Kila napoangalia naona kazi ya kutukuka ya Rais Samia, Tunataka nini tena Watanzania ili turidhike?

Kila napoangalia naona kazi ya kutukuka ya Rais Samia, Tunataka nini tena Watanzania ili turidhike?

Unaumwa mavi we,yaani unatuambia amepunguza bei ya mbolea.
Huku wanatupora mashamba hizo mbolea tunapiga huko nyuma kwako?
 
Mimi huwa ndio nashangaa wazungu wao uchumi unaposhuka wanakuwa wazi tu kuwaambia wananchi wao,lakini huku kwetu yaani kila siku utasikia ohoo,uchumi wetu unazidi kuumalika kila siku,huku ukiangalia maisha ya wananchi ndio yanazidi kurudi nyuma!!Walioshiba utawasikia tu mala WB,IMF,wanatupongeza kwa jinsi uchumi unavyokuwa kwa kasi.
Mama yetu Samia Ni mkweli Sana maana mwaka Jana uchumi ulipokuwa mbaya aliwaambia ukweli watumishi wa umma kuwa asingeongeza mishahara mpaka Hali ya uchumi itengemae, akatusihi watanzania wote kufanya kazi kwa bidii na Sasa uchumi unazidi kuimarika
 
unataka tukuanike hadharani bila nguo ?
Acha vitisho vyako hapa, Anika unachotaka, lakini utuambie kwanini miaka yote ya kupokea Ruzuku mmeshindwa kujenga ofisi ya makao makuu? Kwanini mmeanza kukurupuka saiz kwa aibu kuzindua nyumba za watu na kusema Ni ofisi zenu baada ya kupata kiwewe kutokana na ACT kuzindua ofisi zao,wakati nyie hata rangi tu mmeshindwa kupaka hapo ufipa, Tuambie pesa za join the chain zipo wapi? Au nazo mmetafuna?
 
Ndugu zangu Kama ukiacha akili yako iwe huru, ukaondoa mawazo ya uchama kichwani, ukatazama uongozi wa Rais Samia kwa mawazo huru yasiyofungwa na chochote Wala kupofushwa na chuki binafsi kwa Rais Samia, utakubaliana nami kuwa Rais mama Samia kafanikiwa kufanya kazi njema na ya kutukuka katika kila secta na kila eneo linalogusa maisha ya watanzania wanyonge.

Utagundua kuwa Mama Samia kafanikiwa kugusa maisha ya watanzania moja kwa moja, kajenga uchumi unaomgusa mtanzania,utagundua kuwa Mama Samia anaelekeza mamilioni kwa mabillioni ya pesa za kitanzania katika miradi inayogusa na kumnufaisha mtanzania mnyonge katika maisha yake ya kila siku

Mfano ukienda katika kilimo secta iliyobeba kundi kubwa la watanzania unakuta Rais Samia kaelekeza mabillioni ya pesa takribani billioni Mia moja hamsini kama Ruzuku , Hatua hii ya makusudi , kimkakati , kishujaa na kijasiri imepelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni,. Mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa elfu 70 tu, hii imewasha Taa ya Matumaini katika mioyo ya mamilioni ya watanzania wanyonge ambao wanategemea kilimo kuendeshea maisha yao,kwani hatua hii itafanya wakulima kuongeza uzalishaji na hivyo kuinuka kiuchumi na kupunguza umaskini wa Kaya.

Ukija katika Elimu unakuta mh Rais Samia kachukua uamuzi wa kufuta Ada na kufanya Elimu kuwa bure Hadi kidato Cha sita, hatua hii imewafuta machozi na jasho na kuwatua mzigo wazazi wengi waliokuwa wanahangaika kutafuta Ada kwa ajili ya kusomesha watoto wao,lakini pia hatua hii ya mama yetu mpendwa mama Samia imewasha na kuamsha Matumaini kwa wanafunzi wanaotoka katika familia duni nafasi ya Kuendelea na masomo yao bila kikwazo chochote kile,

Lakini pia mama yetu shupavu na Mama wa shoka amehakikisha ujenzi wa shule mpya nchini kwote na ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu nane nchini,Hali iliyopelekea na kutoa nafasi kwa wanafunzi wote wanaofaulu kupata Nafasi ya kwenda shule kwa wakati bila kukaa nyumbani Kama ilivyokuwa zamani ambapo wanafunzi wengine walikuwa wanakwenda muhula wa pili na hivyo kuwa nyuma kimasomo ukilinganisha na wenzao waliotangulia tangia mwezi January.

