Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Muungano wetu Kimataifa ni muungano wa union ya nchi moja ya JMT, ndio inayotambuliwa kimataifa, ila ndani ya muungano, muungano wetu ni federation ya serikali mbili. ni muungano unique, adhimu.

P
Sasa kwa tafsiri yako hii, mbona mhadhiri hana kosa? Kwanini mmemkamata na kumbambika kesi ya UGAIDI?
 
Sasa katika hizo aina za muungano ulizotaja..mbona huu wa kwetu hauingii popote?
Ni kweli Muungano wetu ni muungano wa kipekee, haupo mahali pengine popote duniani. Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union ya nchi kuungana na kuwa nchi moja ya JMT, ndio inayotambuliwa kimataifa, ila kwa ndani ya muungano, muungano wetu ni muungano wa federation ya nchi mbili na serikali mbili. Huu ni muungano very unique, adhimu na adimu.

P
 
Ni kweli Muungano wetu ni muungano wa kipekee, haupo mahali pengine popote duniani. Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union ya nchi kuungana na kuwa nchi moja ya JMT, ndio inayotambuliwa kimataifa, ila kwa ndani ya muungano, muungano wetu ni muungano wa federation ya nchi mbili na serikali mbili. Huu ni muungano very unique, adhimu na adimu.

P
Muungano wa hovyo kupata kutokea duniani.
 
Habari za chinichini zinapenya kutoka viunga vya UDOM na mitandao ya kijamii kwamba kitu kilichomponza mhadhiri wa UDOM, Dr Kaijage, na kujikuta akipewa kesi ya ugaidi, ni ujasiri wake wa kusimamia taaluma kiuweledi bila kumuogopa mtu yeyote. Habari kamili zinadai wakati mhadhiri huyo akiendelea kufundisha somo la Political Science, mada ya Types of Governments alitoa mfano wa nchi zilizoungana na kutengeneza Union Government, huku akiiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi hizo.

Wahadhiri siku zote ni watu wa facts and evidence. Hawapendi blaablaa! Katika kuthibitisha ukweli wa mambo wanayofundisha, hupenda kufanya citations kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Kwa hiyo, ili kukomelea hoja yake kwamba Tanzania is not a union government, Dr Kaijage alinukuu definition kutoka kwenye kitabu cha Civics cha O-level kama citation hiyo ilivyokuwa highlighted hapo chini (wataalamu mtatusaidia kutambua hiki ni kitabu cha kidato cha ngapi):

View attachment 3651108
Kwa mujibu wa definition ya Union Government, kama ilivyoainishwa hapo juu, Dr Kaijage aliwaambia wanafunzi kwamba Tanzania haimo kwenye orodha hiyo kwa sababu Zanzibar haijapoteza madaraka yake. Yaani, kuna serikali inayoitwa ya Muungano (Union) na pia kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ina mamlaka yake kama nchi ndani ya muungano. Hivyo, aliwaambia wanafunzi kwamba kitabu hiki kilichoandikwa na kuhakikiwa na serikali, kinafundisha uwongo kwa kuwa Tanzania haikidhi vigezo vya kuitwa nchi ya Muungano.

Kana kwamba hilo halitoshi, Dr Kaijage alihamia kwenye kipengele kingine cha Democracy. Katika kipengele hicho alitoa mifano ya serikali ambazo aliziita za kidikteta, na kuitolea mfano Tanzania kama mojawapo ya nchi za kidikteta, hasa kufuatia sintofahamu kwenye chaguzi za 2009, 2020 na 2025. Aidha, alitumia kitabu kimojawapo cha O-level kutoa tafsiri hiyo kama inavyosomeka kwenye kipande kifuatacho:
View attachment 3651110
Kama inavyoonekana, mhadhiri huyo ali-highlight vipande kwenye mafundisho yake ambavyo viliashiria kwamba Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya kidikteta na uvunjivu mkubwa wa haki za binadamu.

Nini kilijiri?
Wakati akiendelea kufundisha, hakujua kuwa alikuwa anarekodiwa na mwanafunzi (chawa) mmoja ndani ya darasa lake. Baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi, mwanafunzi huyo alituma video kwa wakubwa zake kwa ajili ya utekelezaji.

