Mbishi 4 real
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 640
- 651
Tunafahamu juhudi za serikali katika kuhakikisha watoto wote wanaotoka katika familia duni wanapata elimu na ndio maana serikali ilisema marufuku michango ya aina yoyote katika shule za serikali.
Hii imekua tofauti katika shule ya msingi Makabe ambapo kumeanzishwa mitihani ya kila weekend na kila weekend watoto wanatakiwa waende na pesa kwaajiri ya kufanya hiyo mitihani.
Kila mtoto mmoja anatakiwa aende na kiasi cha Tshs 1500 hivyo kama una watoto wawili kila kila wiki inabidi uandae Tshs 3000
Kwa mwingine Tshs 1500 ni pesa ndogo sana ila kuna mwingine hiyo pesa kwake ni kubwa sana mana unaweza kuta hana ajira ya kueleweka, sasa awaze kuitafutia familia walau mlo mmoja na wakati huo huo waalimu wanasubiri awapelekee hiyo 1500 kila wiki kwaajiri ya mitihani.
Serikali kupitia wizara husika naamini mpo humu na mtaluona hili andiko langu, naomba mtusaidie mana mtihani ni muhimu lakini hii ya kila wiki tena unatakiwa ulipie kiukweli inatuumiza baadhi yetu ambao hali zetu ni duni sana kwasasa.
Kibaya zaidi mtoto asipoenda kufanya hiyo mitihani weekend kwakukosa pesa Jumaatatu akienda shule wanampiga kwamba kwanini hakuenda.
Naamini serikali yetu ni sikivu sana itaenda kulifanyia kazi hili suala kwa haraka mana ni zaidi ta kero, wao walimu wana mishahara sasa wanadhani kwamba kila mtu anapokea mshahara.
Ahsante
www.jamiiforums.com

Serikali yaweka ukomo michango kujiunga kidato cha tano. Yaelekeza wanafunzi kutokataliwa kisa michango
Serikali imenuia kupunguza mzigo wa gharama za michango kwa wazazi wa wanafunzi wanaojiunga na masomo ya kidato cha tano. Serikali imeweka ukomo wa michango kuwa Sh80,000 kwa shule za bweni na Sh50,000 kwa shule za kutwa. Hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka...