Kilimanjaro: Askari amuua mwenzake kwa ugomvi wa kukaa siti ya mbele

Utata umeibuka kuhusu kifo cha askari polisi wa kitengo cha upelelezi Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, aliyetambulika kwa jina moja la Linus aliyefariki usiku wa kuamkia Mei 31, mwaka huu ikidaiwa alipigwa risasi shingoni na askari mwenzake.

Alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa kwa kuwa wako kwenye uchunguzi na wakikamilisha atalizungumzia kwa kina.

Akisimulia ilivyokuwa, Mwenyekiti wa kijiji cha Kituri wilayani Mwanga, Thomas Mgala alisema siku hiyo polisi walifika kijijini hapo kuwasaka wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya.

Mgala alisema wakati polisi hao wawili wakiondoka eneo hilo wakiwa na wenzao, kuliibuka mzozo kati yao kuhusu nani anatakiwa kukaa siti ya mbele kwenye gari walilokuwa wakitumia.

“Wakati wanang’ang’ania kukaa siti ya mbele, huyu Linus yeye ndiye alionekana kuwa na cheo kikubwa kuliko mwenzake, kwa hiyo alikuwa na haki ya kukaa mbele, huyu mwenza

“Baada ya hapo Linus alikuwa amesimama pembeni ya gari, huyu askari mwenzake alikwenda kunyanyua kiti akachukua bunduki akarudi akamwelekezea mwenzake shingoni akamfyatulia risasi akaanguka chini...hakupiga kelele wala nini, baadaye akaning’iniza bunduki shingoni akajishika kichwa akisema nimeua,” alidai mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kitendo hicho, askari wengine waliokuwa kwenye gari hilo walipaza sauti wakisema, “umeua...aisee umeua,” huku dereva akiwalaumu wenzake waliokuwepo maporini waliacha risasi chemba, “amefyatua amemuua Linus.”

“Wakashtuka wakarudi, walipofika eneo la tukio wanampigapiga haamki, wakamchukua wakamuweka kwenye gari wakaondoka naye hadi Kituo cha polisi Kifaru kijiji jirani.” Mwenyekiti huyo alidai kuwa baada ya tukio hilo wananchi hawakutaka ukweli ufichwe na hata walipokwenda polisi waliwaeleza ukweli wa kilichotokea.

“Mwanzo walisema alikuwa anafukuza mirungi na pikipiki, wakati anazuia pikipiki yenye mirungi ikaja pikipiki nyingine yenye mirungi ikamgonga akaangukia kwenye kisiki akafa, jambo ambalo lilizua taharuki kidogo kwa sababu ukweli ulikuwa unajulikana,” alidai Mwenyekiti huyo wakati akizungumza na Mwananchi

Mwananchi
Itakuwa walikuwa wametumia madawa hayo waliyokwenda kuyakamata.

By the way.wakati mwingine ni yale machozi ya wale waliowahi kuwabambikia kesi za uongo ndiyo yalikuwa yanakauka.Polisi wanafanya mauwaji na ubambikiaziaji makosa watu hovyo
 
Utata umeibuka kuhusu kifo cha askari polisi wa kitengo cha upelelezi Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, aliyetambulika kwa jina moja la Linus aliyefariki usiku wa kuamkia Mei 31, mwaka huu ikidaiwa alipigwa risasi shingoni na askari mwenzake.

Alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa kwa kuwa wako kwenye uchunguzi na wakikamilisha atalizungumzia kwa kina.

Akisimulia ilivyokuwa, Mwenyekiti wa kijiji cha Kituri wilayani Mwanga, Thomas Mgala alisema siku hiyo polisi walifika kijijini hapo kuwasaka wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya.

Mgala alisema wakati polisi hao wawili wakiondoka eneo hilo wakiwa na wenzao, kuliibuka mzozo kati yao kuhusu nani anatakiwa kukaa siti ya mbele kwenye gari walilokuwa wakitumia.

“Wakati wanang’ang’ania kukaa siti ya mbele, huyu Linus yeye ndiye alionekana kuwa na cheo kikubwa kuliko mwenzake, kwa hiyo alikuwa na haki ya kukaa mbele, huyu mwenza

“Baada ya hapo Linus alikuwa amesimama pembeni ya gari, huyu askari mwenzake alikwenda kunyanyua kiti akachukua bunduki akarudi akamwelekezea mwenzake shingoni akamfyatulia risasi akaanguka chini...hakupiga kelele wala nini, baadaye akaning’iniza bunduki shingoni akajishika kichwa akisema nimeua,” alidai mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kitendo hicho, askari wengine waliokuwa kwenye gari hilo walipaza sauti wakisema, “umeua...aisee umeua,” huku dereva akiwalaumu wenzake waliokuwepo maporini waliacha risasi chemba, “amefyatua amemuua Linus.”

“Wakashtuka wakarudi, walipofika eneo la tukio wanampigapiga haamki, wakamchukua wakamuweka kwenye gari wakaondoka naye hadi Kituo cha polisi Kifaru kijiji jirani.” Mwenyekiti huyo alidai kuwa baada ya tukio hilo wananchi hawakutaka ukweli ufichwe na hata walipokwenda polisi waliwaeleza ukweli wa kilichotokea.

