EL For CCM Chairman 2012 and Eventualy CCM Presidential Candidate for 2015, We believe there is only one in CCM for 2015 and that is Laig'wanani Lowasa
Hilo likitokea basi itakuwa ni uthibitisho tosha kwamba Lowassa ndo mgombea wa urais kupitia CCM. Sina hakika kama JK atakubali hilo lifanyike, ila kwa kuwa aliwekwa na mafisadi, basi ni hao hao ndio wenye uamuzi wa kuendelea kumwacha hapo au kumtoa kabisa.
Mukama na JK wameishanusa hatari ya vua gamba na ndio maana sasa hivi wanaonekana ni kama vile wanaipotezea hoja ya kujivua gamba. Last time Mukama alisema hilo litafanywa na Kamati ya Maadili na Nidhamu, na may be matokeo yake yanaweza kuwa mwezi March na kuendelea. Kwa hiyo tusitegemee chochote mpaka labda baada ya uchaguzi wa ndani ya chama.
Kwa sasa kinachofanyika ni political calculations tu ili kuzuwia damage kwa Mkulu ili asije akapigwa chini uenyekiti au kupigiwa kura ya kuokuwa na imani.
Kuonyesha kwamba JK yuko scared, vikao vya CC siku hizi haviishi kujadili namna ambayo CCM inaweza kuwa independent ili isitegemee mifuko ya mafisadi. Too bad it is too late na sioni anachoweza kufanya maana wajumbe wengi wa NEC walipewa fedha za kifisadi ili kuweza kushinda chaguzi za ndani za chama na hivyo siku zote watabaki kuwa watiifu kwa mafisadi na sio kwa mwenyekiti.
Ninasubiri kwa shauku kubwa sana mabadiliko ya utaratibu wa uchaguzi wa ndani ya chama ili nione kama wataweza kuziba mianya ya mafisadi kuweka watu wao.