Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Kwa muono wangu nashauri tupewe kama Zanzibar walivyopewa na raisi wa muungano atoke Zanzibar
Nasi tuwe na wawakilishi kama hivi sasa na pia gharama za muungano ibebe Zanzibar hata kwa miaka kumi tu
 
Hakuweka interpretation wala translation bali alicheza kwenye definition ileile iliyomo kwenye vitabu hivyo na kusaidia kuondoa upotoshaji wa muda mrefu. Hebu kwanza pitia definitions hizo hapo juu ujiridhishe mkuu.
Kwa nini asitunge cha kwake chenye hizo interpretation zake!
 
Kama alisema kuna Tanzania haina Union Government anapotosha


Zanzibar haina total sovereignty.

Mamlaka yake ni kwa mambo ya ndani tu ila inapokuja kwa maswala ya nje yanayoliwasilisha Taifa yale mambo yanayotambulisha Taifa yamebakia kwa serikali ya JMT.
Lakini hapo bado kuna utata.
Baada ya huo muungano kwa nini jina la Zanzibar limeendelea kuwepo lakini jina la Tanganyika limekufa?
 
Bila muungano huu nyinyi mnataka kuuchezea kisiasa

Nawaambia kutatokea mgogoro mzito na kile leo mnakiita Sijui Tanganyika mjue kinaenda Sambaratika muda
mfupi sana✍️
 
Anataka kuingia kwenye list ya mashujaa?

Wale 16 wa mwanzo wa TANU wenyewe, walioanzisha na kuibeba TANU hawatambuliwi officially mpaka Leo

Kuwa shujaa kunahitaji moyo
 
Muungano wetu ni unique, kwa upande ni union na kwa upande ni federation, ndio maana tunauita muungano adhimu na adimu, wa pekee duniani, Zanzibar japo inajiita nchi, na ina serikali yake, rais wake, bunge lake na mahakama yake, ni nchi jina tuu, lakini sio nchi bali ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani!, sifa kuu ya nchi ni kuwa na sovereignty, Zanzibar haina sovereignty, haina dola, wala haina sarafu, na hayo mabadiliko iliyoyafanya kwenye katiba yaku kujiita nchi ile 2010, mpaka leo katiba ya JMT, haiyatambui!. https://www.jamiiforums.com/threads...i-tuitambue-au-tumchelee-mwana-kulia.2286830/

P
Sasa yafaa nini kuwa na sehemu ya nchi inayojifanyia mambo yake nje ya Katiba? Kwanini tukuze migogoro endelevu isiyokuwa na tija?
Asking for a friend
 
Kwa nini asitunge cha kwake chenye hizo interpretation zake!
Mkuu upo serious kweli? Sasa kama kitabu kinasema uwongo mhadhiri akae kimya? Yaani mimi nikisema watoto wako hawana adabu, unanishauri nizae wa kwangu? Je, nikizaa wa kwangu, mtoto wako atakuwa mtoto mwema?
 
Back
Top Bottom