Kilichojiri Mahakamani Septemba 25, 2026, kesi ya Uhaini Tundu Lissu vs Jamhuri

Maneno yanayofuata: “Who recorded the clip?”

Akiwatafuta Jambo TV walioirekodi hiyo video.

Kwa hayo maneno tu, hiyo video ilichapishwa na Jambo TV.
Kama wewe ungekuwa ni mwanafunzi umekaa darasani mwa huyu mwalimu, kweli ungeshindwa kujuwa/kuelewa jambo lililorahisishwa kiasi hiki kulielewa?

Hata vihiyo kama Tlaatlaah na wenzake wasingeweza kushindwa kuelewa somo la namna hii!

Tundu Lissu angekuwa mwalimu mzuri sana wa sheria.
 
Mahakama ni mahali pa kuelimishana pia.
Na hasa mwalimu akiwa mahili kama alivyo Tundu Antipas Lissu.
Hii kesi litakuwa darasa muhimu sana, siyo kwa wanaohusika na maswala ya sheria pekee, bali hata kwa watu wengine wanaoumizwa na uonevu wa kubambikiziwa kesi.

Na hapo Akili Unde itakapokuwa imetengemaa vizuri, watu wataitumia kutafuta haki zao kwa hizo kesi za uonevu na mchongo.
 
Akili unde itakuwa imesha update memory yaks pia 😃
 
Hakuna sababu yoyote ya kupambania nyuzi, hii kesi ni kubwa mno kuliko waleta nyuzi
Inasikitisha sana hili nalo kuwa jambo la kushindania, nani ataleta taarifa hapa JF.
Kuna mafao/sifa zozote zinazopatikana kwa nani analeta taarifa humu?
 
Nikipandishwa kizmban hata kesho naiman sitakua mbumbumbu wa ishu hizo, hii yote ni kuptia updates zako.
Sitaki kubeza uwezo wako; lakini tambua kuwa hapo kuna kazi kubwa sana iliyofanyika hadi hatua hiyo ya Tundu Lissu kuwasilisha kama alivyofanya..
Siyo kazi nyepesi na inahitaji umakini mkubwa sana.

Ninachoweza kukushauri, tumia muda wako urudi nyuma toka mwanzo kabisa wa haya yaliyowasilishwa humu.
Kwanza kabisa tazama mpangilio wa mawasilisho ulivyo fanyika. Ni mtiririko wa kiufundi mkubwa sana; kuweza kujuwa namna ya sheria inayotumika katika vipengele mbalimbali, na kuona mifano ya kesi zilizofanana na hiyo itakayokuhusu wewe.

Uzuri ni kuwa Akili Unde itakuja kuleta unafuu zaidi, lakini pia itahitaji angalau uwe na uelewa wa kutosha kuhusu taratibu nzima za kimahakama.

Tunaloweza kujifunza kutokana na kesi hii na jinsi Tundu Lissu alivyoitumia kama darasa ni kwamba jambo muhimu katika nyanja yoyote ile ni kujuwa taratibu zake zinavyofanya kazi na ufuate taratibu hizo kimahiri kwelikweli.

Tukifanikiwa kusisitiza hali hiyo katika kila eneo la utendaji, tutapiga hatua mbele haraka zaidi.

Matatizo yetu mengi ni kutofuata taratibu zinavyoelekeza, kila mahali.
 
Akili unde huwa inazunguka mitandao mbalimbali kukusanya taarifa na ndio maana ukiuliza jambo huwa ina search vyanzo mbalimbali na kukupa majibu, huwa inapitia mpaka JamiiForums
Ni zaidi ya hivyo.
Haikusanyi matakataka kama yanayoletwa na akina Tlaatlaah na wengineo.
Ndiyo maana Akili Unde ndiyo teknolojia inayokuja kuleta mabadilko makubwa sana duniani, sawa na kama yale ya "Industrial Revolution", Internet na mengineyo mengi.

Swala muhimu ni kujuwa kuitumia ikupe majibu sahihi na siyo matakataka (Prompting technique).

Siyo kazi ya kutafuta taarifa tu kwa ku'search' mitandao. Inaitwa Akili Unde kwa sababu inao uwezo wa "kutafsiri (inference na ku-reason) kutoa taarifa mpya zaidi ya hizo za kutafuta pekee.

Ndiyo maana italeta manufaa makubwa sana katika ugunduzi, kama wa madawa ya magonjwa mbalimbali.
 
Lakini inategemea ume-Prompt vipi ? Maana nayo huwa inasoma na kiwango cha uelewa wako wa mambo 😃
 

21 September 2026
UJASUSI WA KIDOLA

KESI YA UHAINI ILIVYOSUKWA DHIDI YA MWANASHERIA MKUU CHARLES NJONJO

View: https://m.youtube.com/watch?v=Z2KAVxDZH9wAliyekuwa mwendesha mashtaka mkuu wa Kenya DPP Bw. Sharad Rao aelezea sakata zima la kumtoa Charles Njonjo kumtupa nje ya mfumo wa dola, kisha jinsi vyombo vya mfumo wa dola ulivyomsukia Charles Njonjo kesi ya uhaini ..
 
Manyanza ,

..asante sana kwa HISANI kubwa unayotutendea kwa kutuletea up-dates za kesi ya TL.

..mimi nadhani tunaofuatilia up-dates zako tuko ktk makundi mawili.

..kundi la kwanza, wanapendelea ukipata up-date uiweke pale uzi ulipofikia.

..kundi la pili, ambalo napenda kukiri kuwa nimo humo, tunapendelea up-dates ziwe ktk ukurasa wa kwanza wa uzi wako.

..Nakuomba unapoleta up-dates uyakumbuke makundi hayo mawili na shauku waliyonayo kufuatilia.

..Natanguliza shukurani Mkuu. Tuonane Jumatatu MUNGU akipenda.
 
Mimi huwa naweka kwenye comments, lakini Moderators ndio huwa wanaziunganisha pale kwenye comment ya kwanza
 
..Nadhani ni rahisi kusoma mtiririko wa kesi ikiwa updates zote zitakuwa ukurasa wa kwanza.

..hata mtoa mada angeweza kuwa ana-edit post yake ya kwanza kwa kuongeza updates za kesi.
Hiyo inakuwa na usumbufu kwa wale ambao wapo online kuifuatilie kesi kila hatua unawapa shida waanze Tena kurudi kwenye post alafu hapo hapo wakimbizane na Uzi. Kitu kama hicho kinapaswa kifanywe pale tu usikilizaji wa kesi unapoisha kwa hawakufuatilia ndio unawanganishia kwa pamoja kwenye post Manyanza yupo sahihi
 
Asante mkuu Waufukweni kwa kutuletea madini haya muhimu sana. Tunasubiri update ya Jumatatu tumsikilize Profesa wa sheria Hon Tundu Antipas Mugway Lissu akitema nondo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…