Kilimanjaro: Mwalimu agomea kuhama, vitu vyake vyatolewa nje Siha

Kilimanjaro: Mwalimu agomea kuhama, vitu vyake vyatolewa nje Siha

Hii imekaa kimkakati
Kwamba kwenye ualimu Kuna walimu Fulani ni Bora kuliko wengine?

Wanamtupa kule ili wamweke mtu wao
Sehemu anayo kwenda ni porini sana
Huu ujinga ndio hautakiwi kabisa katika nchi hii kuna upuuzi mwingi sana.
 
Jambo la busara ni kuangalia sababu ya huyu jamaa kugoma sio kuhamishwa maana hizi kujiamulia tu hutaki wakati kuna sehem za kutoa sababu za kutokuhamishwa.
Kwanini sasa hawataki kumsikiliza badala yake wanataka wanamburuza?
 
Kule ni porini, karibia na msitu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro, Nina wasiwasi hata huduma kama zinapatikana?

Unajua kadhia za uhamisho?
Embu mlipe stahiki zake
Ina maana Shule imejengwa Porini?

Huo Usalama anaozungumzia kama concern, vipi kuhusu Walimu na Wanafunzi ambao tayari wapo kwenye hiyo Shule? Kwao ni salama lakini kwake siyo salama?
 
Huu ndio uonevu usio na kichwa Wala miguu.
Halafu Cha kushangaza wanamuona tatizo ni yeye
Huko mawilayani kuna ukenge mwingi sana mkuu. Mtu usipokuwa imara, wanaweza hata wakakutia vijiti makalioni. Huyu jamaa wanamuonea bure na hawana sababu ya msingi ya kumlazimisha kuhama.
 
Unauhakika gani hawajafuata utaratibu? Wilaya nyingi walimu wamekuwa wakihamishwa kuziba mapengo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo vya watumishi wengine, uhaba wa walimu wa kutosha kwenye somo fulani. Kuna kitengo maalum ndani ya Wilaya ambao kazi yao ni kufanya uhamisho wa namna hii.
Kuhama sio jinai mkuu. Lakini kwanini wamhamishe kimabavu bila kufuata utaratibu na kwa kumdhalilisha hadharani? Wewe ungehamishwa kinyama hivyo ungefurahi?
 
Polee sana mwalimu wasichokijua ni kwamba mwalimu hahami ndani ya halmashauri yake. Ndo maana kuna walimu kama watano wa shule X Uchagani walishahamishwa kitambo ila familia zao bado zinaishi quarters
 
Ina maana Shule imejengwa Porini?

Huo Usalama anaozungumzia kama concern, vipi kuhusu Walimu na Wanafunzi ambao tayari wapo kwenye hiyo Shule? Kwao ni salama lakini kwake siyo salama?
Kwanini hawataki kumsikiliza? Huoni kwamba wanamtega? Kwenye halmashauri kuna uonevu mwingi sana mkuu.
 
Polee sana mwalimu wasichokijua ni kwamba mwalimu hahami ndani ya halmashauri yake. Ndo maana kuna walimu kama watano wa shule X Uchagani walishahamishwa kitambo ila familia zao bado zinaishi quarters
Kuna wapuuzi wengine humu hawajui ugumu wa kuhama ndio maana wanashabikia mwalimu kuhamishwa kimabavu bila kufuata utaratibu.
 
Maji ni ya shida pande hizo?
hapo kila mwanafunzi anabeba ndoo kuteka maji asubuhi

Walimu ni wito!
 
Aliitwa akaambiwa aseme ni usalama gani hakuweza kujieleza kwa mkurugenzi jamaa akaenda hadi kwa waziri mkuu na mkurugenzi na kitengo Cha uhamisho Wilaya ya Siha kikamuita jamaa hakutoa sababu zenye mashiko sasa unataka hawa viongozi wafanye je mkuu?

Huko anapoenda hamna walimu wengine, unajua anyway ila watu wanatumia fursa za shule zenye watoto wengi kwaajili ya fursa za kibiashara wanazopata na huduma ambazo shule zinatoa kama makazi.
Kwani usalama wa familia sio hoja mkuu? Wewe unataka kumpangia sababu? Kwa maana hiyo kumbe inaonekana wewe ni mmojawapo wa watu wanaomnyanyasa huyu mwalimu kwa kumhamisha kinyama bila utu. Mungu anawaona.
 
Kwanini sasa hawataki kumsikiliza badala yake wanataka wanamburuza?

Maana ya kuitwa ni nini? Maana ya timu ya uhamisho kwenda alipo kuongea na nini? Maana ya kupewa barua ya kujieleza ni nini?
 
Kwani usalama wa familia sio hoja mkuu? Wewe unataka kumpangia sababu? Kwa maana hiyo kumbe inaonekana wewe ni mmojawapo wa watu wanaomnyanyasa huyu mwalimu kwa kumhamisha kinyama bila utu. Mungu anawaona.

Hivi mtu utasema tu unahofia usalama wako bila kutoa sababu maalum? Je ni ugomvi kati yako na mwalimu mwingine au ni ugomvi gani?

Kwahiyo unaposema usalama unahofia watu wanaangalia mashiko ya sababu uliyotoa sio kuhamishwa tu kwasababu ya maneno.
 
Kuhama sio jinai mkuu. Lakini kwanini wamhamishe kimabavu bila kufuata utaratibu na kwa kumdhalilisha hadharani? Wewe ungehamishwa kinyama hivyo ungefurahi?

Thibitisha uhamisho huo ni wa kimabavu kutokana na dai unalitoa.
 
Back
Top Bottom