Kilimanjaro Hotel Korogwe bei ya vyakula ipo juu sana

Nakubali..
 
Umesema vema. Ila wapuuzi washangaaji huwa ni wengi sana. So ungemwambia wapuuzi wengi tu kukushangaa. Nchi hii asilimia 80 ya watu hawana exposure na wanaropoka tu wakiona mtu hafanyi mambo ambayo wao wamekariri. Ukimuuliza mtu why habebi chakula wengi ni kuogopa macho ya watu hao washamba wasiojua. USHAMBA NA CONFIDENCE NI SHIDA SANA🖐😀
 
Wanauza bei ghari harafu nyama haitupwi inauzwa yote hata iliyoharibika pana siku nimepewa nyama choma mbovu naona wapo busy kutoa risiti za efd ila lishe hasa zile za kuchoma wanauza hata zilizoharibika ziliwa za moto kugundua ni ngumu sana...
 
Pana muda safari unapata ya dharula Mkuu sio safari zote za kujiandaa ukanunue kuku ichomwe usafiri na nusu, nusu utambae nayo pamoja na Chapati...
 
Mimi huwa nafanya maandalizi navyosafiri nanunua kilo ya nyama/kitimoto elfu 7000 nakaanga naweka kwenye watpot nakula mpaka nafika nimetosheka balaa

Mambo yakununua kipande kimoja kwa elfu tano nilishayaacha zamani Sana hotel nyingine mbaya zaidi kuna hotel ata chips zilale yeye anaangalia faida
 
Juzi kati hapo Kilimanjaro bus Korogwe nilinunua anadazi dogo tu kwa elfu moja na kikombe cha maziwa fresh elfu mbili.
Wanajiona bab kubwa utadhani ni ndani ya airport.
Anyway labda wanafidia gharama za kujenga na mishahara ya wale wanaosafisha vyoo ambavyo abiria hujisaidia bure.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…