“Mwanzo walisema alikuwa anafukuza mirungi na pikipiki, wakati anazuia pikipiki yenye mirungi ikaja pikipiki nyingine yenye mirungi ikamgonga akaangukia kwenye kisiki akafa, jambo ambalo lilizua taharuki kidogo kwa sababu ukweli ulikuwa unajulikana,” alidai Mwenyekiti huyo wakati akizungumza na Mwananchi

Mwananchi
wanawasaka wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya Wakati wao ndo watumiaji wakubwa hadi wanauana kijinga
 
Ndo bongo movie zetu zilivyoo.nimeuaaa badae wana saidiana na muuaji
 
wakati IGP anasema wilaya ya Kinondoni inaongoza kwa uhalifu nilicheka sana. Naangalia kwa mfano mabatini na pale Urafiki. Kuna misele usiku kucha kulazimisha wenye makosa tena madogo madogo yasiyo na tija, wawape hao jamaa hela. Wenye makosa makubwa nani anawalea sasa?
Kuna sababu ya kuanza kumulika jeshi la polisi na wale wasio fuata sheria na taratibu za jeshi hilo, ili kumaliza au kupunguza uhalifu.
Hii ya Mwanga ni mfano tu wa jinsi hao watu walivyo na roho ngumu
 
Mwanzo walisema alikuwa anafukuza mirungi na pikipiki, wakati anazuia pikipiki yenye mirungi ikaja pikipiki nyingine yenye mirungi ikamgonga akaangukia kwenye kisiki akafa, jambo ambalo lilizua taharuki kidogo kwa sababu ukweli ulikuwa unajulikana,” alidai Mwenyekiti huyo wakati akizungumza na Mwananchi[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]
[emoji3][emoji3] huu uongo hata mimi ambaye sijasomea uchunguzi siwezi kuukubali,
Kwanza aliyegongwa pikipiki atakuwa na majeraha ya kuburuzwa au kuvunjika

Pili jeraha la risasi na kisiki ni tofauti
Mengine mtaongezea....

Hii ni laana ya uonevu inawatafuna tu
 
Jamani mzaha mzaha hutumbuka usaha. Mungu atuepushe na majanga kama haya maana hakudhamiria kufanya alilofanya
 
Mwanzo walisema alikuwa anafukuza mirungi na pikipiki, wakati anazuia pikipiki yenye mirungi ikaja pikipiki nyingine yenye mirungi ikamgonga akaangukia kwenye kisiki akafa, jambo ambalo lilizua taharuki kidogo kwa sababu ukweli ulikuwa unajulikana,” alidai Mwenyekiti huyo wakati akizungumza na Mwananchi

.......tabia halisi ya Polisi!!!
 
Wapimwe akili waliobaki.
Nakazia .japo huenda jamaa alijua bundik haijakokiwa,akataka kumjoki kumbe kitu kipo on air ,kubofya tu ikakubali,hata hivyo ni ujinga kufanya mzaha na siraha za moto.nakumbuka tulipokuwa wadogo darasa la tatu hiv,Kuna ndg yang mtt wa kaka angu tukiwa ndani chumbani kwa bro,mwenzangu si akafungua drop ya kitanda kuchek katoa mguu wa kuku (bastora)ya baba ake(bro angu) akanielekezea akawa anabofya trigger kacha kacha kacha,amenielekezea mm usoni,si unajua Mambo ya utoto,uzuri haikuwa na risasi kabisa.huwa nikikumbuka hii michezo Basi tu utt bana.ila.hawa ma.poti shwain kabisa .
 
Unaweza ukauwa mtu ukazani hawajakuona, kwa dhima ya Dunia na Mungu pia utajulikana tuu

Damu nzito kuliko maji
 
Hairuhusiwi kabisa kumuelekezea mwenzio bunduki hata kwa bahati mbaya na ni kosa kubwa jeshini ukionekana umemuelekezea mwenzio bunduki.
Unahukumiwa kama uliyejaribu kuua.
Mara nyingi Police hupenda kutaniana. Mara zote katika operation yoyote kiongozi anajulikana na hukaa mbele. Hakuna kitu kama hicho Cha kugombea siti. Mtaniaji ali- assume kwamba hakuna risasi chemba na pengine vilevile kifunga usalama Kiko mahali pake
 
Alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa kwa kuwa wako kwenye uchunguzi na wakikamilisha atalizungumzia kwa kina.
Wakiambiwa wapimwe akili wanahitilafu wanalalamika, sasa kukaa mbele kunamuongezea nini?
“Mwanzo walisema alikuwa anafukuza mirungi na pikipiki, wakati anazuia pikipiki yenye mirungi ikaja pikipiki nyingine yenye mirungi ikamgonga akaangukia kwenye kisiki akafa, jambo ambalo lilizua taharuki kidogo kwa sababu ukweli ulikuwa unajulikana,” alidai Mwenyekiti huyo wakati akizungumza na Mwananchi
Wanadanganya hata pasipodanganyika
 
Back
Top Bottom