Kikwete aonya Serikali kupuuza ushauri. Ataja madhara yake

Kikwete aonya Serikali kupuuza ushauri. Ataja madhara yake

Mwl Nyerere alimkosoa Rais wa awamu ya pili Mzee Mwinyi,Rais wa awamu ya tatu Mzee wetu Mkapa alimkosoa Rais wa awamu ya tano Dr JPM,binafsi sioni taabu Rais wa awamu ya nne akikosoa awamu ya sita
 
Toka aingie madarakani Mwenye nchi yake Mshauri Mkuu wa kazi Dr. Abdurazak Makohashim Bin Hemed, Ushauri mwingine unawekwa kando.
Ndio maana tumekasirika.
 
Wewe kujiaminisha huko CCM au serikalini, sijui Kinana na Chongolo wamekwazika kwa sababu ya uteuzi wa Makonda aina maana huo ndio uhalisia.

Mtu kama Chongolo ndio kwanza alikuwa akiwananga viongozi wa CCM Dar hadharani (clips zipo YouTube) kwa kukosa shukrani katika ziara yake na kujifanya kusahau mazuri ya Makonda aliyowafanyia wakati kawajengea majengo ya chama kwa jitihada zake pamoja na kuongeza ward kadhaa za wazazi ambazo hospitali zimefaidika.

Uteuzi wa Makonda, mimi na wewe strategically hatujui shabaha ya CCM; ila sio wa bahati mbaya.

Hata ukishinda hapa Makonda hivi Makonda vile hiyo teuzi aiwezi badilika wanajua wao wanakitaka nini kutoka kwa huyo mtu.
Sasa Kikwete kakasirishwa na nini au anamaanisha nini katika kauli yake hii?
 
Sasa Kikwete kakasirishwa na nini au anamaanisha nini katika kauli yake hii?
Post yangu #139 uliyo quote mara ya kwanza kule nimesema itakuwa kachukuliwa out of context tu in my opinion alichosema kwenye huo mkutano ili watu watengeneze story za ugomvi ambao haupo.

JK hana sababu ya kulumbana na Samia hadharani watu wote muhimu ambao raisi anashauriana nao ndani ya serikali na kwenye chama ni watu waliokuwa kwenye system ya J.K.

Ukitaka system yako weka wapya, ndio maana Magufuli watu kama kina Lhuwavi aliwatoa nje ya nchi na nafasi za ubalozi, same thing, Samia kapangua Ikulu na kwenye chama watu wa Magufuli kaweka wake.

Be it Samia karudisha watu wa JK Ikulu na kwenye chama sasa sioni sababu ya JK kutaka kulumbana na raisi hadharani wakati logic ni kwamba anapata habari zote za hii serikali hata zile ambazo raisi ana confide to very few individual kuhusu mipango yake.
 
ukitaka kupima uwezo wa raisi yoyote mstaafu Duniani angalia post presidency yake anafanya nini? Hata tu foundation ya kusaidia jamii hakuna, haandiki vitabu, hakuna chochote intelectually, I mean nothing, hilo peke yake linakwambia mengi sana, kila kukicha majungu tu …
Selfishness !!
 
Post yangu #139 uliyo quote mara ya kwanza kule nimesema itakuwa kachukuliwa out of context tu in my opinion alichosema kwenye huo mkutano ili watu watengeneze story za ugomvi ambao haupo.

JK hana sababu ya kulumbana na Samia hadharani watu wote muhimu ambao raisi anashauriana nao ndani ya serikali na kwenye chama ni watu waliokuwa kwenye system ya J.K.

Ukitaka system yako weka wapya, ndio maana Magufuli watu kama kina Lhuwavi aliwatoa nje ya nchi na nafasi za ubalozi, same thing, Samia kapangua Ikulu na kwenye chama watu wa Magufuli kaweka wake.

Be it Samia karudisha watu wa JK Ikulu na kwenye chama sasa sioni sababu ya JK kutaka kulumbana na raisi hadharani wakati logic ni kwamba anapata habari zote za hii serikali hata zile ambazo raisi ana confide to very few individual kuhusu mipango yake.
Hii inafikirisha sana !!
We have been taken for a ride !
Jamaa yupo vizuri sana katika hizo tecnics toka zamani !!
 
Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema Serikali ikikosa ushauri mzuri ama ikipuuza nchi itakwenda pasipostahili.

Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Novemba 22, 2023 alipokuwa akielezea umuhimu wa makongamano na mikutano katika kuishauri Serikali na Rais, kwenye mkutano wa nne wa Maendeleo ya Biashara na Uchumi ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) ambapo alikuwa mgeni rasmi.

“Ukikosa ushauri mzuri ama ukipata ushauri mzuri ukaupuuza hii nchi itakwenda kusikotakiwa kwenda. Ndio maana makongamano haya ni muhimu sana unachota mawazo,” amesema Kikwete aliyekuwa Rais wa nne wa Tanzania (2005-2015).

Amesema unapokuwa Rais hujui kila kitu lakini unatakiwa kushughulika na kila jambo na kwa sababu huwezi kujua kila kitu inakubidi kutegemea ushauri.

“Wenzako wanakuchagua kwamba unafaa kuwa Rais, lakini utakuwa hujui kila kitu, taaluma yako ni uchumi…lakini ukiwa Serikali na Rais hujui kila kitu. Kwa sababu huwezi kujua kila jambo, lazima utegemee sana ushauri,” amesema.

Amesema ndio maana Rais ana mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, makamishna, wakurugenzi na ofisi binafsi ambayo inawashauri.

Amewataka wasomi hao kutoa ushauri kwa Serikali juu ya mambo mazuri ya kufanya na kile ambacho si kizuri kiachwe na kirekebishwe.

Kikwete amesema uchumi hauwezi kukua bila uwekezaji, na unakuwa mahali ambapo mazingira ya biashara ni rafiki ikiwa vinginevyo wawekezaji wataondoka.

Ametoa mfano wa mfanyabiashara maarufu, marehemu Zacharia Hans Poppe ambaye wakati wa uhai wake alikutana naye nchini Afrika Kusini.

Amesema mfanyabiashara huyo alimweleza amehamishia biashara zake na magari yake yote nchini humo kutokana na mazingira ya biashara kutokaa vizuri nchini.

Amepongeza chuo hicho kwa kuandaa kongamano hilo, lakini akashauri kuangalia uwezekano wakuandaa lingine ambalo litashirikisha taasisi nyingine za elimu za juu.

Kikwete amesema kufanya utafiti ni njia ya kuboresha upeo na maarifa ya kila mtu na itasaidia katika maendeleo ya Taifa.

Bei za mafuta kupanda

Kikwete amesema iwapo bei ya mafuta imepanda katika nchi zinazozalisha ni wazi haiwezi kupungua nchini.

“Namshukuru Rais (Samia Suluhu Hassan) kwa utashi wa kisiasa ameweka ruzuku ya Sh100 bilioni lakini hii inapunguza kwa senti chache. Wakishaweka ruzuku ya Sh100 bilioni bei ya mafuta inapanda tena.

“Kwa hiyo ndio mazingira tuliyonayo hadi wakimaliza vita (Ukraine na Israel) na kuruhusu mafuta yao kuingia katika soko tutakuwa na nafuu,”amesema.

Kikwete amesema hali hiyo ipo pia kwa mbolea, mafuta ya kula na ngano ambazo wazalishaji wakubwa ndio nchi hizo zinazopigana vita.

Amesema nchi moja tu ni vigumu kutatua, hivyo kunatakiwa kuwe na ushirikiano wa nchi zaidi ya moja.

Amesema hakuna nchi iliyopiga hatua za maendeleo kwa kujifungia yenyewe bila kushirikiana na nchi nyingine.

Aidha, amesema maendeleo ya nchi yoyote ya uchumi huchochewa na matumizi sahihi ya tafiti na ushauri wa kitaalamu, kinyume cha hapo maendeleo ni madogo.

Akizungumza awali, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema sasa ni wakati wa kuwa na kozi fupi za wajasiriamali walioko nchini.

“Tumejiwekea malengo ya kuainisha wajasiriamali wale wanaoanza ndani ya mwaka mmoja tuweze kuwakuza baada ya miaka mitatu waweze kuwa wajasiriamali wa kati na hatimaye tutengeneze wafanyabiashara wakubwa na mabilionea,” amesema.

Amesema wao ndio wanaowafundisha wafanyabiashara wanapaswa kuwaonyesha namna ya kutoka walipo, mahali pa kupata mitaji ili waanzishe biashara.

Dk Kijaji amesema yapo machapisho duniani yanayoonyesha kuwa biashara baada ya miaka mitatu hufa, hivyo kuna kazi ambayo wao kama chuo hawajaifanya kikamilifu.

