Kilimanjaro: Mume adaiwa kumuua mkewe na kumjeruhi mtoto mchanga


Kwahiyo mgogoro juu ya mtoto ulianza alipofika nyumbani na kukuta mkewe ana mtoto wa wiki mbili? Ina maana alivyoenda machimbo hadi anarudi alikuwa hajui kama mkewe mjamzito/amejifungua?
 
"Mwanaume huyu amemuua mke wake na kumjeruhi mtoto wa wiki mbili kwa wivu wa mapenzi, huyu mwanaume alienda kwenye machimbo huyu mwanamke akawa amepata ujauzito, sasa ikaonekana kuna mgogoro wa familia juu ya huyu mtoto," amesema



uwe unasoma taarifa mpaka mwisho acha kukurupuka
 
Inasikitisha sana,Jamaa ni mental cases , mtoto ana wiki 2 unamchana tumbo? Binti ametoka kujifungua ndani ya week mbili unamuonea wivu wa kimapenzi?
Tofautisha wivu wa mapenzi na USALITI WA NDOA, mtu akisalitiwa anaweza kufanya lolote.
 
Kwahiyo mgogoro juu ya mtoto ulianza alipofika nyumbani na kukuta mkewe ana mtoto wa wiki mbili? Ina maana alivyoenda machimbo hadi anarudi alikuwa hajui kama mkewe mjamzito/amejifungua?
NDIO, Kwa Mujibu wa Taarifa ya Police inaonyesha Jamaa hakujua hayo. Angejua Mapema kuna possibility angeshamuua Mkewe hata kabla Mtoto hajazaliwa.

Sijajua kwanini unafikiria kwamba Mwana Apollo alikuwa na taarifa tokea day One. Kipi kwenye hio taarifa ya Police kimefanya uamini hvyo?
 
Tofautisha wivu wa mapenzi na USALITI WA NDOA, mtu akisalitiwa anaweza kufanya lolote.
Taarifa inasema Wivu wa Kimapenzi halafu mbele wanasema "inasemekana" means Assumption

Hiyo ya wivu wa kimapenzi ni Confirmed ila ya Mgogoro juu ya mtoto ni Assumption according to taarifa ya polisi wenyewe.
 
MWANZO 4:11
Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako
Biblia Walawi 20:10
10. “Kama mwanamume akizini na mke wa jirani yake, ni lazima wote wawili wauawe."
Na damu yao itakuwa juu yao wenyewe"

Huyo ni Bwana Mungu mwenyewe muumba mbingu na nchi anamwambia Nabii Musa, kama Mungu mwenyewe aliona wasaliti wa ndoa wauwawe, si ajabu ukasikia binadamu kufanya hivyo, binadamu tonatofauti na wanabadilika kulingana na maZingira.
 
Kwamba huyo jamaa aliporudi hakuuliza mtoto katoaka wapi , au kamdanganya vipi?
 
Watu wanalaumu tuu bure
Imagine umeenda kumtafutia mkeo halafu huku nyuma anagawa utamu hadi mimba anapata na kuzaa juu ....hivi maumivu yake yanavumilika? Kila mtu Ana moyo wake wa kukabiliana na usalitii.
Mwache aende,umemwoa ana wazazi hujamiliki pumz yake....umemshindwa mwache aende
 
Bado unaishi kwenye agano la kale?😅😅😅stuka,chukua hatua maana kwa kupigwa kwake sisi tumepona,alipowambwa msalabani kwa aibu na siku ya 3 akafufuka,alisema yametimia ,ya kale yakafutwa tukaanza upya 🙏🙏
 
Mimi nilimshauri aende mirembe tu, ndo maana umeona sijibizani nae tena
 
NDIO, Kwa Mujibu wa Taarifa ya Police inaonyesha Jamaa hakujua hayo. Angejua Mapema kuna possibility angeshamuua Mkewe hata kabla Mtoto hajazaliwa.
Ok.
Sijajua kwanini unafikiria kwamba Mwana Apollo alikuwa na taarifa tokea day One. Kipi kwenye hio taarifa ya Police kimefanya uamini hvyo?

