Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Rais wa Marekani John F Kennedy amewahi kuwaambia Wamarekani kuwa wasijiulize Marekani itawafanyia Nini Bali Wajiulize Wataifanyia Nini Marekani, Nimeamua kuazima na kukopa maneno hayo kutoka kwa Rais huyo kutoa Rai na Ushauri wangu kwa waheshimiwa Mawaziri wetu walio teuliwa na Rais wetu mpendwa ili wamsaidie katika kututumikia watanzania wanyonge.
Ningependaa kila Waziri katika wizara aliyopo Ajiulize atafanya Nini Wizara aliyopo kuweza kuleta nuru katika mioyo ya watanzania, atafanyi Nini kuleta matumaini kwa watanzania waliokata Tamaa, atachukua hatua gani kutengeneza Daraja la matumaini kwa watanzania walio vunjika moyo, Atafanya Nini kujenga Imani mahali pasipo na Imani, Kila Waziri Ajiulize ni mikakati gani na hatua gani atafanya wizarani pake zitakazo Leta furaha na shangwe kwa watanzania, kila Waziri Ajiulize ni mswaada gani akipeleka Bungeni utaleta Tabasamu mioyoni mwa watanzania.
Napenda kila Waziri katika kila Wizara awe mbunifu,atangulize mbele maslahi ya Taifa, ajuwe cheo Ni dhamana, atambue kuwa uongozi unatoka kwa Mungu pekee, Atambue kuwa anawajibu wa kufanyaa kazi muda wote kwa ajili ya watanzania, awe na wazo moja tu la kuwatumikia watanzania, ajuwe kuwa Ni uchapa kazi na utendaji uliotukuka ndio utakao mpatia heshima kwa watanzania, Atambue kuwa nyota ya kisiasa itawashwa na kazi na siyo pesa Wala mtandao wa matajiri Wala urafiki na wakubwa Wala kumhujumu Rais wako.
Kila Waziri aingie katika mashindano ya kufanya kazi kwa bidii kuwatumikia watanzania na siyo kuvizia ajenda zisizo na mashiko Wala tija kwa mtanzania, kila Waziri Atambue kuwa Wizara yake moja inaweza kubadilisha na kuleta neema katika maisha ya watanzania endapo mikakati mizuri inafanyika, kila Waziri Atambue kuwa anaweza kutengeneza Tanzania iliyo Bora kupitia Wizara yake, kila Waziri Atambue kuwa watanzania wanaweza kuandika jina lake katika mioyo yao kwa wino wa upendo Kama tu atawagusa kwa utumishi wake.
Kama wewe ni Waziri wa Nishati jiulize utafanya Nini ili Tanzania Iwake umeme muda wote, utafanya nini ili kila eneo kuwe mwanga wa umeme, utafanya Nini ili Tanzania isipigwe kelele za jenereta na kushitua wagonjwa wa presha mahospitalini, utafanya Nini ili hata kukitokea ukame Tanzania iendeleee kuwa na mwanga wa umeme, utafanya Nini ili kuwasaidia mamilioni ya vijana wanaotegemea umeme kuendesha shughuli zao, utafanya Nini kuhakikisha hakuna muwekezaji anayesimamisha shughuli za uzalishaji kwa kuwa tu hakuna umeme, utafanya Nini kuhakikisha bidhàa za viwandani hazizalishwi kwa jenereta na kupelekea kupanda kwa Bei ya bidhàa.
Utafanya Nini kumsaidia Rais wetu mpendwa ili kuhakikisha kuwa hata ikitokea kina Cha maji kinapungua nchi haiingia gizani, utafanya Nini kuhakikisha kuwa wananchi wanapewa Taarifa muda wa kukatika umeme,sababu za kukatika umeme na muda wa kurudi umeme ili wajiandae katika kupanga na kufanya shughuli zao, utafanya Nini na mikakati gani kuhakikisha suala la kukatika umeme halijirudii rudii kila mala hasa kutokana na ukame, utafanya mikakati gani ikitokea mvua mwaka huo Ni chache Sanaa,hatua gani za muda mfupi wa Kati na mrefu kusaidia watanzania kupata umeme muda wote? Hayo maswali Ni lazima Waziri Ajiulize na kuyapatia majibu, Ni lazima Waziri awe mwepesi wa kuwaeleza wananchi kila hatua zinazokuwa zinafanywa na serikali yao ili kutotoa mwanya kwa watu wabaya wanao taka kupandikiza chuki kwa wananchi juu ya serikali yao.
Siyo wote wanaopenda mafanikio ya serikali hii ,wapo wanaotamani kuona serikali ikishindwa kufanya kazi, ikikwama ili wapate cha kuongea na Cha kulaumu, wapo wanaotaka kubeba ajenda kuelekea huko tuelekeako, wapo wanao subiri konani ili wapate pa kubania, wapo wanaosubiri mkono uanguke Kama afanyavyo fisi.
Ni wajibu kila Waziri kuhakikisha kuwa anamsaidia mh Rais wetu kufanya kazi hiyo ya kuziba mianya ya wabaya kwa kufanya kazi kwa weledi na kujituma, kujitoa na kujitolea kwa dhati, Asiwepo waziri wa kumhujumu Rais wetu mpendwa, asiwepo Waziri wa kumkwamisha Rais wetu, Asiwepo waziri wakutaka kuonekana yeye anafaa kuliko Rais wetu , lazima kila mtu ajuwe yupo hapo Alipo kwa uteuzi wa Mh mama Samia suluhu Hassani tu na kwamba Hana ukubwa wowote Wala nguvu yoyote mbele ya Rais wetu mpendwa mama Samia, kila Waziri ajuwe Ni Kama Samaki tu ndani ya Maji na akitolewa hapo atasahaulika ndani ya wiki moja na kazi zitaendelea.
Mawaziri lazima wawe mstari wa mbele kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma, lazima wawe ngao ya Rais wetu, lazima wakubali kubeba lawama kwa ajili ya Rais wetu, lazima wakeshe wakifanya kazi ili huduma zifike kwa watanzania, lazima wajuwe mama yetu amewaamini hivyo lazima wafanye kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa Sana, lazima wafanye kwa nguvu zote, lazimaa wamlinde kwa kufanya kazi.
mawaziri wasikubali kujilinganisha na Rais Wala kuhisi wanaweza Urais Wala kuona wanatakiwa kuheshimiwa Kama Rais Wala kupata Tamaa ya Urais Wala kukaa pembeni kuweka mikakatii ya Urais ilihali wanahitajika muda huo kuweka mikakatii ya kuwatumikia watanzania wanyonge wanaohitaji kuhudumiwa na kupata huduma iliyo Bora,anayeona hawezi kufanya hivi Ni Bora ajiengue na kukaa pembeni.
Nitaendelea na Wizara zingine baadaye ili kutowachosha kwa andiko refu.
Kazi iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge.
Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.