Kilichojiri Mahakamani Septemba 25, 2026, kesi ya Uhaini Tundu Lissu vs Jamhuri

Kilichojiri Mahakamani Septemba 25, 2026, kesi ya Uhaini Tundu Lissu vs Jamhuri

TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1️⃣0️⃣

“I can imagine kwa watu ambao sio wajanja kama mimi sijui wanafanywaje.”

Wanajua sijatenda kosa tangu siku waliponikuwa. Kila mtu anajua hilo.

JAJI NDUNGURU:
“Tuendelee, nimeshaandika.”

🗣️ LISSU:
Kwa hiyo nahitimisha kwa kusema hoja ya sita ni NEGATIVE.

HOJA YA SABA

Waheshimiwa Majaji, hoja ya saba ni:

Je, Serikali ilitishwa na hayo maneno?

Hoja hii inazungumzia matokeo ya nia ya kutenda uhaini chini ya kifungu cha 39(2).

Waheshimiwa Majaji, huwezi kuona hilo katika kesi ya Gray Likungu Mattaka.

Na watu wengi hawajui kwamba kesi ya Gray Likungu Mattaka ndiyo kesi ya Bibi Titi Mohamed.

Bibi Titi Mohamed alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa UWT na mpigania uhuru wa nchi hii.

Ule mtaa unaoitwa Bibi Titi Mohamed umepewa jina lake. Yeye ndiye aliyeshitakiwa kwa uhaini.

Tunaita kesi hiyo Gray Likungu Mattaka kwa sababu ndiye aliyekuwa mshtakiwa namba moja.

Mahakama ni mahali pa kuelimishana pia.

Katika kesi ya Gray Likungu Mattaka, haikufika katika hatua ya intention.

Na ndiyo maana juzi nilisema Mahakama hii ina nafasi ya kuweka historia.

Mahakama hii sasa inaweza kujielekeza katika kifungu cha 10(2).

Kama nia ni kutenda kosa, basi matokeo yaliyokusudiwa kutendwa na nia hiyo lazima yasemwe na yathibitishwe kwa ushahidi.

Waheshimiwa Majaji, kwa maana hiyo, upande wa mashtaka ulitakiwa kuonyesha kwenye hati ya mashtaka, inayotuhumu kwamba kulikuwa na nia ya kuitisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Walitakiwa kuonyesha matokeo ya nia hiyo—Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika au haikutishika.

Na walitakiwa kuonyesha katika Information kwamba, walipokuwa wakileta huo ushahidi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika au haikutishika.

Upande wa mashtaka haukuonyesha hilo kwenye hati yao ya mashtaka (Information).

Walifikiri unarusha mashtaka hivi, litakalompata na limpate.

Hawakubainisha katika mashtaka kwamba:

«“Any particular shown how the Executive of the United Republic has been intimidated.”»

That failure to show the results makes the case defective.

Essentials of the Information must be shown.

Lazima uonyeshe vielelezo vya mashtaka, na usipovionyesha, hati ya mashtaka ni batili.

Siyo tu kwamba hawakuonyesha vielelezo kwenye hati yao ya mashtaka; vilevile hawakuonyesha ushahidi wowote kuhusu jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilivyotishika.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ipo katika Sura ya Pili ya Katiba.

Yote yanaelezea Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaongozwa na Rais.

Ndiyo Kiongozi Mkuu wa Serikali na ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Akipaswa aje atoe ushahidi kama Serikali yake imetishika.

Mimi niliomba aitwe.

Walionishtaki wakapinga vikali, na Waheshimiwa Majaji mkanikubalia.

Mimi, ambaye nilishtakiwa, nilitaka aitwe, lakini hakuna.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Kesi imetumia Trilion zaidi ya 60 ili mtu anyongwe kweli kazi kweli kweli kumbe bora kujinyonga
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1️⃣1️⃣

Mimi nilijua kifungu cha 10(2) kinataka nini, lakini hakuna.

Vilevile, Waheshimiwa Majaji, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ina Makamu wa Rais, na wakati ule alikuwa anaitwa Philip Isdory Mpango.

Mimi niliomba aitwe. Upande wa Serikali ulipinga vikali, kwa hiyo hakukuwa na ushahidi wake, na Waheshimiwa Majaji mliwakubalia.

