Kilimanjaro: Ajinyonga hadi kufa kisa wivu wa kimapenzi

Kilimanjaro: Ajinyonga hadi kufa kisa wivu wa kimapenzi

homa ya akili ni janga kubwa sana siku tu kwa jirani usiombe ukutwe
 
LOFA SANA HUYO
usim2kane jamaa,2metofautiana sana ktk mambo ya majanga!!!......wengine hawawezi ata kumwangalia mkewe akisalimiana na mwanamme mwingine kwa kushikana mikono anaweza ata kuzimia,ndo manake wale jamaa wenye siasa kali wake zao wanavaa sox kwenye viganja na kwenye nyayo,na pia mavazi yao wanajifunika mwili mzima na kuacha macho tu kama cobra,yote hiyo ni wivu mazee!! da!!
 
Kijana mmoja Anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 aitwae Henry amejinyonga hadi kufa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Tukio hilo limetokea leo mchana Katika Kijiji cha Narumu huko katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Sababu Za kijana huyo kujinyonga hadi kufa ni baada ya mke wake wa ndoa ajulikanae kwa jina la Zuhura Luteri kuondoka na kwenda kujihusisha Kimapenzi Na wanaume wengine na hivyo alifanya kila jitihada za kumrudisha lakini zilishindikana.

Polisi wamefika kuchukua mwili na kuondoka nao Kwa ajili ya Uchunguzi. Kijana huyo alikuwa akiishi na mama yake mzazi na ameacha watoto wawili mwenye umri wa miaka 7 na mwingine ana umri wa miaka 5.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Ismael Urassa amethibitisha kutokea Kwa tukio hilo.
Ametuabisha Sana ameacha mwanamke kuchukuwa KOMBE
 
Hendry alimpenda mkewe bila shaka, inavyoonekana dini ilikuwa kikwazo kwa mkewe, kama aliyempata ni Mwislamu kama yeye.
Hii ndiyo maana huwa tunashauriwa hiki kipengele cha dini kiangaliwe kwa jicho la kipekee sana kwenye mahusiano yanayotegemewa kuja kuanzisha familia.

Lakini sadly vijana wa kileo hawasikii mwisho tunabaki na mayatima waliotokana na uzembe wa wazazi wao.
 
Kwa haraka haraka anaweza akaonekana ni mjinga hana akili, lakini maumivu ya mapenzi yanahitaji akili ya ziada kuyahimili. Siwezi kumshangaa kabisa
Maumivu ya mapenzi wewe mwanaume waachie wanawake hayo hatukuumbiwa sisi,mwanaume unatakiwa umthamini mwanamke siyo umpende mthamini kwa yale anakufanyia mpe care nzuri yeye arudishe upendo kwako akiwa haeleweki tupa kule kamata mwengine maisha yaende.

Zamani wazee wetu walikuwa hawapati fursa ya kujichagulia wenza wao walikuwa wanaelekezwa na baba zao nenda nyumba ile oa yule wanachukuana huku mke akijifunza kumpenda mumewe kutokana na anavyotunzwa mwisho tukazaliwa sisi kizazi cha mwisho mwisho cha dhahabu 1980s,hiyo asili ilipopotea miaka ya 90s ndiyo kimekuja kizazi hiki lia lia,wanachanganya makabila hovyo bila kuzingatia kila kabila lina utamaduni wake ambao muoaji anaweza asiuelewe mwisho mke akitaka ku-adopt utamaduni wa kwao ndani ya nyumba mume ana-react matokeo kama hivi kuuwana hovyo au kujiuwa.
 
Back
Top Bottom