Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Huyu ni profesa mzuri sana.

Ana-stmulate akili za wanafunz watumie uwezo wao wa kufikirii na siyo kuwa-'spoonfeed'

Unamfungulia kesi mtu kama huyu, amabaye anafanya kazi yake vizuri kabisa. Kichwani mwako utakuwa umejaza madudu.
Tuanze kwanza kumtafuta kwanza huyo mwanachuo mshamba
 
Tuamini tu kweli mhadhiri kakamatwa kwa hizo sababu ulizosema,japo hujatupa ushahidi wowote na umetumia neno 'inasemekana' kwenye taarifa yako
Hiyo ndiyo sababu ya msingi na kuu na ilivyo ni kwamba huyo muhadhiri huwa na ichambua vizuri katiba na madhaifu yake anapo kuwa anawasilisha mada maana anafundisha pia political science , kitu ambacho vijana wa ccm walianza kumuona kama anapingana na serikali ya ya uchawa, ila kuingiza siasa vyuoni kutaharibu sana taaluma yetu kwakweli hii nchi nyerere aliiharibu sana kwa kila kitu kuanzia kiuchumi,kisiasa na hata kijamii nawashangaa sana wanao muona eti nyerere ni shujaa wa taifa sijui kwa lipi yani.wafungue akili zao ndio watajua haya yote tunayo yapitia sasa ni yeye chanzo
 
Habari za chinichini zinapenya kutoka viunga vya UDOM na mitandao ya kijamii kwamba kitu kilichomponza mhadhiri wa UDOM, Dr Kaijage, na kujikuta akipewa kesi ya ugaidi, ni ujasiri wake wa kusimamia taaluma kiuweledi bila kumuogopa mtu yeyote. Habari kamili zinadai wakati mhadhiri huyo akiendelea kufundisha somo la Political Science, mada ya Types of Governments alitoa mfano wa nchi zilizoungana na kutengeneza Union Government, huku akiiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi hizo.

Wahadhiri siku zote ni watu wa facts and evidence. Hawapendi blaablaa! Katika kuthibitisha ukweli wa mambo wanayofundisha, hupenda kufanya citations kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Kwa hiyo, ili kukomelea hoja yake kwamba Tanzania is not a union government, Dr Kaijage alinukuu definition kutoka kwenye kitabu cha Civics cha O-level kama citation hiyo ilivyokuwa highlighted hapo chini (wataalamu mtatusaidia kutambua hiki ni kitabu cha kidato cha ngapi):

View attachment 3651108
Kwa mujibu wa definition ya Union Government, kama ilivyoainishwa hapo juu, Dr Kaijage aliwaambia wanafunzi kwamba Tanzania haimo kwenye orodha hiyo kwa sababu Zanzibar haijapoteza madaraka yake. Yaani, kuna serikali inayoitwa ya Muungano (Union) na pia kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ina mamlaka yake kama nchi ndani ya muungano. Hivyo, aliwaambia wanafunzi kwamba kitabu hiki kilichoandikwa na kuhakikiwa na serikali, kinafundisha uwongo kwa kuwa Tanzania haikidhi vigezo vya kuitwa nchi ya Muungano.

Kana kwamba hilo halitoshi, Dr Kaijage alihamia kwenye kipengele kingine cha Democracy. Katika kipengele hicho alitoa mifano ya serikali ambazo aliziita za kidikteta, na kuitolea mfano Tanzania kama mojawapo ya nchi za kidikteta, hasa kufuatia sintofahamu kwenye chaguzi za 2009, 2020 na 2025. Aidha, alitumia kitabu kimojawapo cha O-level kutoa tafsiri hiyo kama inavyosomeka kwenye kipande kifuatacho:
View attachment 3651110
Kama inavyoonekana, mhadhiri huyo ali-highlight vipande kwenye mafundisho yake ambavyo viliashiria kwamba Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya kidikteta na uvunjivu mkubwa wa haki za binadamu.