Mtu wa tatu anayeunda Serikali, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati ule alikuwa anaitwa Majaliwa Majaliwa.

Yeye ndiye Kiongozi Mkuu wa Shughuli za Serikali na Kiongozi wa Bunge.

Mimi niliomba aitwe, lakini mkanikatalia.

Serikali inaundwa na Mawaziri; hakuna hata Waziri mmoja ambaye amekuja.

Serikali inaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini hakuja.

Serikali inaundwa na Mkurugenzi wa Mashtaka, lakini hakuja.

Serikali inaundwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lakini hakuna kiongozi hata mmoja kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyekuja.

Serikali inaundwa na Wakuu wa Vyombo vya Dola, lakini hakuna hata mmoja aliyekuja.

Niliomba afike hapa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi, lakini Serikali ilipinga na Waheshimiwa Majaji mkawakubalia.

Mlinikubalia waje Mkuu wa Majeshi, IGP na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.

Kingai alikuja, lakini alinikatalia kutoa ushahidi.

Kwenye rekodi, hakuna hata mmoja aliyekuja kuthibitisha kama Serikali ilitishika.

Kama Serikali haikutishika, maana yake sina kosa.

Upande wa utetezi hatukuwa na burden yoyote kuthibitisha hili.

Burden ilikuwa kwao, lakini wameshindwa kuthibitisha, na hata kujaribu wameishindwa.

Tuna kesi ya uhaini, na wale wanaosema tumeitisha Serikali hawajajaribu hata kuthibitisha hata Mkuu wa Wilaya fulani.

Waheshimiwa Majaji, hawa nilio wataja kutokufika kwao Mahakamani kuna maana gani?

Maana yake ya kutokumwita ni kwamba walizuia asije, kwa sababu kesi yote imejengwa kwenye misingi ya uongo.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, naiomba Mahakama iseme kwamba wangekuja wangesema ukweli, ndiyo maana hawakuitwa.

More importantly, jibu la swali la saba, Waheshimiwa Majaji, can only be NEGATIVE.

Jibu la swali hili ni:

SERIKALI HAIKUTISHWA.

🗣️ LISSU:
Wangekuwa wametishwa, wangeitwa Mahakamani.

Jibu la hili ni HAPANA, HAWAKUTISHIKA.

Naomba twende mapumziko, tutakuja kuzungumzia masuala mengine.

JAJI NDUNGURU:
“Upande wa mashtaka mnasemaje?”

NASSORO KATUGA:
“Waheshimiwa, hatuna pingamizi, isipokuwa hatujajua ni saa 1 au saa 1 na nusu.

Tuombe Mungu amalize akirudi.”

🗣️ LISSU:
“Saa 1 na nusu, Waheshimiwa Majaji.”

Off the record:
“Ni kwamba nakesha usiku kufanya kazi hii.

Ninapoomba kupumzika kwa saa 1 na nusu, ni ili nipate kupumzisha mwili kidogo.”

JAJI NDUNGURU:
“Kwa mengi hayo hayo, kwa leo tuishia hapa. Tuendelee siku ya Jumatatu saa 3:00 asubuhi.”

🚶🏾‍♂️ MAJAJI WANATOKA.

KESI IMEHAIRISHWA MPAKA JUMATATU SAA 3:00 ASUBUHI.

TUKUTANE JUMATATU ASUBUHI.
 
Hawa JamiiForums wiki hii ya final submissions wamekuwa wana utaratibu tofauti na mimi nauona ni wa hovyo kwa sababu unasumbua Members humu, how come unaitoa updates kwenye comment unaipeleka kwenye uzi wa kwanza, kuna wengine wanakuwa hawazioni updates kwa sababu wanakutana na comments za kawaida tu.

Huu utaratibu nimeanza kuona kwenye huu muda wa Mh Lissu anavyiwasilisha mawasilisho yake. Kwanini wanafanya huu utoto?? Waache kama siku zote. Wanajifanya wana ujuaji mwingi matokeo yake wanaharibu (turejee kwenye App 😂😂😂)

Wapunguze ujuaji bhana wanaboa na watu humu tunafanya kwa mapenzi yetu sio kwa kulipwa
Nadhani walipaswa kutoa taarifa badala ya kufanya kimyakimya, sidhani kama wana nia mbaya
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1️⃣0️⃣

“I can imagine kwa watu ambao sio wajanja kama mimi sijui wanafanywaje.”

