma
 
Huyu mzee pamoja na yote ila kwenye diplomasia na maswala ya kijamii yuko vizuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…