Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio rahisi namna hiyo !Naliona anguko la mamake abduli
Sawa kwani ametaja specific Ushauri upi wa maana umepuuzwa?Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema Serikali ikikosa ushauri mzuri ama ikipuuza nchi itakwenda pasipostahili.
Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Novemba 22, 2023 alipokuwa akielezea umuhimu wa makongamano na mikutano katika kuishauri Serikali na Rais, kwenye mkutano wa nne wa Maendeleo ya Biashara na Uchumi ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) ambapo alikuwa mgeni rasmi.
“Ukikosa ushauri mzuri ama ukipata ushauri mzuri ukaupuuza hii nchi itakwenda kusikotakiwa kwenda. Ndio maana makongamano haya ni muhimu sana unachota mawazo,” amesema Kikwete aliyekuwa Rais wa nne wa Tanzania (2005-2015).
Amesema unapokuwa Rais hujui kila kitu lakini unatakiwa kushughulika na kila jambo na kwa sababu huwezi kujua kila kitu inakubidi kutegemea ushauri.
“Wenzako wanakuchagua kwamba unafaa kuwa Rais, lakini utakuwa hujui kila kitu, taaluma yako ni uchumi…lakini ukiwa Serikali na Rais hujui kila kitu. Kwa sababu huwezi kujua kila jambo, lazima utegemee sana ushauri,” amesema.
Amesema ndio maana Rais ana mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, makamishna, wakurugenzi na ofisi binafsi ambayo inawashauri.
Amewataka wasomi hao kutoa ushauri kwa Serikali juu ya mambo mazuri ya kufanya na kile ambacho si kizuri kiachwe na kirekebishwe.
Kikwete amesema uchumi hauwezi kukua bila uwekezaji, na unakuwa mahali ambapo mazingira ya biashara ni rafiki ikiwa vinginevyo wawekezaji wataondoka.
Ametoa mfano wa mfanyabiashara maarufu, marehemu Zacharia Hans Poppe ambaye wakati wa uhai wake alikutana naye nchini Afrika Kusini.
Amesema mfanyabiashara huyo alimweleza amehamishia biashara zake na magari yake yote nchini humo kutokana na mazingira ya biashara kutokaa vizuri nchini.
Amepongeza chuo hicho kwa kuandaa kongamano hilo, lakini akashauri kuangalia uwezekano wakuandaa lingine ambalo litashirikisha taasisi nyingine za elimu za juu.
Kikwete amesema kufanya utafiti ni njia ya kuboresha upeo na maarifa ya kila mtu na itasaidia katika maendeleo ya Taifa.
Bei za mafuta kupanda
Kikwete amesema iwapo bei ya mafuta imepanda katika nchi zinazozalisha ni wazi haiwezi kupungua nchini.
“Namshukuru Rais (Samia Suluhu Hassan) kwa utashi wa kisiasa ameweka ruzuku ya Sh100 bilioni lakini hii inapunguza kwa senti chache. Wakishaweka ruzuku ya Sh100 bilioni bei ya mafuta inapanda tena.
“Kwa hiyo ndio mazingira tuliyonayo hadi wakimaliza vita (Ukraine na Israel) na kuruhusu mafuta yao kuingia katika soko tutakuwa na nafuu,”amesema.
Kikwete amesema hali hiyo ipo pia kwa mbolea, mafuta ya kula na ngano ambazo wazalishaji wakubwa ndio nchi hizo zinazopigana vita.
Amesema nchi moja tu ni vigumu kutatua, hivyo kunatakiwa kuwe na ushirikiano wa nchi zaidi ya moja.
Amesema hakuna nchi iliyopiga hatua za maendeleo kwa kujifungia yenyewe bila kushirikiana na nchi nyingine.
Aidha, amesema maendeleo ya nchi yoyote ya uchumi huchochewa na matumizi sahihi ya tafiti na ushauri wa kitaalamu, kinyume cha hapo maendeleo ni madogo.
Akizungumza awali, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema sasa ni wakati wa kuwa na kozi fupi za wajasiriamali walioko nchini.
“Tumejiwekea malengo ya kuainisha wajasiriamali wale wanaoanza ndani ya mwaka mmoja tuweze kuwakuza baada ya miaka mitatu waweze kuwa wajasiriamali wa kati na hatimaye tutengeneze wafanyabiashara wakubwa na mabilionea,” amesema.
Amesema wao ndio wanaowafundisha wafanyabiashara wanapaswa kuwaonyesha namna ya kutoka walipo, mahali pa kupata mitaji ili waanzishe biashara.
Dk Kijaji amesema yapo machapisho duniani yanayoonyesha kuwa biashara baada ya miaka mitatu hufa, hivyo kuna kazi ambayo wao kama chuo hawajaifanya kikamilifu.