Nini kilijiri?
Wakati akiendelea kufundisha, hakujua kuwa alikuwa anarekodiwa na mwanafunzi (chawa) mmoja ndani ya darasa lake. Baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi, mwanafunzi huyo alituma video kwa wakubwa zake kwa ajili ya utekelezaji.

MAONI YANGU
Kitendo cha kumkamata Dr Kaijage na kumkandika kesi ya ugaidi, kitasababisha wahadhiri wengine waogope kufundisha kiuledi na badala yake kufundisha uongo ili tu kuifurahisha serikali. Hata kama mifano aliyotoa haiwafurahishi serikali, sio busara kumpa kesi mbaya kiasi hiki. Kibaya zaidi, inasemekana familia ya Kaijage imekatiwa huduma za maji na umeme na kupelekea familia hiyo kuishi kwa taabu na shida. Hii sio sawa.

Nawasilisha.
​
Mdogo wangu Dr. Kaijage alistahili kukamatwa. Kama msomi wa Political Science alitakiwa kujua kwamba "Political Terms" are relative according to interpretations of different countries where they are used. Mfano, Korea Kaskazini inajiita "Democratic People's Republic of Korea".

Kwa maelezo ya Dr. Kaijage Korea Kaskazini sio "democratic" lakini wao tafsiri ya nchi yao wao ni "democratic"! Dr. Kaijage should've known this better!!
 
Mdogo wangu Dr. Kaijage alistahili kukamatwa. Kama msomi Political Science alitakiwa kujua kwamba "Political Terms" are relative according to interpretations of different countries where they are used. Mfano, Korea Kaskazini inajiita "Democratic People's Republic of Korea".

Kwa maelezo ya Dr. Kaijage Korea Kaskazini sio "democratic" lakini wao tafsiri ya nchi yao wao ni "democratic"! Dr. Kaijage should've known this better!!
Kwa hiyo ulitaka afundishe uwongo ili kuwafurahisha watawala mkuu?
 
Habari za chinichini zinapenya kutoka viunga vya UDOM na mitandao ya kijamii kwamba kitu kilichomponza mhadhiri wa UDOM, Dr Kaijage, na kujikuta akipewa kesi ya ugaidi, ni ujasiri wake wa kusimamia taaluma kiuweledi bila kumuogopa mtu yeyote. Habari kamili zinadai wakati mhadhiri huyo akiendelea kufundisha somo la Political Science, mada ya Types of Governments alitoa mfano wa nchi zilizoungana na kutengeneza Union Government, huku akiiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi hizo.

Wahadhiri siku zote ni watu wa facts and evidence. Hawapendi blaablaa! Katika kuthibitisha ukweli wa mambo wanayofundisha, hupenda kufanya citations kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Kwa hiyo, ili kukomelea hoja yake kwamba Tanzania is not a union government, Dr Kaijage alinukuu definition kutoka kwenye kitabu cha Civics cha O-level kama citation hiyo ilivyokuwa highlighted hapo chini (wataalamu mtatusaidia kutambua hiki ni kitabu cha kidato cha ngapi):

View attachment 3651108
Kwa mujibu wa definition ya Union Government, kama ilivyoainishwa hapo juu, Dr Kaijage aliwaambia wanafunzi kwamba Tanzania haimo kwenye orodha hiyo kwa sababu Zanzibar haijapoteza madaraka yake. Yaani, kuna serikali inayoitwa ya Muungano (Union) na pia kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ina mamlaka yake kama nchi ndani ya muungano. Hivyo, aliwaambia wanafunzi kwamba kitabu hiki kilichoandikwa na kuhakikiwa na serikali, kinafundisha uwongo kwa kuwa Tanzania haikidhi vigezo vya kuitwa nchi ya Muungano.

