Kikwete: Rais Samia ni kiongozi asiye na papara na ni mtulivu

Na hii ni Moja ya sifa kubwa na sifa adimu sana ndio maana husikii Samia akihemka Wala kupanic Kwa sababu eti ya vimakelele vya wapuuzi huko Nje..

Samia ni Kiongozi sio mtawala kama Jiwe
Uvumilivu ni sifa ya kiongozi bora, habebwi na mihemko ya wakati fulani wala hakamatiki kwa mitego ya kisiasa yenye hisia za muda mfupi.
 
Samia hana papara lile la kusaini mkataba wa hovyo wa bandari hajaliona? au anafaidi pale ndio maana amekuwa kipofu..
Na alitoka hapa dar .na konvyoi ya watu 100 kwa kodi zetu ,bila kushirikisha mwanasheria ndo akaja na huu mkataba eti anafungua nchi.hiyo ni zaidi ya kukurupuka hakika
 
Mh. Rais wetu ana busara sana, ukimsikiliza unaona kabisa kesho yetu iliyobora zaidi ya hapa. Ametibu kelele za madeni ya watumishi, ametibu upungufu wa madarasa, Ametibu value retention fee ya HESLB...niseme tu Asante Dr. SSH Mungu akubariki Sana
 
Huyo Jamaa akubali Enzi zake zilishakwisha na aliharibu. Sasa kama na dadake anataka awe hivyo aendelee kupiga porojo tu
 
Nimefurahi kumuona MZEE wa msoga a.k.a Born in town akiwa na afya timamu na nchi bado inakuhitaji mno. Kanyaga twende JK
 
Na hii ni Moja ya sifa kubwa na sifa adimu sana ndio maana husikii Samia akihemka Wala kupanic Kwa sababu eti ya vimakelele vya wapuuzi huko Nje..

Samia ni Kiongozi sio mtawala kama Jiwe
Mmeshafanikiwa kuweka mwanasesere..

Mshindwe nyinyi tu, baada ya bandari, what next?
 
Kikwete kasema ukweli kabisa. Samia ana utulivu sana. Ni kiongozi hasa maana uongozi ni utulivu
 
Sifa ya utulivu ni muhimu sana kwa kiongozi mkubwa.
Kama Rais akikosa utulivu, atatulizwa na nani kwa katiba yetu hii?
 
Samia hana papara lile la kusaini mkataba wa hovyo wa bandari hajaliona? au anafaidi pale ndio maana amekuwa kipofu..
Hao ndio wenye nchi.
Walitakalo linakuwa, wanaweka viongozi, ukizingua wanakutoa. Hata la bandari washaamua wao litakuwa tu wengine mmeachiwa uhuru wa kupiga mikelele mitandaoni
 
Weh nawe acha kutukoroga
Unajua unachokifanya
Hivi huwa mnatuona hamnazo sana
Hii round Babu zetu wataamka
Tanganyika ni sasa
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anajivunia jinsi Rais Samia Suluhu anavyoongoza nchi kwa utulivu licha ya changamoto anazopitia.

Kikwete ameyasema hayo jioni ya leo julai 18, 2023 jijini Arusha, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Demokrasia Unaoangazia Masuala ya Uongozi barani Afrika, ulioandaliwa na taasisi za MS-TCDC (Tanzania), Center for Strategic Litigation (Tanzania), na Institute for Security Studies (Afrika Kusini).

Amesema kuwa Rais Samia alianza kumvutia kwenye usuluhushi wa mgogoro wa Zanzibar baada ya uchaguzi wa mwaka 2000, ambao alifanikiwa kuuona upeo wake mkubwa katika uongozi baada ya kuwa kwenye kamati moja ya uchaguzi na usuluhishi juu ya mgogoro huo.

Alisema kuwa changamoto mbali mbali anazopitia Rais Samia katika uongozi wake ikiwemo mambo yanayoibuka, angepaniki kidogo tu angevuruga watendaji wake na nchi nzima kwa ujumla lakini utulivu unamsaidia licha ya hasira alizonazo.

"Rais Samia kufanikiwa kufikia leo ni utulivu pekee unamsaidia, maana hakuna nafasi ngumu kama aliyonayo lakini kwa sababu ya utulivu wake ingawa ana hasira lakini mambo yanaenda, hiyo pekee inatosha mimi kujivunia yeye baada ya kumuibua huko Zanzibar na kumleta Muungano," amesema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…