Naye Mkuu wa Chuo cha CBE, Profesa Edda Luoga amesema tafiti zitakazokuwa bora zaidi katika kongamano hilo wanatarajia zitachapishwa kwenye majarida, kmtandao wa chuo hicho.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo hicho, Profesa Wineaster Anderson amesema wana mpango wa kupanua huduma zake ili kuwafikia walengwa wengi nchini na mipango hiyo inatazama zaidi visiwa vya Zanzibar, mikoa ya Lindi na Iringa.
Mzee kamaindi hyo kauli 😁""Ukikosa ushauri mzuri ama ukipata ushauri mzuri ukaupuuza hii nchi itakwenda kusikotakiwa kwenda. Ndio maana makongamano haya ni muhimu sana unachota mawazo,” amesema""
Kwacheo alicho wahi kuwanacho hakuwa na haja ya kuongea maneno kama hayo apo juu.
Makonda alishasemajuzi wastaafu watulie sijui kwanini haeleweki.
Haiwezekani !Kwa taarifa yako hiyo deep state inaundwa na 70% ya watu walio royal kwake.
Mnapenda sana kumtukuza! Yeye ni nani? Lowassa alimshindwa sembuse Samia ako na Urais!Kwa taarifa yako hiyo deep state inaundwa na 70% ya watu walio royal kwake.
Nimecheka sana hii commentKila zama na Kitabu chake
Ikumbukwe Yuda Iskarioti Alikuwa Mshauri wa Yesu kwenye maswala ya Sadaka
Ahhh, ongeza angalau kabusara basi? General Buhari, Joe Biden ni wakubwa kwake lakini wanaongoza nchi.
Kabisa [emoji2957]Huu mwandiko wa Makonda[emoji3][emoji3][emoji3]
Huku anaongea kijana Mzalendo Makonda, Polepole, Heche, Lisu Halafu kule anatokea MTU aliyegawa Vitalu vyote Vya gesi Kwa Wageni Tena Kwa kupitia mtutu Wa Bunduki.Alipokuwa ikulu 2005 to 2015,kulikuwa hakuna Vita ya ukraine wala Israel, na kilimo chetu kilikuwa hovyo, ngsno sukari, nakisi kubwa mpaka kuagiza nje, bei ya mafuta ni kubwa, vigezo vipo vingi, ila Kodi na tozo zinachukua eneo kubwa, taasisi kama ewura,inapata mapato yake kwa kuweka Kodi kwenye kila Lita,
Huyu msoga, alikuja na Sera ya kilimo kwanza, wakaishia kununua magari tu, kilimo Kodi nyingi, mkulima anakufa.
Alipoona ufaulu umepungua shuleni, akaja na u taratibu wake wa kipuuzi na maprofesa wake wa mchongo akashusha pass Mark, ili wafaulu wengi, big result now, matokeo makubwa sasa, siasa ikaingilia utaharamu! Sasa Leo anaongea nini? So pathetic
Umeshawahi kaa na kikwete hata nusu saa ukamsikilizaKwa nchi ambazo zinapima hata maelezo ya mtu tu kabla ya kumpa nafasi ya kugombea urais, Kikwete hakutakiwa kuwa rais.
Tatizo Tanzania hatupimi.
Kikwete anaweza kuwa anaelezea kitu, ukaona kafika katikati ya kukielezea, hajamaliza, halafu kumbe mwenzako ndiyo kashamaliza bila conclusion hapo.
Hata hiyo story ya Zacharia Hans Poppe sijui ni muandishi kafanya uzembe hakuandika conclusion ilikuwa vipi, au ni Kikwete mwenyewe hakutoa conclusion alilifanyia kazi vipi hilo suala.
Ila siwezi kushangaa ikiwa Kikwete katoa story nusu bila conclusion halafu kawaacha watu homework, fill in the blanks.
Ana tabia hiyo sana, halafu ni kama yeye mwenyewe haelewi kwamba amesema mambo in unfinished sentences.
Kikwete ana tabia ya kuongea kama vike watu wote wanaweza kuona anafikiria nini kichwani mwake, hivyo hata asipomalizia sentensi, wataelewa tu kwa kuona mawazo yake.
Unashangaa, huyu kapewaje urais?
Kikwete ndiye owner wa TanzaniaWatu wa hivi hua sio wakuamini kabisa.
Ninanochokiamini uyu mzee hua yupo kimbele mbele kwenye hii nchi sababu ya faida zake, ni tycoon & mafia na hajawahi kua mjinga, so hii kama sio tricky tunachezewa basi ujue mpaka kaongea hivi basi kuna sehemu kaona watu wanamendea ugali wake not otherwise.
Watu tumeona Madereva, nini Makonda.Huu mwandiko wa Makonda😀😀😀
Kwani kumsikiliza Kikwete anavyoongea ni lazima ukae naye hata nusu saa?Umeshawahi kaa na kikwete hata nusu saa ukamsikiliza
Tatizo mnajaji mtu kutokana na mambo ya kisiasa
Mtu ambaye anamfikia mtu yoyote mashuhuri duniani na watu wenye nguvu unamuona kama wewe vile