Kana kwamba hilo halitoshi, Dr Kaijage alihamia kwenye kipengele kingine cha Democracy. Katika kipengele hicho alitoa mifano ya serikali ambazo aliziita za kidikteta, na kuitolea mfano Tanzania kama mojawapo ya nchi za kidikteta, hasa kufuatia sintofahamu kwenye chaguzi za 2009, 2020 na 2025. Aidha, alitumia kitabu kimojawapo cha O-level kutoa tafsiri hiyo kama inavyosomeka kwenye kipande kifuatacho:
View attachment 3651110
Kama inavyoonekana, mhadhiri huyo ali-highlight vipande kwenye mafundisho yake ambavyo viliashiria kwamba Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya kidikteta na uvunjivu mkubwa wa haki za binadamu.

Nini kilijiri?
Wakati akiendelea kufundisha, hakujua kuwa alikuwa anarekodiwa na mwanafunzi (chawa) mmoja ndani ya darasa lake. Baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi, mwanafunzi huyo alituma video kwa wakubwa zake kwa ajili ya utekelezaji.

MAONI YANGU
Kitendo cha kumkamata Dr Kaijage na kumkandika kesi ya ugaidi, kitasababisha wahadhiri wengine waogope kufundisha kiuledi na badala yake kufundisha uongo ili tu kuifurahisha serikali. Hata kama mifano aliyotoa haiwafurahishi serikali, sio busara kumpa kesi mbaya kiasi hiki. Kibaya zaidi, inasemekana familia ya Kaijage imekatiwa huduma za maji na umeme na kupelekea familia hiyo kuishi kwa taabu na shida. Hii sio sawa.

Nawasilisha.
​
Serikali imefanya vizuri sana, kwanza nashangaa mnamwita huyo bwege mhadhiri, huyo ni mpotoshaji,
kuhusu muungano angeeleza aina za union zilizopo duniani. Kuhusu muungano wetu baba wa Taifa aliekeza wazi kwamba muungano wetu ni wa kipekee hapa duniani na alieleza kwanini waliamua aina ya muungano wetu, kubwa aliogopa Zanzibar kumezwa na kupotezwa kabisa utambulisho wake ukizingatia tayari ilishakuwa nchi huru, ingemezwa kwa kuwa ilikuwa na idadi ndogo sana kijiografia na ilikuwa na watu wachache sana.
Vile vile miungano mingi inaitwa shirikisho ina miundo tofauti kabisa. Hata hivyo muundo wa muungano unaweza kurekebishwa kulingana na wakati kwa njia ya maridhiano ya pande zote 2.
Kuhusu demokrasia, kuiita nchi yetu ya kidikteta ni utovu mkubwa wa nidhamu, ni mwehu tu, msaliti, mtu asiye raia au asiye mzalendo aliye kibaraka anaweza kuwa na ujasiri wa kusema hayo maneno.
Nchi yetu ilifanya uchaguzi mkuu uliofuata taratibu zote, vyama 18 vilishiriki, chama kimoja kilijitoa kwa sababu zake. Kwamba huyo mhadhiri uchwara kuwa mfuasi wa hicho chama ndiyo atumie madarasa yetu kupotosha vijana wetu? Achochee vurugu kisa uhuru wa kitaaluma? Huyo bwana achunguzwe vizuri inawezekana siyo raia wa nchi yetu ukizingatia ametokea mkoa wa mpakani, serikali iwe makini ktk ajira nchi km Rwanda ni hatari sana kwa ustawi wa nchi yetu.
Kingine serikali iandae utaratibu wa kuwapa leseni wahadhiri wetu ili mtu mpuuzi km huyo asije kufundisha hata taasisi binafsi, mshenzi huyo hatufai Tanzania, nchi yetu ina tamaduni na desturi zake hatupangiwi na mtu yeyote, ndiyo maana ya uhuru wetu.
Demokrasia definition yake siyo moja, inaendana na muktadha na tamaduni na desturi ya jamii husika.
Kwa maana ya demokrasia ya huyo mhadhiri China ni nchi ya kidikteta? Maana tangia uhuru wake mwaka 1949 mpaka sasa inaongozwa na chama kimoja cha CPC na ni ya pili kwa maendeleo duniani.
Chadema watafute mbinu nyingine si hii siasa za kishamba, za kitapeli, za majitaka kukimbia chaguzi na baada ya uchaguzi waje na propaganda kuwa uchaguzi haukufanyika, mara serikali ya kidikteta, wasitake kuendesha nchi kwa matakwa yao.
Walishashiriki chaguzi nyingi hawakushinda, uchaguzi wa 2015 walipata ushindi mkubwa kwasababu ya Lowassa na wafuasi wake. 2020 walishiriki hawakuambulia chochote, chadema ya sasa hivi dhaifu sana kuliko ya wakati mwingine wowote ule. Upinzani wa kweli nchi hii utatokea CCM ikigawanyika km ilivyotokea 2015, si hii chadema ya kususia chaguzi, chadema ya matusi, chadema ya uchochezi na upotoshaji. HIYO NI BIG NO! MHADHIRI achunguzwe vizuri uraia wake!
 
