KERO Kila mtoto anatakiwa aende na kiasi cha Tshs 1,500 (Shule ya Msingi Makabe)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Walimu wanalengo kubwa sana kukuza elimu japo wazazi tunaona kama wanataka pesa mie mtoto wangu kila siku 500 ya homework ukupiga gharama ya karatasi na muda wa mwalimu wa ziada kusahihisha ni jambo la kujitoa sana.
wazazi tubadilike sio kulalamika
 
JF tuache ujuaji na kujifanya matajiri. Hivi ninyi mnayajua maisha ya Mtanzania wa kawaida hapa Dar es Salaam?
Mimi nimeshashuhudia visa vingi vya ufukara nikabaki kumshukuru tu Mungu kwa anachonijaalia.

Nakupa mfano, kuna mama alikuja nimuombee cheti cha kuzaliwa cha mwanawe, katika kumdodosa nikagundua huyo mtoto ana pacha wake. Nikamuuliza mbona huyo mwingine hatuombi cheti chake?
Akasema hela hana, na hata shule hamwindikishi sababu hana hela ya kuwapa wote 2 kila siku ya kwenda nayo shuleni. Mtoto 1 anahitaji 1,200/=kila siku ili aende shule (chekechea). Nikamhoji baba watoto yuko wapi? Yupo, lakini kipato chake kidogo, kila siku anaacha nyumbani shilingi elfu 5 tu. Yeye mwenyewe (mama ) ni fundi cherehani, anachopata ndio wanakula na kulipa kodi. Just imagine akiwapa wanawe 2,400 kwenye 5k anabakiwa na 2,600.......


Hii ni real story.

Ndipo tunahoji, hizo tuition na mitihani kila week kwa madarasa yote ni ya nini? Darasa la 1, 2, 3, 5, 6 mitihani ya kazi gani kila week? Wanawatesa wazazi masikini.

Ukishaona mtoto anaenda shule na mfuko, kavaa yeboyebo,shati limebadilika rangi......unatarajia mzazi wake anayo hiyo 1,500?

Njooni huku mitaani mjionee hali halisi za Watanzania. Acheni kutoka Goba unaenda ofisini unapitia bar unarudi nyumbani......
 
Mara nying vya bure sio bora
Lakin pia ukwel useme km umeweza kuzaa why ulalamike kuudumia mbona tunapenda kutafta huruma za kijinga sasa km huna uwezo wa kulea na kutunza kwann ufungue surual na kuzaa tuacheni ujinga aisee

Jitu zima linazaa tena watoto weng afu tusomesha unataka usomeshewe na serikal bas toa ata michango midgo midgo km iyo bado ulalalamika
Umasikini ni rahana yan mtu unalalamika kwa mambo ulosababisha ww yan uzae ww afu bado ulalamike kuudumia
 
Acheni ujinga ukizaa ujue na kuhudumia sio kutafta huruma na kusingizia maisha magumu sasa km ni magumu kwann uzae kwann uoe
 
Waelekeze si ndo hawa hawaandai hata kumi mbovu kwa wake zao wanasema kujifungua bure
Hakuna Bure Duniani ,wanakariri maneno ya wanasiasa wanayachukua kama yalivyo matokeo yake wanapata nayo taabu kwelikweli
 
ulivyo malizia iyo stupid teacher plus na limuandiko la herufi kubwa plus humo ndani ki Español ulicho andika maana Sio kiswahili mm uku Sina mbavu aise

NB kabla ujabandika article yako yoyote soma mara mbili kujilizisha

maandishi yako yana ongea personality yako
1 who you are?
2 level of your education
3 what is your character
4 level of respect we should give you
5 standards of living

na mambo kibao soma mara mbili maybe utanielewa na maanisha nn
 
Walimu wa shule za kayumba wamedhidi na hawana utu kabisa, pale secondary ya kawe ukwamani wanawanyima wazazi report za watoto wao kisa hawajatoa elfu tano za walimu wakujitolea,tena wazazi wengine unakuta ni masikini haswa
Swala lakuwa masikini ni sawa na je mtoto niwa nani? Siungi mkono kunyima report ila kama buku5 lipo wape tu sio mbaya...... hawa walimu kazi yao sio mchezo ni ngumu mshahara kiduchu na watoto ni wengi wanajaribu tu kufanya watoto wetu wapende shule na wawe na ufaulu mzuri. Buku5 kwa mtoto hata sio nyingi japo hali inaweza kuwa ngumu ila mjitaidi usirundike watoto wengi uwezo hamna
 
Kama vipi waache kazi wajiajiri, ivyo vimishahara viduchu kuna wengine vitawafaa,,walimu wanachofanya ñikuleta chuki kwa serikali,
 
Kama mwalimu wa shule ya msingi makabe naomba nikujibu kama ifuatavyo.
1. Mzazi naomba uzinduke kutoka usingizini yaani 1500. Unaumia kiasi hiki tena kwa wiki? Tumeamua kufanya hivi ili kuwapa watoto wetu mazoezi ya kutosha kwani hutusaidia sana wanafunzi wetu kufanya vizuri.
2. Nakuleta hesabu hii darasa la tatu wana masomo saba kila somo mtihani wake una karatasi mbili jumla karatai 14 darasa la tano hadi lasaba mitihani yao huwa na karatasi tatu kila somo maana ake 3*6=18 kumbuka kuna kusahihisha na kutoa matokeo je huyu mwalimu anayesahihisha unamuacha vipi bila kummotisha?.
3. Kuna shule kila siku wazazi wao huwapa watoto wao pesa ya kula je wewe huwa una mpa mwanao hata pesa ya kula kweli?.

EWE MLETA MADA NA WATU KAMA WEWE ACHENI ROHO MBAYA DHIDI YA MWALIMU KWANI UNAHISI KABISA KWA 1500 HIYO UNA MNUFAISHA MWALIMU.
ACHA ROHO YA UCHAWI.
 
Hivi Niulize Swali. Je Walimu Wana Posho Wanalipwa Kama Vile Over time Au Extra duty. Kama Hakuna Basi Hivyo Ndivyo Wanavyojilipa. Haiwezekani Mwalimu Anafundishaa Wanafunzi 100 Darasa Moja. Hana Posho Ya Kikao. Over time Hana. Halafu Sekta Zingne Zinajiandikia Posho Za Kutosha.
 
Mzee 3000 ndio unaandika yote hayo tufikie wakati tuchukie vitus vya bure
 
Mkuu bajeti ya Serikali haitoshi kuendesha gharama za matumizi mashuleni hao Walimu wanaowachangisha ni kwafaida yako ww mzazi na watoto wako bila hiyo mitihani ya mara kwa mara Watoto wako hawawezi kupata ufaulu mzuri
 
Jitu kama mwamposa linajilimbikizia tu mali tu limejikausha tu si liwasaidie hata kuwalipia hiyo buku jero hao watoto
 
1500 kwa wiki means kwa mwenzi ni elfu sita 6000

Nadhani mkuu ujitafakari
 
Kama vipi waache kazi wajiajiri, ivyo vimishahara viduchu kuna wengine vitawafaa,,walimu wanachofanya ñikuleta chuki kwa serikali,
Waaache kazi alafu watoto wako nani awasomeshe au wewe ni mwalimu utawasomesha mwenyewe? Tafuta icho kibunda jamaa yangu wape watoto usikubali aibu ndogo ndogo hizi
 
Bure ni ghali kwa kimombo wanasema cheap is very expensive na kuna ukiona elimu ni gharama jaribu ujinga.
Mwisho wa siku utakuja huku kulalamika kanda Fulani inapendelewa mpambanie mwanao kama Mungu kakujalia kidogo. Pia tuzae watoto tunaoweza kuwamudu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…