Ukija katika Afya,Unakuta mama wa shoka kipenzi Cha watanzania Tumaini la wanyonge na chaguo la watanzania Mama Samia ameimarisha Sana secta ya Afya kwa kuhakikisha ujenzi wa zahanati na vituo vya Afya mbalimbali nchini,mfano majuzi hapa takribani vituo vya Afya 234 vimejengwa nchini kwote,lakini pia ameimarisha upatikanaji wa vifaa Tiba , madawa na hata wataalamu wa Afya nchini kwote Kama ambavyo tumeshuhudia utoaji wa ajira za Afya miezi michache iliyopita ambapo zilitoka pamoja na zile za ualimu,

Hatua hii imesaidia na kusogeza huduma Karibu kabisa ya mtanzania na kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma. Lakini pia huduma za kibingwa zinapatikana na hivyo kupunguza zile safari za kupeleka wagonjwa nje ya nchi ambapo watanzania masikini wasio na uwezo wa kupeleka wagonjwa wao nje ya nchi waliishia kuwapoteza na kubaki na majonzi na uchungu mioyoni mwao ya kupoteza wapendwa wao kwa kukosa tu fedha, Sasa Hali Ni ya Matumaini Sana kwetu watanzania kutokana na juhudi za Rais Samia kuimarisha secta ya Afya

Ndugu zangu kila eneo utakalo kwenda iwe Ni suala la demokrasia au usambazaji wa maji, au umeme unakuta Rais Samia kafanya kazi kubwa Sana ya kugusa maisha ya watanzania, Ni ngumu kumaliza yote aliyoyafanya Rais Samia maana hapa patajaa kabisaa

Watanzania tukubali kuwa taifa Letu halitaongozwa na Malaika kwa kuwa hatuna Malaika miongoni Mwetu, Na katika Ubinadamu wake Rais Samia Anastahili pongezi kubwa Sana kutoka kwetu watanzania, Anastahili kuungwa mkono na kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii, Anastahili kuombewa na kila mtanzania ili mwenyezi Mungu amjalie Afya njema na nguvu za kututumikia watanzania.

Watanzania tunataka Nini Tena ambacho Rais Samia hajafanya? Nini ambacho Hakipo katika mipango ya Rais Samia ambacho tunaona kina umuhimu kwetu? Nini na wapi ambako hajagusa kiutendaji? Mimi naona kagusa na kufanyia kazi kila eneo linalo gusa maisha ya mtanzania mnyonge, kila eneo kaweka mkono wake wa upendo na huruma kwa mtanzania mnyonge na kila eneo kalitazama kwa macho ya utayari

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Mkuu
hujagusia ishu ya vitu kupanda bei holelaholela tuu, hujazungumzia ishu ya umeme na maji (kumbuka nchi ili kupata maendeleo thabiti, nishati ni muhimu sana, sasa huezi kuniambia kuwa mama anafanya maendeleo wakati wananchi wake wanakaa tu bila kufanya kazi kwa sababu ya ukosefu wa umeme(hasahasa wajasiriamali wadogo wadogo), mgao wa maji wa kijingajinga tuu!)haya yote huyaoni mkuu??jibu kwa hoja!uchama uweke pembeni
 
Mgao wa umeme umesababishwa na Hali ya ukame inayoendelea hivi Sasa iliyopelekea kupungua kwa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme, hata hivyo juhudi za serikali kupitia TANESCO zinaendelea ikiwepo kutumia mitambo ya gesi kuzalisha umeme ili kupunguza makali,

Lakini pia watanzania Tuendelee kupeana Elimu juu ya utunzaji wa mazingira yetu na vyanzo vyetu vya maji, tusilime kandokando ya vyanzo vya maji Wala kuchoma misitu yetu hovyo
Kipindi cha CHUMA JPM ukame ulikuepo lkn hatukuona mgao wa ovyoovyo na ninakumbuka pale bungeni akitoa hotuba yake alisema kabisa kuwa anajua yanayofanywa na mameneja wa mabwawa!hvo waache mara moja!na hatukusikia mgao wala ujinga ujinga kama wa sasa hvi!
 
Hapana Sina matatizo ya akili
Maandishi yako tu yanaonyesha unaumwa......nenda hospital ya mkoa mtafute daktari au muuguzi anaehusika na kuwahudumia wagonjwa wa akili muelezee hali unayojisikia funguka kila kitu nina imani utapata msaada......pole sana mkuu
 
Maandishi yako tu yanaonyesha unaumwa......nenda hospital ya mkoa mtafute daktari au muuguzi anaehusika na kuwahudumia wagonjwa wa akili muelezee hali unayojisikia funguka kila kitu nina imani utapata msaada......pole sana mkuu
Nakukaribisha kwa mawazo mbadala mkuu yenye Afya njema
 
Back
Top Bottom