Wanajua sijatenda kosa tangu siku waliponikuwa. Kila mtu anajua hilo.

JAJI NDUNGURU:
“Tuendelee, nimeshaandika.”

🗣️ LISSU:
Kwa hiyo nahitimisha kwa kusema hoja ya sita ni NEGATIVE.

HOJA YA SABA

Waheshimiwa Majaji, hoja ya saba ni:

Je, Serikali ilitishwa na hayo maneno?

Hoja hii inazungumzia matokeo ya nia ya kutenda uhaini chini ya kifungu cha 39(2).

Waheshimiwa Majaji, huwezi kuona hilo katika kesi ya Gray Likungu Mattaka.

Na watu wengi hawajui kwamba kesi ya Gray Likungu Mattaka ndiyo kesi ya Bibi Titi Mohamed.

Bibi Titi Mohamed alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa UWT na mpigania uhuru wa nchi hii.

Ule mtaa unaoitwa Bibi Titi Mohamed umepewa jina lake. Yeye ndiye aliyeshitakiwa kwa uhaini.

Tunaita kesi hiyo Gray Likungu Mattaka kwa sababu ndiye aliyekuwa mshtakiwa namba moja.

Mahakama ni mahali pa kuelimishana pia.

Katika kesi ya Gray Likungu Mattaka, haikufika katika hatua ya intention.

Na ndiyo maana juzi nilisema Mahakama hii ina nafasi ya kuweka historia.

Mahakama hii sasa inaweza kujielekeza katika kifungu cha 10(2).

Kama nia ni kutenda kosa, basi matokeo yaliyokusudiwa kutendwa na nia hiyo lazima yasemwe na yathibitishwe kwa ushahidi.

Waheshimiwa Majaji, kwa maana hiyo, upande wa mashtaka ulitakiwa kuonyesha kwenye hati ya mashtaka, inayotuhumu kwamba kulikuwa na nia ya kuitisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Walitakiwa kuonyesha matokeo ya nia hiyo—Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika au haikutishika.

Na walitakiwa kuonyesha katika Information kwamba, walipokuwa wakileta huo ushahidi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika au haikutishika.

Upande wa mashtaka haukuonyesha hilo kwenye hati yao ya mashtaka (Information).

Walifikiri unarusha mashtaka hivi, litakalompata na limpate.

Hawakubainisha katika mashtaka kwamba:

«“Any particular shown how the Executive of the United Republic has been intimidated.”»

That failure to show the results makes the case defective.

Essentials of the Information must be shown.

Lazima uonyeshe vielelezo vya mashtaka, na usipovionyesha, hati ya mashtaka ni batili.

Siyo tu kwamba hawakuonyesha vielelezo kwenye hati yao ya mashtaka; vilevile hawakuonyesha ushahidi wowote kuhusu jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilivyotishika.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ipo katika Sura ya Pili ya Katiba.

Yote yanaelezea Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaongozwa na Rais.

Ndiyo Kiongozi Mkuu wa Serikali na ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Akipaswa aje atoe ushahidi kama Serikali yake imetishika.

Mimi niliomba aitwe.

Walionishtaki wakapinga vikali, na Waheshimiwa Majaji mkanikubalia.

Mimi, ambaye nilishtakiwa, nilitaka aitwe, lakini hakuna.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Hii ndio hoja ambayo inaonekana ndio ingetumiwa na Mawakili wa Serikali kumuangamiza kabisa Lissu kwa sababu kwenye zile vifungu vya kisheria ya makosa ya Uhaini ipo na inaonesha ikitumiwa vizuri Lissu angekutwa na kosa la uhaini tofauti na hoja zingine zote ambazo zipo nje kabisa na uhaini waliomstaki but kwa haya majibu ya Lissu kapangua ile mbaya nimemvulia kabisa kofia huyu jamaa Sheria anajua ile mbaya.
 
Back
Top Bottom