Kilichompata Andrew Mayalla Baba wa Pascal Mayalla kutoka Kwenye system (Wasiojulikana wanaotambulika)

Kilichompata Andrew Mayalla Baba wa Pascal Mayalla kutoka Kwenye system (Wasiojulikana wanaotambulika)

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Mzee Mayalla, RSO, RPC, DSO na OCD wa Mwanza wote walistaafishwa kwa manufaa ya umma, walihamishwa usiku usiku na kurudishwa kijijini (detention fulani za Nyerere).

Wakati yote haya yakifanyika, bwana Pascal Mayalla alikuwa mdogo sana, hakujua hili wala lile, hadi ilipoanza kuunguruma, Kesi ya mauaji Mwanza, ndipo aligundua nafasi ya baba yake alikuwa nani!, na thanks God, mtu pekee aliyenasuka ni Mzee Andrew Mayalla (RIP) kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na wakili Murtaza Lakha.

Kwa wale tuliofuatilia ile kesi ya Uhaini ya mwaka 1982 tulisoma jinsi TISS wanavyoteka, wanavyotesa na wanavyoua yakiwemo mauaji ya Martin Tamimu. Utekaji wa Hatty Magee, kule jijini Nairobi, etc.

Mahakama ndio Mhimili pekee wa haki ndani ya Katiba yetu, kwenye kesi hiyo ya uhaini, tumeshuhudia watuhumiwa wakitoa ushuhuda jinsi walivyoteswa na TISS kwenye torture chambers zao na kulazimishwa kukiri, hivyo kupelekwa kwa walinzi wa amani kukiri kuhusika kwao halafu walipofika mahakamani wakavikana viapo vyao kwa walinzi wa amani na kusema waliteswa ndio maana wakakiri.

Kila nikisoma maandishi hayo juu nakumbuka pia yaliyomkuta babu yangu ambaye alipata majanga kwa Oder ya Mwalimu Nyerere kuwa lazima ataifishwe.

Mzee Mulokozi amempokea Nyerere katika siasa za Tanzania, ikumbukwe kipindi Ikulu bado iko Bagamoyo mzee huyu alikuwa secretary, wa ikulu ya Wajerumani miaka ya 1919.

Kama unakumbuka Mzee Mulokozi baada ya maaskari kwenda kwenye vita ya pili ya dunia alikaa pale Bagamoyo akapewa bendera 2 na watawala kwamba ukiona meli inakuja ina bendera ya waingereza inyooshe hii ili msiendelee kushambuliwa, ukiona wana ya namna hii ni ya wajerumani basi sisi ndio tutakuwa tumeshinda nyoosha hii ,lakini waingereza ndio walishinda.

Matatizo yaliyomkuta ni makubwa mno na mengine siyo ya kuweka hadharani kwa manufaa ya familia.

Pamoja na kwamba TANU ,CCM kuyafanya hayo sijawahi kuwaza kujiunga upinzani japo mimi siyo CCM,

Upinzani haujaimarika sana mpaka kutushawishi kujiunga.


Pongezi Kwa Pascal Mayalla kukuzwa katika misingi ambayo inaonesha system yetu ilivyo.

Ndo maana chambuzi zako zimejikita katika ukweli na kujua mambo mengi ya Taifa na usalama Kwa ujumla, ndio maana ukipost jambo lazima nipitie kusikia kipi kipya.

Uzi unaweza kuwa wa utani kumbe unawasilisha jambo la maana kutokana na vyanzo vilivokuzunguka.

Kwahiyo kulia lia si vema bila kutafuta suluhisho maana watoto wa Kijitonyama kazi yao ni ya kitambo sana.
 
Wajeruman na ikulu ya Bagamoyo 1945_1960[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Nakosea bwana ilikuwa 1919 lakin wajerumani ndo walikuwapo kabla ya waingereza

Kama unakumbuka Mzee mlokozi baada ya kwenda vita ya pili ya dunia alikaa pale bagamoyo akapewa bendera 2 na watawala kwamba ukiona meli inakuja ina bendera ya waingereza inyooshe hii ili msiendelee kushanbuliwa, ukiona wana ya namna hii ni ya wajerumani basi Sisi ndo tutakuwa tumeshinda nyoosha hii
 
Back
Top Bottom