Alikuwa na taarifa kwasababu si alikuwa mkewe? Kama alimficha kwanini polisi waseme direct kwamba ni wivu wa kimapezi? kwanini wasingesema kwamba chanzo ni kuzaa nje ya ndoa baada ya mwamba kwenda machimbo na kumficha mmewe? Wivu wa kimapenzi means hisia kwamba unachapiwa(Not confirmed).
 
JF ni Home of Great Thinkers ,digest taarifa siyo unameza tu bila kufikiria.

Polisi:
Mwanaume huyu amemuua mke wake na kumjeruhi mtoto wa wiki mbili kwa wivu wa mapenzi,

Assumption.
huyu mwanaume alienda kwenye machimbo huyu mwanamke akawa amepata ujauzito, sasa ikaonekana kuna mgogoro juu ya huyu mtoto

Polisi ilitakiwa waseme direct chanzo ni kuzaa nje ya ndoa wakati mmewe akiwa machimbo na siyo wivu wa kimapenzi.
 
Mwanaume anahitaji kipawa kuhimili wivu wa mapenzi. Imagine unahisi mkeo anafuga mimba ya mwanaume mwingine nyumbani kwako.
Unatulia tu ,unasubiri kumlea malaika.Hivi kama Yusufu angekurupuka si angemsaidia vizuri Herode?
 

Kwa andiko hili hiyo hukumu aliyopewa huyo mama haina haki
Yuko wapi aliyezini nae!?
 
Wadada wadada wadada nimewaita mara tatu..

Wanaume tukivurugwa na mapenzi sisi 90% lazma afe mtu kama unaona mkaka wa watu humpendi ondoka muache sio unakaa unakula vyake kumbe humpendi...

Ka unaona kaka wa watu shoo mbovu sepa nenda huko kwny shoo kali usiendelee kula vyake mwsho wake akijua huwa sio mzuri kama tunavoona hapa...

Wanaume hawasamei lazma ki happen...
 
Mwanaume anahitaji kipawa kuhimili wivu wa mapenzi. Imagine unahisi mkeo anafuga mimba ya mwanaume mwingine nyumbani kwako.
Inauma kama pasi ila busara tu hapo inahitajika,muachane kwa amani ya bwana baasi akikataa sepa zako atajua mwenyewe
 
Ila ukifikiria deep mpaka mtu anaua sio bure sometime wadada wana jeuri sana hasa huko kaskazin mweee,nshawahi jibiwa fanya unachokitaka,kuepusha shari anakufuata we si mwanaume huna lolote,nkatoka nje nkazomewa dah kama si kujishusha mwenyew nlitaka kumvunja mikono yote miwil
 

Wivu wa Mapenzi kwa Lugha ya kipolisi sio Hisia za kuwa Unachapiwa, Kwa Lugha ya kipolisi Wivu wa Kimapenzi ni sababu iliyopeleka hilo tukio. Yaani hata Ukimfumania Wife anagongwa(uka Confirm) then ukalawiti mgoni wako, Police kwenye report yao bado watasema umetenda kosa la Ulawiti kutokana na Wivu wa Mapenzi.

WIVU WA MAPENZI kwenye report ya Police sio Hisia, ila ni KISABABISHI kilichopelekea Mtuhumiwa kufanya uhalifu. haijalishi alithibitisha au hakuthibitisha.

 

Kwahiyo Said aliyempiga risasi 7 mkewe na yeye kujiua chanzo ni wivu wa kimapenzi au missed call 42(Simu)?


Polisi wajitafakari sababu zao ,haiwezekani kuzaaa nje ya ndoa/Kubambikiwa mtoto iwe ni wivu wa kimapenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…