Kilangi aweza kuwa ndiye AG mbovu kuliko wote waliowahi kuhudumu nchini Tanzania tangu Wakoloni waondoke

Kilangi aweza kuwa ndiye AG mbovu kuliko wote waliowahi kuhudumu nchini Tanzania tangu Wakoloni waondoke

Kilangi ni "Victim of Circumstances", hii hali inawakumba wote wanaohudumu katika utawala huu kwa sasa. Wanalazimika kucheza muziki wowote unaopigwa na DJ...!!!!

Sasa hivi taasisi zote zimekufa na zimebakia kwenye makaratasi tu, sio ya Kilangi peke yake.

Mwaka 1974 aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda alimwambia aliyekuwa rais Dictator Idi Amin kuwa serikali haikuwa kabisa na fedha ndipo Amin alipomwambia huyo Gavana kuwa:

"Print more money, the governments never go bankrupt because they're the ones who print money, so you just print more money".

Na huyo Gavana alifanya hichohicho alichoagizwa na rais wake na kilichofuata ni historia sasa ila tunakumbuka tuliyokuwepo.

Hivyo watu waoga hufanya kazi kulingana na matakwa ya bosi wao na wala hawawajibiki kufuata matakwa ya taaluma yao au hata weledi ila kwa wenzetu wazungu hili halipo kabisa...!!!!

Miaka ya nyuma wakati dikteta Al Bashir akiitawala Sudan, aliwahi kuamuru watu waliopatikana na hatia kwa makosa ya wizi wapelekwe hospitalini na madaktari wawakate mikono.

Walivyofikishwa hospitalini madaktari walikataa kutii amri hiyo wakidai ilikuwa ni kinyume cha maadili ya taaluma yao kumkamata mtu kiungo bila sababu za kitiba (Without Underlying Medical Grounds) lkn pamoja na kutishiwa kufungwa jela, madaktari walishikilia msimamo wao na kizaazaa kiliisha baada ya nchi za nje kuingilia na madaktari kuachiwa bila masharti.

Hivyo watu wenye misimamo kama madaktari wa Sudan kwa bahati mbaya Tanzania hatunao, tuna watu wanaoona fursa za kuteuliwa kama "Privilege" inayomfanya amuabudu aliyemteua na kusalimisha maadili ya taaluma yake. Tuna safari ndefu sana kuja ku-catch up na wengine.

Idd Amin had the Late Kiwanuka who said no no and Kiwanuka was killed by Amin, God bless you comrade Kiwanuka.
 
06 JUNE 2020
Utawala wa Sheria

Uchambuzi wa Mswada Na. 3 wa Mwaka 2020, mtaalamu wa sheria afafanua

Uchambuzi wa Mswada Na. 3 wa Mwaka 2020 Mei 29, 2020, Bunge la Tanzania limekaribisha wadaua na wananchi kutoa maoni yao kuhusu Mswada Na. 3 unaorekebisha sheria mbalimbali ikwemo Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Kimsingi na Wajibu, 1994 (BRADEA) na Sheria ya Uongozi wa Mahakama namba 4 ya 2011.

Moja ya mambo yanayopendekezwa katika mswada huo wenye lengo la kubadili sheria 13 ni pamoja na kuongezwa kinga ya kisheria kwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, na Jaji Mkuu kutokushitakiwa moja kwa moja na badala yake mashitaka kuelekezwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mapendekezo hayo pia yanapekwenda kuwapa kinga wafanyakazi wa mahakama, ambapo kinga hiyo ikitumika vibaya itapelekea uvunjifu mkubwa wa haki. Tazama uchambuzi huu kisha toa mano yako.

Source : HAKI TV
 
Shukrani sana mkuu
 
Marejeo katika nchi za Commonwealth

Oktoba 22, 2018
Nairobi, Kenya

Jopo lateuliwa kupima mamlaka ya DPP
Na RICHARD MUNGUTI
KATIKA historia ya nchi hii hakuna jaji amewahi kamatwa na kushtakiwa kabla ya kuhojiwa na tume ya kuajiri idara ya mahakama (JSC).

Kesi ya Naibu Jaji Mkuu (DCJ) Mwilu ndiyo ya kwanza kuwahi kufanyika tangu nchi hii ianze kujitawala miaka 55 iliyopita.

