Wanasemaga "meno ya mbwa hayaumani" sasa hapo sijui imekuwaje
Kwa maelezo ya mtoa mada, muuaji alifanya kama mzaha kutokana na kauli ya kujutia aliyoitoa baada ya kuua.
Hukumu ya kosa hilo hataiepuka kwa sababu kafanya uzembe usiomithilika wenye kuweza kuepukika, kalibeba sasa ni lake na litamkost sana.
Kifupi, kosa hilo nami nusura linikumbe enzi zetu zilee!
Kuna siku kiutani utani tu, hapa na hapa(zero distance) nikamnyooshea jamaa yangu bastola bila kuihakiki nikijua kwamba ipo tupu!
Kilichonisaidia mpaka leo huwa nasema ni Mungu pekee na siku zangu za kuadhirika na kudhalilika zilikuwa hazijapangwa!
Ile bastola sijui ni nani aliyeitumia na kuiacha ikiwa na risasi chemba kisha kurudisha hamer mbele bila ya kutoa risasi kwanza!
Katika mzaha huo, roho ilikuwa ikinituma nirudishe hamer nyuma kisha nifyatue ili katokee kale kamlio 'ndaa' kama jokes za kikamanda!
Roho ilisita, nikatoa magazine, kuangalia haina risasi, lakini niliopoikoki, lahaulah risasi ilikuwa chemba ikadondoka!
Nilinywea na kukosa raha hadi leo siwezi kusahau, lakini nikaficha mzaha huo wa kifo niliotaka kuufanya.
Katika mafunzo ya kutumia silaha, hata bunduki isiwe na risasi hauruhusiwi kuelekeza mtu, unatakiwa kuelekeza juu ama chini.
Pole kwa wafiwa, pole kwa muuwaji ninajua hakudhamiria, lakini hapo mkosi wa kimaisha tayari ushamkumba.