Kilimanjaro: Mume adaiwa kumuua mkewe na kumjeruhi mtoto mchanga

Kilimanjaro: Mume adaiwa kumuua mkewe na kumjeruhi mtoto mchanga

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanaume mmoja, mkazi wa Mero, wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kumuua mkewe na kumjeruhi mtoto mchanga kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.

Mwanamke huyo ambaye anatambulika kwa jina la Fausta Tesha (26) aliuawa kwa kukatwa na kisu sehemu za tumboni, kifuani na ubavuni pamoja na kichanga chake kujeruhiwa usiku wa kumkia jana, Februari 23, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Polisi, mtoto huyo mchanga wa wiki mbili amelezwa katika hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu baada ya kuchanywa tumboni na kusababisha utumbo kutoka nje.

======

kichanga-pic.jpg

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanaume mmoja, mkazi wa Mero, wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kumuua mkewe na kumjeruhi mtoto mchanga kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.

Mwanamke huyo ambaye anatambulika kwa jina la Fausta Tesha (26) aliuawa kwa kukatwa na kisu sehemu za tumboni, kifuani na ubavuni pamoja na kichanga chake kujeruhiwa usiku wa kumkia jana, Februari 23, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Polisi, mtoto huyo mchanga wa wiki mbili amalezwa katika hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu baada ya kuchanywa tumboni na kusababisha utumbo kutoka nje.

Akizungumza na Mwananchi digital jana Februari 23, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simoni Maigwa amesema wanamshikilia mwanaume huyo kutokana na mauaji ya mke wake.

"Mwanaume huyu amemuua mke wake na kumjeruhi mtoto wa wiki mbili kwa wivu wa mapenzi, huyu mwanaume alienda kwenye machimbo huyu mwanamke akawa amepata ujauzito, sasa ikaonekana kuna mgogoro wa familia juu ya huyu mtoto," amesema.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori amelaani tukio hilo na kutoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kuchukua sheria mkononi na kusema wanaofanya vitendo kama hivyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

"Serikali tunakemea vikali matukio kama haya na sio ustaarabu na kama kwenye familia kuna utofauti kuna vyombo vya sheria, hakuna sheria inayoruhusu mtu kumuua mwenzake kwasababu ya tofauti zao, kama kunakutofautiana basi vyombo vya sheria vipo na sio kuuana,” amesema.

Cc. Mwananchi digital
"Huyu Mwanaume"
Yaani hana jina? Seems huyo Mwanaume ni tishio sana kiasi kwamba juna lake haliwezi kuwa disclosed
 
Alikuwa provoked
Nakwambia akipata wakili mzuri miaka itapungua. Mbona kesi nyingi zipo za hivyo

Ngoja utaona,
Kesi za mauaji mara nyingi zenye vifungo vilivyopungua ni zile zinazotokea kama ajali, lakini za scenario ya tukio Hilo haijatokea Kwa ajali. Ni mauaji ya Dhamiri hata kama yaliongozwa na hasira ya muda mrefu
 
Wewe nae sijui umesomea wapi....kwani nimesema hatafungwa?? Hata kukuelewesha nilichoandika basi....maana nshaona mwenzangu sio
Wewe nae sijui umesomea wapi....kwani nimesema hatafungwa?? Hata kukuelewesha nilichoandika basi....maana nshaona mwenzangu sio
Umeandika kwa mihemko bila kuangalia uzito wa kesi ya mauwaji ya kukusudia vipi kama hata hakuwa na ndoa.?kulikuwa na sababu gani ya kuuwa watu wawili ndivyo mnafundishwa kutatua matatizo kwa kisingizio mapenzi yanauma? Kama alikuwa ana madai yenye msingi kwann hakwenda kudai kisheria...?
 
Inasikitisha sana,Jamaa ni mental cases , mtoto ana wiki 2 unamchana tumbo? Binti ametoka kujifungua ndani ya week mbili unamuonea wivu wa kimapenzi?
 
Inasikitisha sana,Jamaa ni mental cases , mtoto ana wiki 2 unamchana tumbo? Binti ametoka kujifungua ndani ya week mbili unamuonea wivu wa kimapenzi?
Either hujasoma uzi au una kichwa kizito. Kulikuwa na hisi tangu awali kwamba mimba imepatikana wakati mume yupo machimbo..., so inawezekana ukweli kaugundua ghafla
 
Je kama alieweka mimba alikuwa nae anatoa za matumizi pengine hata zaidi? hii mijitu yenye wivu kwanza ndo huwa haijui hata kutunza mke...
Sasa si aende akaishi na huyo anaehudumia? Ya nini kuhatarisha maisha yako na mtu humpendi?
 
Either hujasoma uzi au una kichwa kizito. Kulikuwa na hisi tangu awali kwamba mimba imepatikana wakati mume yupo machimbo..., so inawezekana ukweli kaugundua ghafla
Mimba iliingia bila mume kushiriki akiwa machimbo

Kwahiyo ukienda Machimbo ndiyo mtoto anakuwa siyo wako? What if kama alitungisha mimba na ndiyo akenda Machimbo? Wapi kwenye hayo maelezo wamesema kwamba jamaa alienda machimbo wakati mkewe alikuwa hana mimba? Kwahiyo mmeconclude kwamba jamaa alivyoenda machimbo mpaka anarudi alikuwa hajui kwamba mkewe mjamzito/amejifungua?
 
Back
Top Bottom