Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

Habari za chinichini zinapenya kutoka viunga vya UDOM na mitandao ya kijamii kwamba kitu kilichomponza mhadhiri wa UDOM, Dr Kaijage, na kujikuta akipewa kesi ya ugaidi, ni ujasiri wake wa kusimamia taaluma kiuweledi bila kumuogopa mtu yeyote. Habari kamili zinadai wakati mhadhiri huyo akiendelea kufundisha somo la Political Science, mada ya Types of Governments alitoa mfano wa nchi zilizoungana na kutengeneza Union Government, huku akiiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi hizo.

Wahadhiri siku zote ni watu wa facts and evidence. Hawapendi blaablaa! Katika kuthibitisha ukweli wa mambo wanayofundisha, hupenda kufanya citations kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Kwa hiyo, ili kukomelea hoja yake kwamba Tanzania is not a union government, Dr Kaijage alinukuu definition kutoka kwenye kitabu cha Civics cha O-level kama citation hiyo ilivyokuwa highlighted hapo chini (wataalamu mtatusaidia kutambua hiki ni kitabu cha kidato cha ngapi):

View attachment 3651108
Kwa mujibu wa definition ya Union Government, kama ilivyoainishwa hapo juu, Dr Kaijage aliwaambia wanafunzi kwamba Tanzania haimo kwenye orodha hiyo kwa sababu Zanzibar haijapoteza madaraka yake. Yaani, kuna serikali inayoitwa ya Muungano (Union) na pia kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ina mamlaka yake kama nchi ndani ya muungano. Hivyo, aliwaambia wanafunzi kwamba kitabu hiki kilichoandikwa na kuhakikiwa na serikali, kinafundisha uwongo kwa kuwa Tanzania haikidhi vigezo vya kuitwa nchi ya Muungano.

Kana kwamba hilo halitoshi, Dr Kaijage alihamia kwenye kipengele kingine cha Democracy. Katika kipengele hicho alitoa mifano ya serikali ambazo aliziita za kidikteta, na kuitolea mfano Tanzania kama mojawapo ya nchi za kidikteta, hasa kufuatia sintofahamu kwenye chaguzi za 2009, 2020 na 2025. Aidha, alitumia kitabu kimojawapo cha O-level kutoa tafsiri hiyo kama inavyosomeka kwenye kipande kifuatacho:
View attachment 3651110
Kama inavyoonekana, mhadhiri huyo ali-highlight vipande kwenye mafundisho yake ambavyo viliashiria kwamba Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya kidikteta na uvunjivu mkubwa wa haki za binadamu.

Nini kilijiri?
Wakati akiendelea kufundisha, hakujua kuwa alikuwa anarekodiwa na mwanafunzi (chawa) mmoja ndani ya darasa lake. Baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi, mwanafunzi huyo alituma video kwa wakubwa zake kwa ajili ya utekelezaji.

MAONI YANGU
Kitendo cha kumkamata Dr Kaijage na kumkandika kesi ya ugaidi, kitasababisha wahadhiri wengine waogope kufundisha kiuledi na badala yake kufundisha uongo ili tu kuifurahisha serikali. Hata kama mifano aliyotoa haiwafurahishi serikali, sio busara kumpa kesi mbaya kiasi hiki. Kibaya zaidi, inasemekana familia ya Kaijage imekatiwa huduma za maji na umeme na kupelekea familia hiyo kuishi kwa taabu na shida. Hii sio sawa.

Nawasilisha.
​
Jamani nammiss sana waziri mkuu
 
Raisi wa JMT na zanzibar nani boss, mbona hakuna rais wa Tanganyika
The big boss ni rais wa nchi, rais wa JMT ambayo ndio nchi, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT.

Hakuna rais wa Tanganyika, kwasababu Tanganyika doesn't exist anymore. Baada ya Muungano, zile nchi zote mbili, Tanganyika and Zanzibar, died and buried, ila ile sehemu iliokuwa nchi ya Zanzibar, ikapewa utawala wake wa ndani, ila sio nchi, bali ni sehemu ya JMT.
P
 
Mkuu unataka kusema kwamba Rais wa Zanzibar ni ceremonial? Mbona analindwa na jeshi lake na anapigiwa mizinga 21?
 
Ndio maana tunapaswa kubadirsha katiba hii hili kuwepo na mamlaka ya elimu rasmi kabisa, aidha pia katiba iliyopo kwenye tovuti ya www.katibampya.com imeweka mamlaka ya elimu iitwayo NEA "National Education Authority" unaweza kuipatia katiba hiyo kwenye tovuti tajwa hapo juu.
 
Mkuu unataka kusema kwamba Rais wa Zanzibar ni ceremonial? Mbona analindwa na jeshi lake na anapigiwa mizinga 21?
Kwa vile kimataifa Zanzibar sio nchi, hivyo rais wa Zanzibar ni ceremonial tuu, ila kwa ndani ya Zanzibar ni rais kamili wa sehemu ya JMT inayojitegemea kwa utawala wake wa ndani. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT, nchi ni moja tuu, JMT!.
P
 
Uonevu wa kijinga kabisa huu. Sasa kosa liko wapi hapa? Au tuamini watu wenye akili ndogo wamepata nafasi ya kutawala watu wenye akili kubwa?
Rais wa muungano ana mamlaka na Zanzibar,ana jeshi na idara ya usalama kule,ana wizara ya elimu,fedha, mambo ya ndani kule Zanzibar,ana mamlaka na kila milimita ya ardhi Zanzibar, anakusanya Kodi kupitia TRA kule, Zanzibar ni milki yake
Rais wa Zanzibar Hana jeshi kule na huteuliwa na mamlaka za jmt kukalia kiti cha smz

Mhadhiri kudai Tanzania hakuna muungano wakati kuna jmt ni upotoshaji na kilichomkuta ni sahihi
 
Kwa hiyo huyo Mhadhiri kudai Tanzania hakuna muungano ndiyo ugaidi?
 
The big boss ni rais wa nchi, rais wa JMT ambayo ndio nchi, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT.

Hakuna rais wa Tanganyika, kwasababu Tanganyika doesn't exist anymore. Baada ya Muungano, zile nchi zote mbili, Tanganyika and Zanzibar, died and buried, ila ile sehemu iliokuwa nchi ya Zanzibar, ikapewa utawala wake wa ndani, ila sio nchi, bali ni sehemu ya JMT.
P
This is absolutely unbelievable...nothing could be more ridiculous! Soma katiba ya Zanzibar 2010

1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizungukana bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar

2. Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyoteinatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvuna sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.
 
We unaamini ndicho alichokamatiwa,umewekewa ushahidi?
Kwani hapa tuko mahakamani, au tunachangia mjadala? Mtoa mada hajatoa sababu mwanzoni mwa mada yake? Au huna macho!
Au una sababu halisi za huo ugaidi? Si uzitoe hapa? Unaficha nini?
 
All in all Dr yupo sahihi kabisa binafsi sioni ugaidi hapo watu wasitoe maoni sasa (facts)
 
Back
Top Bottom