Kilimanjaro: Ajinyonga hadi kufa kisa wivu wa kimapenzi

homa ya akili ni janga kubwa sana siku tu kwa jirani usiombe ukutwe
 
LOFA SANA HUYO
usim2kane jamaa,2metofautiana sana ktk mambo ya majanga!!!......wengine hawawezi ata kumwangalia mkewe akisalimiana na mwanamme mwingine kwa kushikana mikono anaweza ata kuzimia,ndo manake wale jamaa wenye siasa kali wake zao wanavaa sox kwenye viganja na kwenye nyayo,na pia mavazi yao wanajifunika mwili mzima na kuacha macho tu kama cobra,yote hiyo ni wivu mazee!! da!!
 
Ametuabisha Sana ameacha mwanamke kuchukuwa KOMBE
 
Hendry alimpenda mkewe bila shaka, inavyoonekana dini ilikuwa kikwazo kwa mkewe, kama aliyempata ni Mwislamu kama yeye.
Hii ndiyo maana huwa tunashauriwa hiki kipengele cha dini kiangaliwe kwa jicho la kipekee sana kwenye mahusiano yanayotegemewa kuja kuanzisha familia.

Lakini sadly vijana wa kileo hawasikii mwisho tunabaki na mayatima waliotokana na uzembe wa wazazi wao.
 
Kwa haraka haraka anaweza akaonekana ni mjinga hana akili, lakini maumivu ya mapenzi yanahitaji akili ya ziada kuyahimili. Siwezi kumshangaa kabisa
Maumivu ya mapenzi wewe mwanaume waachie wanawake hayo hatukuumbiwa sisi,mwanaume unatakiwa umthamini mwanamke siyo umpende mthamini kwa yale anakufanyia mpe care nzuri yeye arudishe upendo kwako akiwa haeleweki tupa kule kamata mwengine maisha yaende.

Zamani wazee wetu walikuwa hawapati fursa ya kujichagulia wenza wao walikuwa wanaelekezwa na baba zao nenda nyumba ile oa yule wanachukuana huku mke akijifunza kumpenda mumewe kutokana na anavyotunzwa mwisho tukazaliwa sisi kizazi cha mwisho mwisho cha dhahabu 1980s,hiyo asili ilipopotea miaka ya 90s ndiyo kimekuja kizazi hiki lia lia,wanachanganya makabila hovyo bila kuzingatia kila kabila lina utamaduni wake ambao muoaji anaweza asiuelewe mwisho mke akitaka ku-adopt utamaduni wa kwao ndani ya nyumba mume ana-react matokeo kama hivi kuuwana hovyo au kujiuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…