Kitendo hiki cha kumtoa DCJ Mwilu ofisini na kumpeleka kortini kimeleta mkinzano mkali kati ya afisi ya raia na idara ya mahakama.

Ndipo mbivu na mbichi zijulikana mamlaka ya utenda kazi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Noordin Haji yamehojiwa na DCJ Mwilu.

DCJ Mwilu anaomba mahakama kuu itafsiri Kifungu nambari 157 cha Katiba kinachompa mamlaka DPP uwezo wa kumfungulia mshukiwa yeyote mashtaka ikiwa amevunja sheria.

Huku akinusa kuwa huenda dau lake likaenda mrama DPP aliwasilisha ombi jopo la majaji zaidi ya mmoja iteuliwe kuamua ikiwa alitumia mamlaka yake vibayana kumshtaki DCJ Mwilu.

DPP anaomba korti iamue iwapo kitendo cha kumshtaki DCJ Ngilu kinagonganisha afisi ya Rais na Idara ya Mahakama.
Afisi ya DPP iko chini ya afisi ya Rais pamoja na afisi ya Mwanasheria mkuu (AG).

DCJ Mwilu, kwa upande wake anasema haki zake binafsi zimekiukwa na kuongeza kuwa idara yote ya mahakama inakabiliwa na tisho la kuvurungwa na afisi ya rais.
aa-6-800x519.jpg
Naibu wa Jaji Mkuu DCJ Philomena Mwilu (kushoto) akiwa naibu wa Gavana wa Makueni Adelina Mwau wakiwa mahakamani. Picha/ Richard Munguti
Kuamua mtafaruku huu Jaji Mkuu (CJ) David Maraga atateua jopo la majaji watatu kusikiza kesi na kubaini ikiwa Bw Haji alitumia vibaya mamlaka ya kwa kunyoosha mkono na kumkamata DCJ Mwilu akiwa katika harakati za kutekeleza majukumu yake ya kikatiba.

DCJ Mwilu amehoji kitendo cha Bw Haji kumkamata na kumfikisha kortini kujibu mashtaka akiwa angali naibu wa CJ na wapili kwa ukuu katika idara ya Mahakama.
Watakapotoa uamuzi iwapo Jaji anayehudumu anaweza kamatwa kiholela na kusukumwa kortini akiwa angali anahudumu.

Swali ambalo jopo la majaji watatu watakalojibu ni ikiwa afisi ya rais inaweza dhulumu idara ya mahakama ambayo ni mojawapo wa vitengo vitatu vinavyojumuisha Serikali.

“Je DPP anahujumu uhuru wa idara ya mahakama na kukaidi sheria zinazoithibiti? ” anahoji DCJ Mwilu.

Katika ushahidi aliowasilisha mahakamani , DCJ Mwilu anasema DPP amekaidi sheria zote kwa kuvuka mipaka na kutwaa mamlaka ya tume ya kuajiri wafanyakazi wa idara ya mahakama (JSC) iliyopewa mamlaka ya kuwaadhibu majaji na mahakimu wanaojihusisha na visa visivyoambatana na mwongozo wa idara ya mahakama.

Kwa mujibu wa sheria JSC ndiyo hupokea malalamishi dhidi ya majaji na mahakimu kisha inawahoji na kutoa maamuzi iwapo wako na makossa au la.

DCJ Mwilu anasema iwapo kuna yeyote aliyedai alikosa ama kukiuka maadili ya kazi ya ujaji , basi angelipeleka malalamiko kwa JSC kisha achunguzwe na ripoti kutolewa kwa Rais Uhuru Kenyatta ateue jopo la kuamua kesi dhidi yake.

Baada ya jopo hilo la rais kutoa uamuzi humpendekezea kinara wa nchi amtimue kazini ama achukuliwe hatua za kisheria.
DCJ Mwilu amesema kupitia kwa mawakili wanaomwakilisha kuwa DPP amekiuka sheria na mwongozo unaofuatwa kumwondoa jaji wanaolindwa kikatiba dhidi ya kutimuliwa ofisini kama makanga.
Wakili James Orengo (kushoto) na Okong’o Omogen (kati) wakiwa kortini. Picha/ Richard Munguti
Wakili James Orengo (kushoto) na Okong’o Omogen (kati) wakiwa kortini. Picha/ Richard Munguti

Jopo atakaloteua CJ litakuwa na kibarua kigumu kwa vile kitaamua iwapo mmoja akipokea mkopo wa Benki na aulipe , makosa ni yapi?