Naye Mkuu wa Chuo cha CBE, Profesa Edda Luoga amesema tafiti zitakazokuwa bora zaidi katika kongamano hilo wanatarajia zitachapishwa kwenye majarida, kmtandao wa chuo hicho.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo hicho, Profesa Wineaster Anderson amesema wana mpango wa kupanua huduma zake ili kuwafikia walengwa wengi nchini na mipango hiyo inatazama zaidi visiwa vya Zanzibar, mikoa ya Lindi na Iringa.
Wale vipepeo na wale Gt wanaelewa Nini maana ya maneno hayo!!

Kwamba

Mama ameenda kinyume na ushauri fulani fulani hivi na italikost taifa sio au utawala wake au!!?

Ngoja tuone sinema!!!
 
Post yangu #139 uliyo quote mara ya kwanza kule nimesema itakuwa kachukuliwa out of context tu in my opinion alichosema kwenye huo mkutano ili watu watengeneze story za ugomvi ambao haupo.

JK hana sababu ya kulumbana na Samia hadharani watu wote muhimu ambao raisi anashauriana nao ndani ya serikali na kwenye chama ni watu waliokuwa kwenye system ya J.K.

Ukitaka system yako weka wapya, ndio maana Magufuli watu kama kina Lhuwavi aliwatoa nje ya nchi na nafasi za ubalozi, same thing, Samia kapangua Ikulu na kwenye chama watu wa Magufuli kaweka wake.

Be it Samia karudisha watu wa JK Ikulu na kwenye chama sasa sioni sababu ya JK kutaka kulumbana na raisi hadharani wakati logic ni kwamba anapata habari zote za hii serikali hata zile ambazo raisi ana confide to very few individual kuhusu mipango yake.
Usijidanganye mkuu!!

Move ya mama kutaka kugombea na kutaka kutengeneza himaya yake mpya yaan kikosi itakua imeenda out of context!!!
Unakumbuka wakati was JPM Mzee alianza hivi hivi hadi walipoambiwa wanawshwa ndio akatulia!!!?

Ishu ya "operation imesitishwa the state wamesema apewe muda"

Halafu "original plan is on in and out"!maneno hayo yata signal pande zote kuanza kutafutana!

Alikua akimsema jpm!eti watu wanataka mambo mapya na sii ya zamani Yale yale!!!?

Ngoja tuone!!
 
Hata kama Rais hajui kila kitu, lazima awe na uwezo wa kuchanganua mambo ili asidanganywe, tatizo linakuja kama hata huo uwezo wa kuchanganua mambo haupo, hapo inakuwa bora hata huo ushauri wenyewe asipewe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
ZUZU MASHUNGI AKILI ZA KUCHAMBUA MAMBO AZITOE WAPI WAKATI KAPATA CHEO.KWA KWA HISANI YA TOBO ZA CHINI
 
Ushauri wake ni mzuri lakini nikiutazama vizuri nikama anamtishia mtu hivi,

Na nikienda mbele zaidi nikama anatetea kitu ambacho anahofia kuki poteza na anaonyesha yupo tayari hata kiwake inchi nzima
Ila tu asipoteze anacho kihofia kuki poteza

Binafsi naanza kumtafsiri kikwete zaidi ya nnavyo watafsiri umaskini na ujinga kwenye inchi hii

Sina uhakika Ila kikwete nikiumbe wa kuangaliwa Sana kwa nyakayi hizi ambazo mama ameamua kuweka mbele masrahi ya familia kuliko undugu

Let's pray for her

Hii yote umepata kwa kusoma hii taarifa hapa ama ulikuwepo ukumbini ukamuona mpaka lugha ya mwili wakati akiongea?

Hoja yako ni nzito.
 
Naweza kumwelewa JK, CC is supposed to be teamwork.
Makonda is uncontrollable, a stray missile.
Na kwamba alitumika na JPM basi also ni missile isiyo aminika.
Hatujasahau Makonda aliwahi kusema Riz anahusika na madawa ya kulevya!!
Tatizo JK ni mtu anakuambia kitu huku anacheka, lakini deep down tayari anafikiria next step.

Kwanini ninyi viumbe mnalazimisha kuziweka hizi Siasa za nchi hii kibinafsi sana?

Mko way too personal and emotional, kwanini hasa?

Huu uchonganishi unasaidia nini?

Kwanini Rais asiachwe akatimiza wajibu wake kuliko ili mradi hakuna sheria inayovunjwa?

Hii hofu yote ya nini??
 
Back
Top Bottom