Nadhani ndivyo walivyokubaliana waasisi kulingana na hali zetu navyofikiri.

Maana muungano wetu ni replica ya ule wa UK.

UK wana articles of Union hata sisi tunazo.

Ila namna wanavyofanya mambo yao ni tofauti kidogo na sisi.

Mimi naona mfumo huu ni sawa tu kwakuwa ndio umesaidia kulinda Muungano mpaka sasa hivi.

Kama serikali ya Tanganyika ingekuwepo Muungano ingekuwa rahisi kuvunjika.
Hivi unajua kwamba kule Zanzibar kuna jimbo la uchaguzi lina watu pungufu ya 1,000 lakini lina mbunge anayehudukiwa na serikali ya Tanganyika sawa na mbunge anayewakilisha mamilioni ya wananchi?
Hivi unajua kuwa Mtanganyika yeyote akifika Zanzibar anabaguliwa wazi wazi tofauti na Mzanzibari akifika Tanganyika?
 
Serikali imefanya vizuri sana, kwanza nashangaa mnamwita huyo bwege mhadhiri, huyo ni mpotoshaji, kuhusu muungano angeeleza aina za union zilizopo duniani. Kuhusu muungano wetu baba wa Taifa aliekeza wazi kwamba muungano wetu ni wa kipekee hapa duniani na alieleza kwanini waliamua aina ya muungano wetu, kubwa aliogopa Zanzibar kumezwa na kupotezwa kabisa utambulisho wake ukizingatia tayari ikishakuwa nchi huru, ingemezwa kwa kuwa ilikuwa ndogo sana kijiografia na ilikuwa na watu wachache sana. Vile vile miungano mingi inaitwa shirikisho ina miundo tofauti kabisa. Hata hivyo nuundo wa muungano unaweza kurekebishwa kulingana na wakati kwa njia ya maridhiano ya pande zote 2. Kuhusu demokrasia, kuiita nchi yetu ya kudikteta ni utovu mkubwa wa nidhamu, ni mwehu tu, msaliti, mtu asiye raia au asiye mzalendo aliye kubaraka anaweza kuwa na ujasiri wa kusema hayo maneno. Nchi yetu ilifanya uchaguzi mkuu uliofuata taratibu zote, vyama 18 vilishiriki, chama kimoja kilijitoa kwa sababu zake. Kwamba huyo mhadhiri uchwara kuwa mfuasi wa hicho chama ndiyo atumie madarasa yetu kupotosha vijana wetu? Achochee vurugu kisa uhuru wa kitaaluma? Huyo bwana achunguzwe vizuri inawezekana siyo raia wa nchi yetu ukizingatia ametokea mkoa wa mpakani, serikali iwe makini ktk ajira nchi km Rwanda ni hatari sana kwa ustawi wa nchi yetu. Kwanza serikali iandae utaratibu wa kuwapa leseni wahadhiri wetu ili mtu mpuuzi km huyo asije kufundisha hata taasisi binafsi, mshenzi huyo hatufai Tanzania, nchi yetu ina utamaduni na desturi zake hatupangiwi na mtu yeyote, ndiyo maana ya uhuru wetu. Demokrasia definition yake siyo moja hapa duniani inaendana na muktadha na tamaduni na desturi ya jamii husika. Kwa hiyo China ni nchi ya kidikteta? Maana tangia uhuru