Kilangi ni "Victim of Circumstances", hii hali inawakumba wote wanaohudumu katika utawala huu kwa sasa. Wanalazimika kucheza muziki wowote unaopigwa na DJ...!!!!
Sasa hivi taasisi zote zimekufa na zimebakia kwenye makaratasi tu, sio ya Kilangi peke yake.
Mwaka 1974 aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda alimwambia aliyekuwa rais Dictator Idi Amin kuwa serikali haikuwa kabisa na fedha ndipo Amin alipomwambia huyo Gavana kuwa:
"Print more money, the governments never go bankrupt because they're the ones who print money, so you just print more money".
Na huyo Gavana alifanya hichohicho alichoagizwa na rais wake na kilichofuata ni historia sasa ila tunakumbuka tuliyokuwepo.
Hivyo watu waoga hufanya kazi kulingana na matakwa ya bosi wao na wala hawawajibiki kufuata matakwa ya taaluma yao au hata weledi ila kwa wenzetu wazungu hili halipo kabisa...!!!!
Miaka ya nyuma wakati dikteta Al Bashir akiitawala Sudan, aliwahi kuamuru watu waliopatikana na hatia kwa makosa ya wizi wapelekwe hospitalini na madaktari wawakate mikono.
Walivyofikishwa hospitalini madaktari walikataa kutii amri hiyo wakidai ilikuwa ni kinyume cha maadili ya taaluma yao kumkamata mtu kiungo bila sababu za kitiba (Without Underlying Medical Grounds) lkn pamoja na kutishiwa kufungwa jela, madaktari walishikilia msimamo wao na kizaazaa kiliisha baada ya nchi za nje kuingilia na madaktari kuachiwa bila masharti.
Hivyo watu wenye misimamo kama madaktari wa Sudan kwa bahati mbaya Tanzania hatunao, tuna watu wanaoona fursa za kuteuliwa kama "Privilege" inayomfanya amuabudu aliyemteua na kusalimisha maadili ya taaluma yake. Tuna safari ndefu sana kuja ku-catch up na wengine.