Kilichonitokea kituo cha Daraja la Salenda baada ya kushuka kwenye daladala saa nne usiku

Kilichonitokea kituo cha Daraja la Salenda baada ya kushuka kwenye daladala saa nne usiku

Long time! Maeneo hapo Shekilango,saa sita usiku,nilavuka barabara ili nipande bus la Mbezi,nina kibegi na kina Ipad,nikaona jamaa wawili nao wakavuka na kunifuata,nikahisi hawa sio watu wema,nikaongeza mwendo,nao wakaongeza,nikatimua mbio wakaunga,jamaa wa daradara wanaona mchezo wakipiga kelele kimbia wewe kimbia,mbele kuna daradara ikaja ikasimama mbele yangu nikajitupa haraka,jamaa alirusha panga likagonga mlango[emoji3][emoji3]....nikapona.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ve wa mlongo, hinu ukajumbalila kwoki? Ve vandu va dala dala havo ndawa ya kyani vahuruki ng'oyi kukutangatila??

Niheki hadi maholi gihuma. Ila vibaka jamaniii uwiiiih
 
Siku nakatiza mitaa hiyo toka upanga na stress zangu sa mbili hivi sijui ikawaje .
Lile kundi hawa hapa vibaka.
Tulikimbizana mpk wanarudi tuko miembeni kino makaburini.
Wakarudi maana walijua huku huyu jamaa anatupeleka mitaa yake tukatandikwe😅😅😅😅.
Na kweli wangefika tu American chips siku hiyo cha moto wangekipata
 
Hahahaha
Hama huko Vikindu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nipo Mawasiliano, ila sikuwahi jua km kuna Campus ya Mzumbe hapa Dar, pia ni kwa postgraduate ndo maana sio maarufu.

Au pia mie niko buzzy sana na mambo yangu.
 
Nakumbuka nikitokea maeneo ya Slipway baada ya boss wangu kunipa laki moja nikatafute samaki,

Nikaenda msasani nikakosa hivo nikaona niende feri, nikapanda gari la kwenda Kariakoo tulipokaribia Salender nikamwomba konda anishushe hapo, konda kwa mshtuko, unasema?

Nikamwambia tena nishushe Sarenda muda huo ni saa 4 usiku basi bhana kama unavojua kuna watu hawapendi fuatilia mambo ya watu gari ikasimama nikashuka

Mbele yangu kulikuwa na gari moja ndogo imesimama halafu but I la mbele limenyanyuliwa nahisi ilipata hitilafu, nyuma kulikuwa na trafiki anaelekeza magari ile njia ya kwenda Coco beach, njia ya kutokea Coco nikaona vijana kama sita hivi muda huo wote yaani ni kama dk 10 zimepita toka nishuke ila kila gari ninalolisimamisha la kwenda Posta kutoka Makumbusho hayasimami yaana yanapita na mia

Sasa wale jamaa walikuwa na vifaa vikubwa balaa nikafikiri ni wanamazoezi, nikafikiri kujiunga nao ili nivuke pale darajani

Bado nawaza haijaisha sekunde kumi naona wameanzisha timbwili kwenye gari lile lililokuwa limepaki hapo mbele, kulikuwa na vijana wawili, kama sio waarabu basi ni wahindi, mara jamaa wakafungua milango muda huo hawa jamaa wenye gari wamekimbia mmoja anaelekea kwa askari anayeongoza magari hapo njia ya Coco beach mwingine anakimbia huko upande wa Pili wa barabara

Sikumbuki nini kilitokea ila nilijikuta ile njia ya Muhimbili nipo kwenye kituo karibu na chuo sijui ndo Mzumbe nasubiri gari ya kutoka Kariakoo nirudi Masaki
Kwahiyo ndugu mwandishi inaonekana hata wew hujui nni kilitokea
 
Ndio hiyo hiyo mikoko mkuu ndani ya ile hifadhi ya maliasili kuna bango lao pale la kukataza watu wasifanye shughuli yoyote mle ndani🤣🤣🤣Sijasoma biology so sijui kutofautisha mimea mkuu.
Kama mikoko ndiyo hiyohiyo mianzi unanitia mashaka pamoja na uandishi wako wote unaoonesha kila kitu hukijui.
 
Kama mikoko ndiyo hiyohiyo mianzi unanitia mashaka pamoja na uandishi wako wote unaoonesha kila kitu hukijui.
Mkuu sawa silijui hilo daraja la salender dar nimekuja juzi🤣🤣🤣🤣🤣.But huu uzi wakati unaanza jana ucku nilikua nachati na @ Cocastic na mdau @ George pk nikiwa las vegas casino tunazungumzia matukio ya hapo darajani way back.
 
Siku nakatiza mitaa hiyo toka upanga na stress zangu sa mbili hivi sijui ikawaje .
Lile kundi hawa hapa vibaka.
Tulikimbizana mpk wanarudi tuko miembeni kino makaburini.
Wakarudi maana walijua huku huyu jamaa anatupeleka mitaa yake tukatandikwe😅😅😅😅.
Na kweli wangefika tu American chips siku hiyo cha moto wangekipata
Mkuu walianzia kukukimbiza pale darajani mpaka kule juu kino shamba(Makaburini)kweli una mapafu ya mbwa🤣🤣🤣🤣🤣Pale miembeni makaburini ndio kijiwe chao,kule juu mitaa ya ilipokuwepo american chips jau🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mkuu shekilango ucku mpaka wale boda boda wa kituo cha mwendokasi ni wakwapuaji hasa wakiona mtu yupo tungi
Hata Buguruni she'll,kuna jamaa yangu alichukua boda mida saa 5 usiku!anaenda ubungo,kufika maeneo ya Tabata kuna boda nyingine ikawapita,kufika kule mbele jamaa kwa spidi akakunja kona kuelekea kushoto huko mbele kuna kama shamba na nyumba zipo mbali,chap na boda mwingine akafika,wakatoa mapanga kwenye makoti,jamaa akapukutishwa visenti vyote na simu alizokuwa nazo...
 
Back
Top Bottom