una uhakika iran inasimama yenyewe? iran silaha zake zote ni za urusi unalijua hilo? ebu nitajie silaha ambazo iran imezigundua yenyewe
Tunachojua na kinachojulikana duniani kote ni silaha za Iran kufanya maangamizi makubwa huko Ukraine baada ya Mrusi kumuomba Mu Iran silaha hizo ili zimsaidie kuibomoa ngome ya Ukraine aliyopewa na bwana wake Mmarekani. Hili hata Wamarekani wenyewe, Nato, Ukraine na Umoja wa mataifa walilipigia kelele.
Sasa hilo swala lako unaloandika hapa ni la dhana tu, halina ukweli wala ushahidi wowote. Kwanza unachotakiwa kujua ni kwamba Iran ambayo ilikuwa inajulikana kama Persia hapo zamani, ni moja kati ya nchi zilizokuwa na himaya kubwa kama vile Himaya ya Roma (Roman Empire) Himaya ya Ottoman (Ottoman Empire) sasa ya Iran ilikuwa Persia Empire ambayo ni ya muda mrefu, namaanisha ni ya kale kabla ya kuzaliwa Yesu wala roman empire kuanzishwa. Hivyo hiyo nchi ina historia ndefu mno ya miaka zaidi ya elf 3 kabla hata hiyo Russia haijaundwa. Hata biblia inalitambua taifa la waajemi na utawala wake. Ndiomaana hapo Mashariki ya kati wazungu wote wakishirikiana na hao wayahudi wa mchongo wamekuwa wakipambana usiku na mchana kuidhibiti, lakini wameshindwa.
1. Wameiwekea vikwazo vikali mno vya kiuchumi kwa zaidi ya miaka 50, lakini bado ina uchumi imara zaidi hata ya nchi yako Tanzania.
2. Wameiwekea vikwazo vya kutengeneza, na kununua silaha, lakini bado inatengeneza silaha bora na za kisasa zinazowanyima usingizi wamarekani, waisrael, waingereza nk. Tena anatengeneza silaha za kujilinda na za kuuza kama zinavyouza nchi nyingine. Silaha hizo ndo zilizobadilisha hali ya vita huko Ukraine baada ya waukaine kujifanya wanazijua silaha za Russia, sasa Putin akawaletea chombo ya muajemi ambayo imebadilisha hali ya vita. Sasa waukraine na wamarekani wao wamefyata na kuanza kutumia mbinu za magaidi kuvamia na kuuwa watu kwenye mikusanyiko ya sherehe.
Wamejaribu kuitengenezea maadui wa mchongo kama vile Saudi Arabia nk, lakini leo hii Saudi Arabia na Iran wamepatana baada ya Saudia kushtuka kuwa anaingizwa chaka makusudi na jirani yake ili waje watwangane na Israel na washirika wake wapate pa kuanzia.
Fikiria sasa kama hali hiyo ya vikwazo ingeikuta Israel japo kwa miaka mitano tu, leo hii ingekuaje. Kama nchi inapokea misaada ya kijeshi na silaha kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani nk kila mwaka lakini bado imeendelea kuomba misaada ya kupambana na kakundi ka Hamas ambako hakana meli wala kifaru, je wangekuwa na vikwazo au kunyimwa misaada ya silaha na kijeshi miaka miwili tu si ndo wangechakazwa hata na wavaa misuli wa Houth.
Waajemi sio watu wa kuchezewa kijana. Unatakiwa utumie fikra huru kupima uwezo wa kivita kati ya nchi na nchi.