Kilimanjaro: Askari amuua mwenzake kwa ugomvi wa kukaa siti ya mbele

Huu ni mfano mzuri wa jinsi kesi zinavyo pindishwa
 
Hata Kama hamna risasi hauruhusiwi kumnyoshea mtutu wa bunduki Askari mwenzio au mutu yoyote,ukishitakiwa kwa kumnyoshea Ni sawa na kutishia kuua hata Kama Haina risasi.
 
Kuanzia Tittle, contents na comments nimekua nasoma huku nasmile. Yaani kusema kweli sijawahi umia nikisikia habari mbaya za hawa jamaa.
 
Askari unamnyooshea mwenzako silaha

JKT si wanafundisha bunduki hata kama haina risasi ni haramu kumuelekezea mtu
 
Hii inaniingia kiaina!
 
Hivi mtoto wa kiume unaanzaje kushobokea gari lá mwanaume mwengine?
 
Linus Valentino mkatoliki Safi, Footballer Hadi tukakubatiza Cazorla way back Tarime Sec!!


Hakika umetutoka kamanda nenda ndugu yangu!!
 
Hairususiwi kabisa kumuelekezea mwenzio bunduki hata kwa bahati mbaya na ni kosa kubwa jeshini ukionekana umemuelekezea mwenzio bunduki.
Unahukumiwa kama uliyejaribu kuua.
Hairuhusiwi kbs hata kubambikiza kesi.....lakin ona wanavyofanya!!
 
Wanasemaga "meno ya mbwa hayaumani" sasa hapo sijui imekuwaje
Kwa maelezo ya mtoa mada, muuaji alifanya kama mzaha kutokana na kauli ya kujutia aliyoitoa baada ya kuua.

Hukumu ya kosa hilo hataiepuka kwa sababu kafanya uzembe usiomithilika wenye kuweza kuepukika, kalibeba sasa ni lake na litamkost sana.

Kifupi, kosa hilo nami nusura linikumbe enzi zetu zilee!

Kuna siku kiutani utani tu, hapa na hapa(zero distance) nikamnyooshea jamaa yangu bastola bila kuihakiki nikijua kwamba ipo tupu!

Kilichonisaidia mpaka leo huwa nasema ni Mungu pekee na siku zangu za kuadhirika na kudhalilika zilikuwa hazijapangwa!

Ile bastola sijui ni nani aliyeitumia na kuiacha ikiwa na risasi chemba kisha kurudisha hamer mbele bila ya kutoa risasi kwanza!

Katika mzaha huo, roho ilikuwa ikinituma nirudishe hamer nyuma kisha nifyatue ili katokee kale kamlio 'ndaa' kama jokes za kikamanda!

Roho ilisita, nikatoa magazine, kuangalia haina risasi, lakini niliopoikoki, lahaulah risasi ilikuwa chemba ikadondoka!

Nilinywea na kukosa raha hadi leo siwezi kusahau, lakini nikaficha mzaha huo wa kifo niliotaka kuufanya.

Katika mafunzo ya kutumia silaha, hata bunduki isiwe na risasi hauruhusiwi kuelekeza mtu, unatakiwa kuelekeza juu ama chini.

Pole kwa wafiwa, pole kwa muuwaji ninajua hakudhamiria, lakini hapo mkosi wa kimaisha tayari ushamkumba.
 
Hivi mtoto wa kiume unaanzaje kushobokea gari lá mwanaume mwengine?
Siyo la mwanaume mwingine.

Kutokana na maelezo ya mtoa mada, hiyo ni gari ya serikali.

Kwenye magari ya serikali unayemuona kakaa mbele kaweka na 'kipeps' dirishani ndiye boss wa wenzake na ndicho walichokuwa wanagombania kwamba nani akae mbele aonekane boss(nadhani walikuwa ni cheo kimoja).

Mambo ta vijana ukiyasikiliza yatakushangaza sana.
 
Duuuh najaribu kuwaza yule askari aliye mnyooshea Nape bastola angejisahau kidogo tungekuwa tunaongea mengine. Cha kustikisha unaweza kuta bado anakula mshaara wa serikali wakati alifanya makosa makubwa sana.
 
Laana ya kubambikiza watu Bangi na kesi za ajabu hata wasiohusika...
..Una Hoja kubwa hapo Mkuu. Kumbuka na yule wa kule Mwanza ambaye tuliambiwa amezama baharini wakati akimfukumza mhalifu!
Mhalifu alipojitupa ziwani ili kuwakimbia Polisi Askari naye akajitosa Ziwani kumkimbiza ila akajikuta akikamwa na nyavu za kuvua samaki na akazama?
Karma??[emoji848][emoji848]
 
Hawa jamaa askari waliwahi mrubuni bodaboda wangu Bangi wakamkamatisha, nikaitwa mwenye pikipiki kituo cha sekei Arusha wanataka million moja waachie pikipiki, sitasahau... Story ndefu lkn hizi ni laana
 
Kama Police kwa Police wanaficha ukweli. Vipi kwa mwananchi wa kawaida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…