Je ni uhalifu upi mmoja utenda akikopa pesa kutoka kwa benki?

Swali lingine ambalo DCJ Mwilu anauliza ni ikiwa benki iliyomkopesha pesa haijalalamika kwa nini DPP amempeleka mahakamani kumdhulumu.

Pia DCJ Mwilu anahoji ikiwa mahakama ikitoa uamuzi wa kesi waliosikiza na kuamua wanapasa kushtakiwa?

Swali lingine ambalo mawakili Okong’o Omogen, James Orengo, Daniel Maanzo na wengine wasiopungua 1,000 kutoka kwa shirika la wanawake mawakili (FIDA) ni je kuna mtafaruku kati ya afisi ya rais na idara ya mahakama?

Pia majaji wataamua ikiwa uhuru wa majaji umeingiliwa na DPP?

Akipeleka faili hiyo kwa CJ kuteuliwa kwa majaji watakaosikiza kesi ya DCJ Mwilu na DPP, Jaji Enock Chacha Mwita , alisema, “Kesi hii hii inaimbua maswali magumu na nyeti ya kikatiba yanayofaa kusikizwa na kuamuliwa na jaji zaidi ya mmoja.”

Jaji Mwita aliyekuwa ameombwa na DCJ Mwilu kupitia kwa mawakili wake aamue kesi hiyo isikizwe na kuamuliwa na jaji mmoja , alisema “mtazamo wa majaji zaidi ya mmoja hauwezi lingana na wa mmoja.”
Alikubaliana na DPP kuwa kesi ya DCJ Mwilu iko na umuhimu wa kitaifa na ambao utaimarisha ustawishaji wa idara ya mahakama.

Kabla ya kuamuliwa kwa masuala haya , Jaji Mwita aliamuru DCJ Mwilu asifikishwe kortini kujibu mashtaka ambayo DPP alimfungulia.

Source : Jopo lateuliwa kupima mamlaka ya DPP – Taifa Leo
 
Mkuu Mungu akubariki sana kwa wema huu
 
Rejea ya nguvu ya Katiba na DPP katika kufungua mashtaka Tanzania

Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa
By
Mtanzania Digital
-
March 17, 2019

maxresdefault-2-1024x515.jpg

Awaasa wenye siasa za malengo, tamaa Ikulu

NA AZIZA MASOUD-DAR ES SALAAM

JAJI Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inaonyesha kuwa Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kutokana na kile kinachoitwa ‘kinga ya urais’ kuwa na mipaka yake.

Jaji Samatta ambaye amepata kuwa Jaji Mkuu kwa takribani miaka saba kabla hajastaafu mwaka 2007 alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwasilisha mada ya ‘Uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika vyombo vya dola pamoja na utekelezaji wa sheria na utoaji wa haki’ katika kipengele cha wajibu wa Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) na Takukuru kwa wanafunzi wa Shule ya Sheria nchini.

Akiwasilisha mada hiyo katika mkutano wa uwajibikaji ulioandaliwa na taasisi isioyo ya serikali ya Wajibu, Jaji Samatta ambaye amekuwa akisifika kwa misimamo na kusimamia haki alirejea Ibara 46(3) ya Katiba akisema kinga aliyopewa Rais katika ibara hiyo haihusu vitendo Rais alivyovifanya akiwa Rais lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais.

“Ni ukweli kuwa chini ya Katiba ya nchi hii Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka Mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).Ni muhimu sana ukweli huu ukaeleweka.

“Ni sahihi kabisa kusema kuwa chini ya Ibara 46(3) ya sheria mama hiyo rais aliyeacha madaraka ana kinga dhidi ya mashtaka, hata hivyo kinga hiyo ina mipaka. Inahusu tu “jambo …..alilofanya……kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba…..”kinga hii haihusu vitendo alivyofanya Rais akiwa Rais,lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais,”alisema Samatta.

Alisema kuna tofauti kubwa na iliyo wazi kati ya maneno ya ‘akiwa’ na ‘kama’,kwa mujibu wa kifungu hicho cha Katiba aliyekuwa rais hana kinga dhidi ya mashtaka kuhusu jambo lolote ambalo hakufanya kama Rais.

“Kuhusu jambo la aina hiyo Mkurugenzi wa mashtaka ana mamlaka ya kumfungulia mashtaka na mahakama zina mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi hiyo kama ilivyo kwa kesi za jinai zinazoweza kufunguliwa dhidi ya watu wengine nchini.

