KERO Kila mtoto anatakiwa aende na kiasi cha Tshs 1,500 (Shule ya Msingi Makabe)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
HIZI DILI ZOTEEEEE MAAFISA ELIMU WILAYA WANAZIJUA MNAHISI N MPYA KWAOO YAAN KUNA KIPINDI UKWAMANI NILIWAAMBIA HATA MUENDE WAPII HAWA WATU NAWAHISI WANA MISHAHARA NA HIZI SHULE BADALA YA KUONEKANA WAKIZISIMAMIA SHULE UNAKUTANA NAO UKOOOO......N SHIDA SANA
 
Hiyo shule ipo wilaya gani mkuu??
 

Ama kweli sera za ujamaa ndizo zimeua hii nchi. Kila kitu serikali hutaki kuchukua responsibility yeyote kwa mwanao.

Tsh 1500 kwa wiki no sawa na Tsh 6,000 kwa mwezi, kama mzazi hutaki kugharamia Tsh 6,000 kwa mwezi kwa ajili ya mwanao mwenyewe kusoma na kujiinua hapo mlipo sidhani kama utaweza kusaidika
 
Kwa 1500 tu ulalamike huo ni uchizi kwa mtu anae jua gharama za elimu, na nimefurahi wadau wamemshambulia na amekimbia uzi wake.....watu tuwahamasishe tu.
Awasomeshe kwa gharama kubwa ili baadae waje kuisumbua serikali iwape ajira?
 
Unazaa unashindwa kuhudumia mtoto 1500
Acha ujinga na utahila.

Hao walimu hata wakila hiyo pesa sio mbaya
 
Unakaa wapi ww?
au kwa mzee Ndele
 
Jitahidi sana kuhudhuria vikao vya shule pale vitakapo itishwa
 
Jitahidi san
Jitahidi sana mkuu kutafuta hela




Yaani ongeza sana bidii kwenye utafutaji wa pesa na sio wanawake
 
Hizi habari za ELIMU Bure ni upumbavu tu na kujaribu kuiga vitu tusivyo viweza na matokeo yake ni kuwa na watu (wanaoitwa wataalam ) wenye uwezo duni

How comes kitu Cha thamani kama ELIMU ikatolewa Bure ?

Wote wenye kujua thamani ya ELIMU hawataki kusikia hizo maswala za Bure angalia kama watunga Sheria hizo za ELIMU Bure kama wao wanapeleka wanao huko kwenye Bure, wanajua kinacho endelea kwenye Bure


Anyway pamoja na kwamba umepewa Bure hata ukiambiwa kuchangia kidogo napo hutaki, Sasa ndugu zangu kwani hao watoto ulimzalia nani ?



Unataka watoto uliozaa wewe awajibike nani ?



Swali la ziada pesa unazo tafuta za shughuli Gani kama wanao tu hutaki kuwahudumia na kuwatengenezea future ?
 
Ni bahati mbaya kuzaliwa na mzazi asiyetaka kuwajibika
 
Aisee hii nchi ngumu sana.
Mkuu hao wanafunzi wanaoambiwa waende na 1500 umewaona lakini?kama mwanafunzi anaenda shule na yeboyebo zimechakaa shati limebadilia rangi kabeba mfuko badala ya bag hiyo unadhani mzazi anauwezo wa kuitoa?
 
Ila waTanzania tuna mambi ya ajabu sana, yaani mzazi unakuja kulalamika mwanao kuchangia 1500..!!!
Hii nchi bora tuendelee kutawaliwa na sisiem tu, maana kumbe bado kuna wababa hawajielewi kabisa....🤨
Alafu......
Kwani nani alikulazimisha uzae wakati unaona kabisa bado unamaisha magumu..??
Sasa ungekua unawatoto wanane (8) na wapwa zako wawili (2) na wote wanasoma kama nilivyo mimi sindio ungeikimbia familia kabisa mkuu....☹️
 
1500?😃😃😃😃Hii nchi ngumu sana
Kuongoza nchi kazi sana
 
Wakati mkurugenzi akienda Makabe ampitie mratibu waje Upendo shule ya msingi hapo Mbezi mwisho.
 
Elimu Bure ilikuwa wakati wa mwalimu Nyerere sio leo hii, ukiambiwa elimu Bure usichukulie serious ni maneno na propaganda za siasa na wanasiasa
 
Hii issue ipo shule nyingi hapa Dar ni kama vile wamepeana muongozo ktk vikao vyao vya mkoa na maAfsa elimu
 
Lipeni jambo dogo hilo sana mtihani anafanya mwanao kwa 1500 tu unakuja kulalamika, hizo mentality za ujamaa msipo ziacha utashindwa kuishi katika mfumo wa ubepari.
Hakika! Yaan mtu analalamikia 1,500/=, si uulizie shuleni kama unaona kuna hoja unahitaji kueleweshwa?
 
Hii issue ipo shule nyingi hapa Dar ni kama vile wamepeana muongozo ktk vikao vyao vya mkoa na maAfsa elimu
Acheni ufala serikali hazipeleki mafungu ya kueleweka.
Sasa walimu wasitunge mitihani au watoto wasile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…