mwaka 1949 mpaka sasa inaongozwa na chama kimoja cha CPC na ni ya pili kwa maendeleo duniani. Chadema watafute mbinu nyingine si hii siasa za kishamba, za kitapeli, za majitaka kukimbia uchaguzi na baada ya uchaguzi waje na propaganda kuwa uchaguzi haukufanyika, mara mara ya kidikteta, wasitake kuendesha nchi kwa matakwa yao. Walishashiriki chaguzi nyingi hawakushinda, uchaguzi wa 2015 walipata ushindi mkubwa kwasababu ya Lowassa na wafuasi wake. 2020 waliashiriki hawakuambulia chochote, chadema ya sasa hivi dhaifu sana kuliko ya wakati mwingine wowote ule. Upinzani wa kweli nchi hii utatokea CCM ikigawanyika km ilivyotokea 2015, si hii chadema ya kususia chaguzi, chadema ya matusi, chadema ya uchochezi na upotoshaji. HIYO NI BIG NO! MHADHIRI achunguzwe vizuri uraia wake!
Mkuu ulienda shule kweli? Hebu nenda shule walimu wakufundishe jinsi ya kuandika INSHA.
 
Kwa kawaida binadamu anapokuwa kwenye matatizo na kwenye magumu, watu wenye roho za ubinaadamu, na utu, wanaumizwa na anayopitia, lakini watu wenye roho za kishetani, wanazidi kuchochea moto!, bandiko hili ni adding an insult to an injury!, kuna watu, mnajichumia laana bila kujijua kwa kumsingizia uongo kama, huu uliouleta hapa ili aonekane ni lecture kilaza!,

Kuna aina kuu tatu za miungano ya nchi,
  1. Muungano wa Union na kuunda a unitary gornment kwa kuunda union, nchi mbili au zaidi zinaungana kwa union na kuunda nchi noja. Hizi nchi zote zinapoteza its sovereignty na nchi mpya ya union. Kama GBRT.
  2. Muungano wa Federation, nchi moja au zaidi zinaungana kwenye baadhi tuu ya mambo, kunakuwa na federal government, lakini kila states inakuwa na utawala wake wa mambo yake ya ndani, kama US.
  3. Muungano wa Confederation, kama Ujerumani,
Muungano wa Tanzania na Zanzibar, ni muungano adhimu na adimu.
Kimataifa ni muungano wetu ni muungano wa Union, nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar zimeungana kwa union, kuunda nchi moja ya JMT, nchi zote mbili zimepoteza sovereignty zake na JMT ndio the new sovereign.

Lakini ndani ya muungano, JMT ni moja ya JMT yenye muungano wa federation ya nchi mbili, nchi mama ya JMT, na nchi mtoto ya Zanzibar yenye utawala wake wa ndani, lakini hauna sovereignty. Kimaifa Tanzania ni nchi moja tuu, Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani kama ilivyo Kwazulu Natal kwa Chief Mangosotho Buthelezi,

Kitendo cha kumsingizia uongo mtu aliyeko matatzoni ni kujichumia laana za bure bila wewe kujijua!.