“Kwa mfano kama alipokuwa madarakani Rais aliamua siku moja kuendesha gari yeye mwenyewe na akamgonga mtu na kusababisha kifo chake kutoakana na uzembe mkubwa kinga chini ya Ibara 46(3) ya Katiba haitamwokoa kutokana kwenye mashtaka ya kitendo hicho,vitendo vya ufisadi navyo vitakosa kinga hiyo,”.

Katika hilo hilo, Jaji Samatta alikwenda mbali na hata kuwaasa wale aliowaita wenye siasa za malengo au tamaa ya kuwa mpangaji Ikulu akiwataka watambue fika kwa faida ya nchi,ukweli huo.

Alisema watawala pia wanapaswa kuzingatia kuwa safari yao ya kuelekea huko na wakati wote watakapoongoza nchi kwenye jumba hilo kwamba ukweli ni kuwa Rais aliye madarakani hana mamlaka ya kutoa msamaha kwa mhalifu yeyote kabla hajapatikana na hatia mbele ya mahakama isipokuwa tu kama ibara ya 45(1) ya Katiba itabadilishwa kumpa mamlaka hayo.

Alisema hakuna shaka yeyote kuwa ofisi ya DPP ni moja ya ofisi kuu muhimu ndani ya dola hivyo jinsi Katiba inavyoelekeza ndivyo inavyopaswa kuwa katika nchi yenye kufuata utawala wa sheria.

“Ofisi ya DPP ikiyumba na utawala huo utatereka vibaya, hilo likitokea hakuna mwananchi ambaye hataathirika kwa namna moja au nyingine, moja ya malengo ya sheria ni kumpa DPP uhuru katika kutumia mamkala yake na kuhakikisha hakuna woga, uonevu au upendeleo katika kuamua mshukiwa ashtakiwe au mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya mtu huyo yafutwe au laa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema utenganisho huo wa mamlaka hayo pia unalenga kuzuia siasa kuingilia au kutumika katika masuala hayo nyeti na kitaalamu.

Alisisitiza kuwa ofisi ya DPP haipo kwa lengo la kuhakikisha kuwa mshukiwa lazima ashitakiwe au mshitakiwa lazima aonekane na hatia.

Alisema DPP na maafisa walio chini yake ni watumishi wa nchi ambao wajibu wao ni kulinda maslahi ya umma yakiwemo yale yanayohitaji mtu asiye onyeshwa na ushahidi kuhusika na utendaji wa kosa la jinai hashtakiwi na mshitakiwa ambaye ushahidi dhidi yake hauthibitishi kwamba alitenda kosa hatiwi hatiani.

Alisema kutumia njia za uonevu na udanganyifu hakuwezi kuyafanya mapambano dhidi ya uhalifu likiwemo kosa la rushwa yafanikiwe kinyume chake hatua hizo zitafanya mapambano dhidi ya uhalifu kutofanikiwa na chuki dhidi ya watawala kujengeka.

“Mwananchi aliyeshitakiwa na kosa la rushwa na inaonekana na mahakama kuwa haijathibitishwa kutenda kosa hilo ana haki ya kuachiliwa ,kama mshitakiwa aliyeshitakiwa na kosa lingine lolote na ushahidi dhidi yake unaposhindwa kulazimisha atiwe hatiani.

“Wakati mwingine siku hizi ninaposikiliza taarifa ya habari kupitia vituo vya televisheni napata picha kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wanateka mamlaka ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, bila shaka yoyote hatua hizo ni kinyume cha Katiba na zinaweza kusababisha viongozi wakahukumiwa kama watafunguliwa kesi za madai mahakamani na kuwalipa wanaonewa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema hatua hizo za watawala zinaweza kusababisha kuharibika kwa kesi ambazo vinginevyo zingeweza kuthibitisha hatia za washtakiwa, uovu huo unaweza kutokea hata kwenye kesi za rushwa na mapambano dhidi ya uovu huo lazima yafanyike kisheria na si vinginevyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa taasisi ya Wajibu ambaye ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh alisema a alisema lengo la taasisi hiyo ni kuongeza ushirikishwa wa wananchi katika suala zima la uwajibikaji.

