Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Ni kweli Muungano wetu ni muungano wa kipekee, haupo mahali pengine popote duniani. Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union ya nchi kuungana na kuwa nchi moja ya JMT, ndio inayotambuliwa kimataifa, ila kwa ndani ya muungano, muungano wetu ni muungano wa federation ya nchi mbili na serikali mbili. Huu ni muungano very unique, adhimu na adimu.

P
Kuna nini special sanaa mpk sis kuwa na muungano wetu na kudanganya kuwa unajulikana kimataifa wakat hakuna nchi nyingine yyte inaofuata huo muungano..huoni tunajidanganya wenyew kwa kuifaidisha nchi moja kwa jina la kuuita muungano?
 
Kama alisema kuna Tanzania haina Union Government anapotosha


Zanzibar haina total sovereignty.

Mamlaka yake ni kwa mambo ya ndani tu ila inapokuja kwa maswala ya nje yanayoliwasilisha Taifa yale mambo yanayotambulisha Taifa yamebakia kwa serikali ya JMT.
Soma na kuelewa acha kutetea upumbavu
 
Kuna nini special sanaa mpk sis kuwa na muungano wetu na kudanganya kuwa unajulikana kimataifa wakat hakuna nchi nyingine yyte inaofuata huo muungano..huoni tunajidanganya wenyew kwa kuifaidisha nchi moja kwa jina la kuuita muungano?
1000358121.jpg
 
Habari za chinichini zinapenya kutoka viunga vya UDOM na mitandao ya kijamii kwamba kitu kilichomponza mhadhiri wa UDOM, Dr Kaijage, na kujikuta akipewa kesi ya ugaidi, ni ujasiri wake wa kusimamia taaluma kiuweledi bila kumuogopa mtu yeyote. Habari kamili zinadai wakati mhadhiri huyo akiendelea kufundisha somo la Political Science, mada ya Types of Governments alitoa mfano wa nchi zilizoungana na kutengeneza Union Government, huku akiiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi hizo.

Wahadhiri siku zote ni watu wa facts and evidence. Hawapendi blaablaa! Katika kuthibitisha ukweli wa mambo wanayofundisha, hupenda kufanya citations kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Kwa hiyo, ili kukomelea hoja yake kwamba Tanzania is not a union government, Dr Kaijage alinukuu definition kutoka kwenye kitabu cha Civics cha O-level kama citation hiyo ilivyokuwa highlighted hapo chini (wataalamu mtatusaidia kutambua hiki ni kitabu cha kidato cha ngapi):

View attachment 3651108
Kwa mujibu wa definition ya Union Government, kama ilivyoainishwa hapo juu, Dr Kaijage aliwaambia wanafunzi kwamba Tanzania haimo kwenye orodha hiyo kwa sababu Zanzibar haijapoteza madaraka yake. Yaani, kuna serikali inayoitwa ya Muungano (Union) na pia kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ina mamlaka yake kama nchi ndani ya muungano. Hivyo, aliwaambia wanafunzi kwamba kitabu hiki kilichoandikwa na kuhakikiwa na serikali, kinafundisha uwongo kwa kuwa Tanzania haikidhi vigezo vya kuitwa nchi ya Muungano.

Kana kwamba hilo halitoshi, Dr Kaijage alihamia kwenye kipengele kingine cha Democracy. Katika kipengele hicho alitoa mifano ya serikali ambazo aliziita za kidikteta, na kuitolea mfano Tanzania kama mojawapo ya nchi za kidikteta, hasa kufuatia sintofahamu kwenye chaguzi za 2009, 2020 na 2025. Aidha, alitumia kitabu kimojawapo cha O-level kutoa tafsiri hiyo kama inavyosomeka kwenye kipande kifuatacho:
View attachment 3651110
Kama inavyoonekana, mhadhiri huyo ali-highlight vipande kwenye mafundisho yake ambavyo viliashiria kwamba Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya kidikteta na uvunjivu mkubwa wa haki za binadamu.

Nini kilijiri?
Wakati akiendelea kufundisha, hakujua kuwa alikuwa anarekodiwa na mwanafunzi (chawa) mmoja ndani ya darasa lake. Baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi, mwanafunzi huyo alituma video kwa wakubwa zake kwa ajili ya utekelezaji.

MAONI YANGU
Kitendo cha kumkamata Dr Kaijage na kumkandika kesi ya ugaidi, kitasababisha wahadhiri wengine waogope kufundisha kiuledi na badala yake kufundisha uongo ili tu kuifurahisha serikali. Hata kama mifano aliyotoa haiwafurahishi serikali, sio busara kumpa kesi mbaya kiasi hiki. Kibaya zaidi, inasemekana familia ya Kaijage imekatiwa huduma za maji na umeme na kupelekea familia hiyo kuishi kwa taabu na shida. Hii sio sawa.

Nawasilisha.
​
Uonevu wa kijinga kabisa huu. Sasa kosa liko wapi hapa? Au tuamini watu wenye akili ndogo wamepata nafasi ya kutawala watu wenye akili kubwa?
 
Aliwr



Siku muungano ukivunjwa/ukivunjika ningali hai, nitauza hiki kiwanja changu, nifanye sherehe.

Bora nife nikiitwa mpangaji, kuliko kujenga ndani ya muungano wenye, machungu, mateso, ubaguzi, mauaji na dharau.
Sasa kiwanja ulinunua cha nini Boss
 
Kama alisema kuna Tanzania haina Union Government anapotosha


Zanzibar haina total sovereignty.

Mamlaka yake ni kwa mambo ya ndani tu ila inapokuja kwa maswala ya nje yanayoliwasilisha Taifa yale mambo yanayotambulisha Taifa yamebakia kwa serikali ya JMT.
It's okay...

Then, Tanganyika yenyewe iko wapi ikiwa na hata hayo mamlaka yake machache ya ndani kama ilivyo kwa mshirika wake huyu mwingine yaani Zanzibar..?

Mimi nasema, ni kweli muungano huu ni WA KIPEKEE sana (kwa sauti ya Pascal Mayalla). Lakini ni upekee hatari wenye madhara makubwa na ndio maana watu wanahoji...

Na ulihojiwa sana huko nyuma (kumbuka kundi lile la Wabunge maarufu kama G55 chini ya kina Tuntemeke Sanga) walipoitaka Tanganyika yao...

By then, movement hiyo ilizimwa kiaina. Lakini hii ya miaka hii leo chini ya GenZ wa kizazi cha AI, kitawaka tu na sidhani kama atakuwepo mzee yeyote au bunduki wala mabomu ya wa kuuzima moto huu wa mabadiliko....!

The world now is going through very big social, political & economical changes..

Kizazi cha wazee Steven Masatu Wasira wa miaka ya 1947 ni the past hao. Sasa tuko kwenye kizazi cha GenZ na AI, ni lazima tukubaliane na haya...
 
Hata chama cha majambazi chenyewe kinajutia
Nani hao.
Akina Kabuti wanaosema Samia yupo kwa sababu kawekwa na mungu?
Au akina Sokwe wa Gombe na huyu Asha wanaosherehekea mauaji ya waTanzania kuwa ni "kazi inayotukuka"?

Nani huko kwenye hicho chama cha Majabazi, sijamsikia yeyote; hata kuguna tu, kwa sababu minofu imewajaa mdomoni.
 
Uonevu wa kijinga kabisa huu. Sasa kosa liko wapi hapa? Au tuamini watu wenye akili ndogo wamepata nafasi ya kutawala watu wenye akili kubwa?
Siku zote akili ndogo ikishika madaraka haitaki akili kubwa iisogelee!
 
Back
Top Bottom