JF tuache ujuaji na kujifanya matajiri. Hivi ninyi mnayajua maisha ya Mtanzania wa kawaida hapa Dar es Salaam?
Mimi nimeshashuhudia visa vingi vya ufukara nikabaki kumshukuru tu Mungu kwa anachonijaalia.
Nakupa mfano, kuna mama alikuja nimuombee cheti cha kuzaliwa cha mwanawe, katika kumdodosa nikagundua huyo mtoto ana pacha wake. Nikamuuliza mbona huyo mwingine hatuombi cheti chake?
Akasema hela hana, na hata shule hamwindikishi sababu hana hela ya kuwapa wote 2 kila siku ya kwenda nayo shuleni. Mtoto 1 anahitaji 1,200/=kila siku ili aende shule (chekechea). Nikamhoji baba watoto yuko wapi? Yupo, lakini kipato chake kidogo, kila siku anaacha nyumbani shilingi elfu 5 tu. Yeye mwenyewe (mama ) ni fundi cherehani, anachopata ndio wanakula na kulipa kodi. Just imagine akiwapa wanawe 2,400 kwenye 5k anabakiwa na 2,600.......
Hii ni real story.
Ndipo tunahoji, hizo tuition na mitihani kila week kwa madarasa yote ni ya nini? Darasa la 1, 2, 3, 5, 6 mitihani ya kazi gani kila week? Wanawatesa wazazi masikini.
Ukishaona mtoto anaenda shule na mfuko, kavaa yeboyebo,shati limebadilika rangi......unatarajia mzazi wake anayo hiyo 1,500?
Njooni huku mitaani mjionee hali halisi za Watanzania. Acheni kutoka Goba unaenda ofisini unapitia bar unarudi nyumbani......