MrsPablo1
JF-Expert Member
- Jun 9, 2013
- 1,240
- 2,340
Kila mtu anasapport upande wake na hakuna anae taka kukosolewa sio wanao support serikali sio wanaosapoti upinzani ukijaribu kuweka hoja tofauti na upande wowote unaoga mvua ya matusi.
Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali mitandaoni kuhusu masuala ya kisiasa, kama hili la kufungiwa kwa kanisa la Askofu Gwajima na la Lema kuzuiwa kuingia Kenya.
Cha kushangaza na kwa kusema kweli, kinachotia huzuni ni kwamba kila upande, iwe ni wanaounga mkono au wanaopinga, hawataki kabisa kukosolewa.
“Team Support” hawataki hata kusikia hoja tofauti – wao ni kushabikia tu. “Team Pinga” nao ni hivyo hivyo wakikosolewa, ni matusi au kejeli. Kila mtu amejiaminisha kuwa upande wake ni sahihi 100%, na hata tone la maoni tofauti linachukuliwa kama dhambi.
Sasa najiuliza:
Huu ni mjadala wa kisiasa au ni vita ya ushabiki?
Kwa nini tusiwe watu wa hoja badala ya hisia?
Mbona siasa siyo dini? Kiongozi siyo malaika. Na kila upande una mapungufu.
Mfano Halisi: Suala la Gwajima
Wapo waliopinga hatua ya serikali kumfungia kanisa – jambo ambalo ni haki yao kabisa na walipinga kwa hoja.
Lakini waliokuwa wakiunga mkono hatua hiyo walionekana kushabikia tu bila msingi wengine walikuwa na msimamo wa “ni sawa tu afungiwe” bila kuuliza maswali ya msingi kama:
• Je, haki ya kuabudu imezingatiwa?
• Je, taratibu za kisheria zimefuatwa?
• Je, hatua hii inawasiliana vipi na uhuru wa kidini unaolindwa na katiba?
Mwisho wa siku, mjadala ukaishia kuwa ni “Team Support vs Team Pinga” – hakuna hoja kwa wanao support ni hisia tupu.
Halafu Likaibuka Suala la Lema
Mimi kwa mtazamo wangu nilisema, labda Lema alikuwa anataka kutumia mbinu ile ile aliyowahi kutumia awali alipoenda Canada kwanini asingetumia mbinu nyingine
Lakini cha ajabu, nikajikuta nashambuliwa na watu wa “Team NRNE"
Sasa nauliza: Mbona wapinzani nao hawataki kusikia hoja tofauti inshort na wao hawataki kupingwa
Tatizo Sio ku support au Kupinga – Tatizo ni Kukosa Facts pale unapo support au unapo pinga
Tatizo ni namna tunavyofanya hivyo bila hoja, bila takwimu, bila mifano, na bila mantiki.
Hatutaki kusikilizana.
Hatuna uvumilivu wa hoja tofauti.
Tunashindana kwa sauti, jazba, na matusi – badala ya akili, mantiki na heshima.
Leo hii mtu akisema ukweli unaogusa upande fulani, anachukuliwa kama adui. Lakini ukweli unabaki kuwa huu:
Sio kila jambo ni la kupinga, na sio kila jambo ni la kuunga mkono.
Kila tukio linahitaji:
• Kufikiriwa kwa kina
• Kuchambuliwa kwa hoja
• Kuangaliwa kwa jicho la pande zote
Sio kutukana watu mitandaoni kwa sababu “amekosoa upande wangu.”
Wito Wangu
Nitoe wito kwa Watanzania wenzangu:
Tuchangie siasa kwa akili, hoja, na heshima.
Tujenge jamii ya fikra huru, si ya ushabiki usiofikirika.
Tukoseane kwa hoja – siyo kwa matusi.
Tupinge kwa sababu – siyo kwa hasira.
Tusapoti kwa msingi – siyo kwa upofu.
Naomba kuwasilisha.