P.
Ubarikiwe kuchangia hiki kidogo hata sindano ni tone na huponya mgonjwa! Zanzibar ingekuwa nchi ingekuwa na kiti chake umoja wa mataifa, ingekuwa inaweza kukopa yenyewe km nchi kutoka mifuko ya kimataifa km World Bank, IMF, ingekuwa mwanachama wa mashirika ya kimataifa.
Zanzibar haina wizara ya Ulinzi, Mambo ya ndani, Mambo ya Nje, Elimu, hizi wizara ni roho ya nchi bado mnasema ni nchi kamili mlitaka i-surrende nini zaidi na hayo ni baadhi tu!
Huyo mbwa hata akitoka asiruhusiwe kufundisha tena popote Tanzania, huyo ni kibaraka na adui wa Taifa hasa ktk sekta ya elimu, hata wale wahadhiri wapumbavu wanaomtetea na kutaka kuleta upuuzi wapewe onyo kali km hawatii fukuza kazi! Hatuwezi kufanya siasa za kipuuzi km hizo ili tu mtu aingie madarakani.
Hii serikali km inafikiri inaweza kuiridhisha chadema kwa lolote inajidanganya, kitu pekee kitakachowaridhisha ni kuingia Ikulu kwa njia yoyote ile.
Huyo Kaijage siyo raia wa nchi yetu achunguzwe vizuri na afukuzwe arudi huko kwao, nchi ilindwe kwa nguvu kubwa sana angalieni Sudan imesambaratika, je kuna umoja wa Ulaya, Bunge la Ulaya, Bunge la Marekani au kima mwingine yoyote anatoa msaada? Hata wanaizungumzia? Ni sawa na mwanamke aliye kwenye ndoa anavyosumbuliwa kwa kutongozwa ila siku akiachika hakuna anayetaka hata kumsalimia.
 
Kwa kawaida binadamu anapokuwa kwenye matatizo na kwenye magumu, watu wenye roho za ubinaadamu, na utu, wanaumizwa na anayopitia, lakini watu wenye roho za kishetani, wanazidi kuchochea moto!, bandiko hili ni adding an insult to an injury!, kuna watu, mnajichumia laana bila kujijua kwa kumsingizia uongo kama, huu uliouleta hapa ili aonekane ni lecture kilaza!,

Kuna aina kuu tatu za miungano ya nchi,
  1. Muungano wa Union na kuunda a unitary gornment kwa kuunda union, nchi mbili au zaidi zinaungana kwa union na kuunda nchi noja. Hizi nchi zote zinapoteza its sovereignty na nchi mpya ya union. Kama GBRT.
  2. Muungano wa Federation, nchi moja au zaidi zinaungana kwenye baadhi tuu ya mambo, kunakuwa na federal government, lakini kila states inakuwa na utawala wake wa mambo yake ya ndani, kama US.
  3. Muungano wa Confederation, kama Ujerumani,
Muungano wa Tanzania na Zanzibar, ni muungano adhimu na adimu.
Kimataifa ni muungano wetu ni muungano wa Union, nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar zimeungana kwa union, kuunda nchi moja ya JMT, nchi zote mbili zimepoteza sovereignty zake na JMT ndio the new sovereign.

Lakini ndani ya muungano, JMT ni moja ya JMT yenye muungano wa federation ya nchi mbili, nchi mama ya JMT, na nchi mtoto ya Zanzibar yenye utawala wake wa ndani, lakini hauna sovereignty. Kimaifa Tanzania ni nchi moja tuu, Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani kama ilivyo Kwazulu Natal kwa Chief Mangosotho Buthelezi,

Kitendo cha kumsingizia uongo mtu aliyeko matatzoni ni kujichumia laana za bure bila wewe kujijua!.

P.
Wewe umeamua kututukana sisi wanzazibari kwamba zanzibar sio nchi walah omba toba nyie vichogo ni madhurumati sana.. ila safari hii tutawanyoosha..
 
Back
Top Bottom