Alisema aliamua kumualika Jaji Samatta kwakuwa ni mmoja kati ya viongozi waadilifu ambao wanaongea na kutenda vitu ambavyo wanaviamini na kwamba ni miongoni mwa watu wanaochukia rushwa kutoka moyoni.

Alisema mkutano wa jana ambao ni wa tatu baada ya kufanyika mikutano mingine mwishoni mwa mwaka jana katika Chuo Kikuu Dodoma pamoja na Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro ni muendelezo wa kutoa elimu kuhusu uwajibikaji kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Mwisho

Source : Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa |
 
Huu sasa utakuwa ni ujinga kama sio upumbavu, watu baada ya kufanya sana uhalifu wanatafuta njia ya kujilinda.

Lakini kitu wasichokijua ni kuwa hivyo hivyo wanavyobadilisha hizi sheria ili kuwabeba ndivyo zitakavyobadilishwa tena ili wawajibishwe kwa uhalifu walioufanya wakiwa madarakani.

Hii mbinu feki haikuweza kumsaidia Omar Hassan Al Bashir wa Sudan ambaye sasa anakabiliana na wakati mgumu kuwahi kushuhudia katika maisha yake.

All this measures this government is taking are merely temporary that will help the beneficiaries for a short while.
 
Usihangaike Erythrocyte, nakuhakikishia kuwa nafasi zote za uteuzi zilizofanyika baada ya 2016 ni watu wabovu ambao dunia haijapata kushuhudia kutokea Tanzania!
Jaribu kutafuta hata mmoja tuu unitajie ambaye ni bora aliyepo katika ofisi ya umma.
Kumbuka hata uwe mzuri kiasi gani, kama unayaona mabovu kwa nafasi yako hata kunyamaza kwako ni ubovu mkubwa
Mh Bashe je?
 
Huu sasa utakuwa ni ujinga kama sio upumbavu, watu baada ya kufanya sana uhalifu wanatafuta njia ya kujilinda.

Lakini kitu wasichokijua ni kuwa hivyo hivyo wanavyobadilisha hizi sheria ili kuwabeba ndivyo zitakavyobadilishwa tena ili wawajibishwe kwa uhalifu walioufanya wakiwa madarakani.

Hii mbinu feki haikuweza kumsaidia Omar Hassan Al Bashir wa Sudan ambaye sasa anakabiliana na wakati mgumu kuwahi kushuhudia katika maisha yake.

All this measures this government is taking are merely temporary that will help the beneficiaries for a short while.
Swadakta !
 
Kuna Malalamiko kwamba uteuzi wake uligubikwa na uvunjifu mkubwa wa Katiba ya nchi , inasemekana pia hakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa AG baada ya kuokotwa kutoka mahali kusikojulikana , sheria za nchi zinakataza kuokoteza popote AG.

Katika uongozi wa Kilangi ndio mahali sheria nyingi za kijinga zimeletwa bungeni na kupitishwa , ikiwemo hii mpya ya kumlinda "mhalifu" Ndugai asije kufungwa jela mwaka ujao , ni sheria inayoitia aibu nchi bila sababu yoyote ya msingi , kama Mahakama ni yao wanaogopa nini wahalifu wa makusudi kushitakiwa ?

Wachunguzi wa mambo wanaona kwamba pamoja na Mapungufu ya Mh Chenge wakati alipokuwa AG enzi zile lakini rekodi yake imevunjwa na Kilangi .

Ngoja tuone mwisho wake .
HUYU KILANGI ALIKUWA NI HALL WARDEN HUKO ST AGUSTINE UNIVERSITY MWANZA.DAH MZEE BABA AKAMLETA NAHISI WANA UNDUGU NA MZEE MNIKULU THAT Y.
 
HUYU KILANGI ALIKUWA NI HALL WARDEN HUKO ST AGUSTINE UNIVERSITY MWANZA.DAH MZEE BABA AKAMLETA NAHISI WANA UNDUGU NA MZEE MNIKULU THAT Y.
Yawezekana , maana hawezi kupewa cheo kikubwa vile kwa uwezo mdogo alionao
 
Mtemi Chenge ni AG bora kabisa kuwahi kutokea barani Afrika!
Mkuu hata Mimi Mtemi Chenge namkubali sana bahati mbaya yake ni kuwa anaishi Tanzania ambapo watu wake wengi akili zao ni below average hivyo hushindwa kumuelewa Mtemi.
 
Back
Top Bottom