Kilimanjaro Hotel Korogwe bei ya vyakula ipo juu sana

Kilimanjaro Hotel Korogwe bei ya vyakula ipo juu sana

hotel sio charity, NGO kama hutak Bei mbaya (elekezi) ukishuka nenda toilet then kapige picha na wauza matunda kule barabarani
 
Pole mwenyewe juzi kati nimefika Dodoma usiku pale Chako ni chako nikanunua mbuzi na ndizi za kuchoma wamenifungia gari imeondoka nafika mbele nifungue nile nakuta wamejaza shingo ndogondogo za kuku badala ya mbuzi na ndizi mbichi. Halafu wanauza bei balaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miongoni mwa upumbavu ninaouchukia ni kutoa hela nyingi na kupewa chakula kidogo siku nitakojolea chakula cha mtu kwa hasira ntakung'uta kabisa pump isibaki hata na tone la mkojo ndani ntaukamulia wote kwenye sahani
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee toka nyumbani ukiwa umeshiba...! Ata kama ni usiku wa manane, kula kama una kula daku msimu wa ramadhani
Huko kujishindilia kabisa home Mambo yanaweza yakaenda kombo ukiwa ndani ya basi kibaya zaidi unaweza kushindwa hata kujamba kwa kuhofia uliyekaa naye siti moja atakuchukuliaje ukibanwa na kimba ndio itakuwa fedheha zaidi hakuna rangi utaacha kuiona utabadilisha mikao ya kila aina lakini kimba msimamo wake upo pale pale kwamba "niachie njia nipite bwana mkubwa"
 
ni hela ya kawaida tu, Ila kwa kweli hali ni ngumu sana ndio mana mambo madogo tu yanatushuhulisha.
 
Hata kihotel Chao cha hapo shekilango bei mkasi , wali maharage tuu 3500
 
Heshima sana,

Jana nilikuwa natokea Dar kwenda Arusha.Muda wa saa 2 asubuhi tukapitia hotel ya Kilimanjaro Bus pale Korogwe.
Nikaagiza mtori na sambusa tatu na mwenzangu naye akaagiza kama mimi.Baada ya kumaliza tukaletewa bill kibakuli cha Mtori tsh 5,000 sambusa moja 2,000.

Nikawauliza huu mtori wa ndizi mbili tatu na nyama mbili sh 5,000 na sambusa 2,000 nikaambiwa ndio duh nikalipa bill kwa mshangao.

Nikaondoka kuendelea na safari mbele kidogo ipo hotel nyingine parking imejaa kweli kweli tofauti na Kilimanjaro.Kwakuwa muda wa saa 2 asubuhi magari mengi yalikuwa binafsi nikagundua wadau wa usafiri njia ya Dar to Arusha wameistukia hotel ya Kilimanjaro inauza vyakula bei za kiukraine.

Nilichojifunza wasafiri wanaotumia mabus ya Kilimanjaro wanauziwa vyakula bei kubwa na hawana option labda turejee zama zile za kusafiri na vyakula.
Mazee ulitoka na basi gani Chugga na kufika Korogwe saa 2?
 
Back
Top Bottom