Kilichomkuta rafiki yangu kazini kwake

Safi kwa kumpa ndugu yangu starting point nimependa
 
Siku moja nliaga kazini kwenda kwenye matatizo binafsi ya kifamilia ,kama ilivyo sheria za kazi inaruhusiwa kumbe nmetarget kuiwahi imterview ya shirika moja la kimataifa huko unalipwa kwa umate umate wa dollars 😂, bana kufika kwenye oral interview na mahojiano pap boss wqngu huyu hapa yuko kwenye panel ya wasaili !!, Nilifanya lakini hajawahi niuliza kitu mpaka sasa na maisha yanaendelea , uwoga hautasaidia Kumbukeni ,You have family to feed ,and not community and bosses to impress!
 
😂😂😂😂😂😂😂kaka hukuzimia???
 
Hiyo ofisi sio wazazi wako.... Muda wowote unaweza kuondoka au kuondolewa, kama umeona fursa kwingine omba kazi nenda.

Bosi kununa kidogo ushachachawa
 
Umeandika kama unawaandikia watoto wenzako
Wengine elimu zetu ndogo nisamehe bure nina four ya 39, nashukuru kupitia jukwaa hili nimepata mawazo mazuri sana, mchango wako nitautumia kujifunza kuandika vizuli kaka.
 
Ulifanikiwa kupata huo mchongo? na vipi ulivorudi ofisini kwako ulikuwa una ujasiri wa kupishana na boss wako kwenye makorido
Sikupata ,na uzuri wa haya mashirika ya kimataifa wanakuambia kwa email kwanini hujapata ,Kigezo ilikuwa uzoefu kazini wao huhitaji 7+ yrs’hapo ndio walinizingua na kazini nilirudi kimya namajukum yakaendelea wala sijawahi kuilizwa , nngejibu nlikuwa nasearch green pasture 😁
 
😁😁mambo ya green pasture sio, Big up nimeipenda sana experience yako
 
Kuingia saa moja asubuhi kutoka saa 1 na nusu jioni 🤔
Mambo mengine unafanya saa ngapi mkuu?

Turudi kwenye mada
Kuomba kazi sehemu nyingine sio kosa, kutafuta nafasi nzuri zaidi ni wajibu wake. Aache kuwaza kuhusu boss wake.

Asijisaliti nafsi yake na familia yake kwa kumuogopa boss ambaye nae anaweza kuacha kazi akaende sehemu nyingine au kama ni founder akafungua nyingine na hapo akaacha mwingine.

Kama boss anamuelewa amuongezee msharaha na kumpunguzia masaa ya kazi hayo aweze kufurahia hata huo msharaha 😂😂

Otherwise apige kazi akisikilizia mchongo wake aache kujishtukia.
 

Huyo Bocy hafai
 
hiyo ndio ile dhana uoga wako ndio umaskini wako ndio inamtafuna huyo muungwana.....

nidhamu ya uoga inafanya anakua mtumwa mwa bosi wake, dah umaskini mwingine ni mzigo sana aise.....

wakati wengine tunatuma maombi ya kazi na tunaenda hadi kwa boss atusainie kabisaa ili kuambatanisha na ridhaa ya ofisi kabisa kwenye maombi ya kazi, yeye anaogopa kukutwa tu anatuma maombi, kweli?

uoga gani huo wa kinyonge hivyo? au hana elimu kwamba akitoka hapo hawez kuajiriawa wala kupata kazi kwingine, na hawezi kufanya kitu kingine kumuongezea kipato?

tafadhali sana,
nenda umueleze akamalizie kutuma hiyo application mara moja, mwambie na jana kuna ajira mpya zimetoka asiache kuaply akiwa hapo hapo ofisini, sawa?🐒

Boss akimwambia chochote ananiambie...

na sasa,
nawaombea Baraka na Neema za Mungu katika yote, awaondolee roho ya hofu na nidhamu ya woga, awavishe Roho ya ujasiri na kujiamini katika hali zote daima,
kwa Jina la Baba Mwana na Roho Mtakatifu, Aimen🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…