MAONI YANGU
Kitendo cha kumkamata Dr Kaijage na kumkandika kesi ya ugaidi, kitasababisha wahadhiri wengine waogope kufundisha kiuledi na badala yake kufundisha uongo ili tu kuifurahisha serikali. Hata kama mifano aliyotoa haiwafurahishi serikali, sio busara kumpa kesi mbaya kiasi hiki. Kibaya zaidi, inasemekana familia ya Kaijage imekatiwa huduma za maji na umeme na kupelekea familia hiyo kuishi kwa taabu na shida. Hii sio sawa.

Nawasilisha.
​
Sasa wanataka wanafunzi wanafunzi wafundishwe uongo? Je wakienda kwenye exchange programs wanataenda na uongo waliomezeshwa? Samia and CCM are curse to the country.
 
Hujui maana ya kuwa profesa ni kitu gani; halafu unakuja kuuliza swali la kijinga kabisa.

Huyu ni mfano wa profesa mzuri sana kwa haya yaliyoelezwa hapa kama ndiyo kweli.

Wewe inawezekana hata darasa la Chuo Kikuu hujawahi kuingia, au kama uliingia, basi ulikutana na walimu wa high school na siyo maprofesa.
Profesa gani anapitia kitabu kimoja halafu anatoa hitimisho? .... huu ni ushahidi wa elimu ya magumashi wanayopata watoto wetu kwenye hiyo 'changanyikeni' inayoitwa UDOM!
 
Wewe umeamua kututukana sisi wanzazibari kwamba zanzibar sio nchi walah omba toba nyie vichogo ni madhurumati sana.. ila safari hii tutawanyoosha..
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, Tanzani ni nchi moja ya JMT, yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, Zanzibar sio nchi, bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani. Hivyo kuwaambia Zanzibar sio nchi, sio kuwatukana bali kuwaambia ukweli, it is a fact.
P
 
Mkuu upo serious kweli? Sasa kama kitabu kinasema uwongo mhadhiri akae kimya? Yaani mimi nikisema watoto wako hawana adabu, unanishauri nizae wa kwangu? Je, nikizaa wa kwangu, mtoto wako atakuwa mtoto mwema?
Atunge kitabu ambacho kitatufikia wengi kuliko kuishia kukosoa akiwa darasani ambapo ujumbe unawafikia wachache sn
 
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, Tanzani ni nchi moja ya JMT, yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, Zanzibar sio nchi, bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani. Hivyo kuwaambia Zanzibar sio nchi, sio kuwatukana bali kuwaambia ukweli, it is a fact.
P
na katika uhalisia likoje?,Zanzibar ni nchi ama si nchi?
 
Nadhani ndivyo walivyokubaliana waasisi kulingana na hali zetu navyofikiri.

Maana muungano wetu ni replica ya ule wa UK.

UK wana articles of Union hata sisi tunazo.

Ila namna wanavyofanya mambo yao ni tofauti kidogo na sisi.

Mimi naona mfumo huu ni sawa tu kwakuwa ndio umesaidia kulinda Muungano mpaka sasa hivi.

Kama serikali ya Tanganyika ingekuwepo Muungano ingekuwa rahisi kuvunjika.
Aisee!
 
Sasa wanataka wanafunzi wanafunzi wafundishwe uongo? Je wakienda kwenye exchange programs wanataenda na uongo waliomezeshwa? Samia and CCM are curse to the country.
1786869591272.png
 
Atunge kitabu ambacho kitatufikia wengi kuliko kuishia kukosoa akiwa darasani ambapo ujumbe unawafikia wachache sn
Vitabu vya ukweli vipo vingi. Sioni sababu CCM kuwalazimisha walimu kufundisha kwa kutumia kitabu cha uwongo.
 
Nyerere hana utakatifu wowote. Yeye ndiye aliyetuletea hii balaa ya muungano.
Tupate sifa za mtu kuwa mtakatifu kwanza then tulinganishe na sifa za yeye kuwa mtakatifu. Nimesikia ni mwenye Heri sijui...sifa za kuwa mwenye heri ni zipi?? Tusaidiwe yawezekana tuko wengi wenye heri!
 
Back
Top Bottom