Kikwete na Kinana wamtaka Kubenea na MwanaHalisi Kuomba Radhi kwa madai ya kuwalipa wanaopinga Mkataba wa Bandari

Huyu Kubenea aliponea chupuchupu macho yake kupofuka kabisa kwa kumwagiwa tindikal katika awamu ya nne.

Sasa kwa uchokozi huu mwingine kwa watu wale wale, Kubenea anaweza kupumzishwa kabisa.

Mwenyezi Mungu amuepushie mbali asipatwe na mabaya.
 
Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana wamemwandikia Barua Saed Kubenea na Gazeti lake la Mwana Halisi wakimtaka kutimiza madai yao mawili ambayo ni 1. Kufuta Kashfa Dhidi yao na Kuomba Radhi 2. Kuahidi Kuacha Kuwakashifu kutokana na chapisho la kuwahusisha na kupinga Uwekezaji wa Dubai katika Bandari za Tanzania.

Kwa mujibu wa Barua ya Ofisi ya Mawakili ya Eric S. Ng'maryo Advocates, Kubenea na Kampuni yake hiyo wanadaiwa kuchapisha taarifa katika Gazeti Namba 413 Alhamisi ya Julai 20, 2023 mpaka 26 Julai likiwa kashfa zilizoelezwa kuwafedhehesha, kutweza na kuwashushia hadhi viongozi hao.

Aidha, barua hiyo imesema Gazeti la Mwana Halisi limechapisha taarifa kuwa Kikwete na Kinana wamekuwa wakiwalipa watu fedha ili waendelee kupinga uwekezaji wa Bandari.
View attachment 2712977
Same mistake ya dodo, sijui kwanini hatujifunzi.
 
Hawa wazee wanajisafisha kwa umma kupitia gazeti la kibaraka wao Said kubenea

Ni mjinga na mpumbavu tu atakayeamini Rais samia anaweza kufanya mambo haya bila baraka za kikwete na kinana samia hawezi kufanya kitu chochote nchi hii

Samia anaweza kuteua mkuu wa wilaya bila kumuuliza kikwete lkn sio hili la mkataba unaoelekea kuuza nchi kwa waarabu

Tunajua bila kikwete,samia asingekuwa makamo wa Rais
Hawa wazee wanajisafisha ili baadae wawe wamejiwekea kinga ya kutokuhisishwa.

TANGANYIKA inaangamizwa
 
Kama mheshimiwa KIKWETE anapinga Bandari kuanzia leo nimeacha kupinga uwekezeaji wa Bandari
 
Ifike wakati tuzungumze ukweli ,hasa kwenye masuala kama haya ambayo yanagusa wananchi moja kwa moja ,bila kujali utofauti uliopo kati yetu iwe kidini ,kikabila na kiitikadi. Kwanza kabisa lazima kila mtu aelewe kwamba nnachotaka kuzungumza hapa kitu ambacho wengi hawakijui, kiasi kwamba mimi mwenyewe sijui nataka kuongea nini.
Asanteni sana.
Duh
 
Hawa wazee wanajisafisha kwa umma kupitia gazeti la kibaraka wao Said kubenea

Ni mjinga na mpumbavu tu atakayeamini Rais samia anaweza kufanya mambo haya bila baraka za kikwete na kinana samia hawezi kufanya kitu chochote nchi hii

Samia anaweza kuteua mkuu wa wilaya bila kumuuliza kikwete lkn sio hili la mkataba unaoelekea kuuza nchi kwa waarabu

Tunajua bila kikwete,samia asingekuwa makamo wa Rais
Hawa wazee wanajisafisha ili baadae wawe wamejiwekea kinga ya kutokuhisishwa.

TANGANYIKA inaangamizwa
Sukule la wanasiasa uchwara, umekuja kucheua pumba zako ulizomezeshwa na mabwana zako huko porini. Tatizo vijana wengi mnagombania kuwa watumwa wa fikira za wanasiasa uchwara ili mpate viji Like kutoka kwa misukule mingine ya wanasiasa uchwara hao.

Bahati nzuri mods wameufyekelea mbali kwa kuunganisha na uzi wa mtu mungine. Badala ya kutafuta pesa umekalia kuandika majungu kwa wenzako kwa sababu ya kusaka vi Like ambavyo havina faida na wewe kimaisha wala kimaendeleo.
 
JamiiForums576928805_400x298.jpg
 
Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana wamemwandikia Barua Saed Kubenea na Gazeti lake la Mwana Halisi wakimtaka kutimiza madai yao mawili ambayo ni 1. Kufuta Kashfa Dhidi yao na Kuomba Radhi 2. Kuahidi Kuacha Kuwakashifu kutokana na chapisho la kuwahusisha na kupinga Uwekezaji wa Dubai katika Bandari za Tanzania.

Kwa mujibu wa Barua ya Ofisi ya Mawakili ya Eric S. Ng'maryo Advocates, Kubenea na Kampuni yake hiyo wanadaiwa kuchapisha taarifa katika Gazeti Namba 413 Alhamisi ya Julai 20, 2023 mpaka 26 Julai likiwa kashfa zilizoelezwa kuwafedhehesha, kutweza na kuwashushia hadhi viongozi hao.

Aidha, barua hiyo imesema Gazeti la Mwana Halisi limechapisha taarifa kuwa Kikwete na Kinana wamekuwa wakiwalipa watu fedha ili waendelee kupinga uwekezaji wa Bandari.
View attachment 2712977

View attachment 2713071View attachment 2713072View attachment 2713073View attachment 2713074View attachment 2713075View attachment 2713076View attachment 2713077View attachment 2713078
Kuna watu hawana albu, hawa wazee wametajwa sana kashfa nyingi lakini hawana aibu nadhani kiburi cha pesa wanazo miliki na vyeo. Yana mwisho ipo siku mungu atasikia manung'uniko ya wanyonge
 
Yawezekana sana hawa wawili, Kinana na Kikwete ndio makuhani wakuu wa matatizo yanayolikumba taifa hili kwa sasa.
 
Kuna watu hawana albu, hawa wazee wametajwa sana kashfa nyingi lakini hawana aibu nadhani kiburi cha pesa wanazo miliki na vyeo. Yana mwisho ipo siku mungu atasikia manung'uniko ya wanyonge
Hapana, tuachane na sifa hiyo ya "unyonge".

Hii ni nchi yetu, hatuwezi kuwa tunachezewa na watu wapuuzi wa namna hii eti sisi ni wanyonge.

Hawa ni watu wa kuwatia adabu.
 
Aidha, barua hiyo imesema Gazeti la Mwana Halisi limechapisha taarifa kuwa Kikwete na Kinana wamekuwa wakiwalipa watu fedha ili waendelee kupinga uwekezaji wa Bandari.
Hii hapa imekaa sawa kweli, au ni mchanganyiko malum, kama kachumbali?

This does not add up.
 
Kwamba hizi sarakasi zote Kikwete na Mwenzake hawajui nini kinaendelea nyuma ya pazia?
watanzania sio wajinga wa zama zile!
 
Back
Top Bottom