Kilimanjaro: Askari amuua mwenzake kwa ugomvi wa kukaa siti ya mbele

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Utata umeibuka kuhusu kifo cha askari polisi wa kitengo cha upelelezi Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, aliyetambulika kwa jina moja la Linus aliyefariki usiku wa kuamkia Mei 31, mwaka huu ikidaiwa alipigwa risasi shingoni na askari mwenzake.

Alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa kwa kuwa wako kwenye uchunguzi na wakikamilisha atalizungumzia kwa kina.

Akisimulia ilivyokuwa, Mwenyekiti wa kijiji cha Kituri wilayani Mwanga, Thomas Mgala alisema siku hiyo polisi walifika kijijini hapo kuwasaka wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya.

Mgala alisema wakati polisi hao wawili wakiondoka eneo hilo wakiwa na wenzao, kuliibuka mzozo kati yao kuhusu nani anatakiwa kukaa siti ya mbele kwenye gari walilokuwa wakitumia.

“Wakati wanang’ang’ania kukaa siti ya mbele, huyu Linus yeye ndiye alionekana kuwa na cheo kikubwa kuliko mwenzake, kwa hiyo alikuwa na haki ya kukaa mbele, huyu mwenza

“Baada ya hapo Linus alikuwa amesimama pembeni ya gari, huyu askari mwenzake alikwenda kunyanyua kiti akachukua bunduki akarudi akamwelekezea mwenzake shingoni akamfyatulia risasi akaanguka chini...hakupiga kelele wala nini, baadaye akaning’iniza bunduki shingoni akajishika kichwa akisema nimeua,” alidai mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kitendo hicho, askari wengine waliokuwa kwenye gari hilo walipaza sauti wakisema, “umeua...aisee umeua,” huku dereva akiwalaumu wenzake waliokuwepo maporini waliacha risasi chemba, “amefyatua amemuua Linus.”

“Wakashtuka wakarudi, walipofika eneo la tukio wanampigapiga haamki, wakamchukua wakamuweka kwenye gari wakaondoka naye hadi Kituo cha polisi Kifaru kijiji jirani.” Mwenyekiti huyo alidai kuwa baada ya tukio hilo wananchi hawakutaka ukweli ufichwe na hata walipokwenda polisi waliwaeleza ukweli wa kilichotokea.

“Mwanzo walisema alikuwa anafukuza mirungi na pikipiki, wakati anazuia pikipiki yenye mirungi ikaja pikipiki nyingine yenye mirungi ikamgonga akaangukia kwenye kisiki akafa, jambo ambalo lilizua taharuki kidogo kwa sababu ukweli ulikuwa unajulikana,” alidai Mwenyekiti huyo wakati akizungumza na Mwananchi

Mwananchi
 
Kiti cha mbele kina nini hasa!??
 
nasema hivi...jeshi letu la polisi.....60% wanavuta bangi... na hawavuti kama starehe...yaani andasi....bali wanajidanganya inawapa ujasiri...yes...ujasiri ndio huo wa 1) kubishana na askari mwenzio aliekuzidi cheo, 2) kumuelekezea askari mwenzi mtutu 3) silaha zinawekwa kama vipisi vya fegi kwenye ash tray.......bado tuna safari ndefu sana...
 
[emoji3577]
Screenshot_20210405-074523~2.jpg
 
Back
Top Bottom