unachoshangaa ni nini wakati hapa niko huru kutumia rejista ya neno/istilahi/contex/sarufi/grammer nitakavyo? Elewa sipo darasani nao unakosoa sentensi hizo hizo kana kwamba nalazimika kutumia lugha, kiswahili sanifu/proper english. Hapa huwa tuko huru kutumia misamiati na maneno fulani kulingana na mukhtadha wa mada na unaandika ukiwa wapi. Sijaandika habari/makala gazetini kiasi cha kulazimika kutumia lugha na maneno sahihi, hata hivyo si kazi yangu kuhariri na kuhakiki usahihi wa manenoUmesema wewe ni mwalimu wa English!!!!!! Hii ni hatari zaidi ya danger.
Majority ni Wachaga na Wapare ndo wanaongelewa hapa!mind kuwa Kilimanjaro yote si ya wachaga na wapare tu kuna vieneo vina makabila mengine kama wakahe, waarusha na wamasai huko ukanda wa chini moshi vijijini
hapa tunapiga stori mzee wangu, sifundishi darasani. Darasani huwa naandaa cha kufundisha kwa mujibu wa miongozo ya ufundishaji inaitwa Azimio la kazi na Andalio la somo. Darasani hukurupuki kufundisha mada, unaadaa lengo kuu na lengo mahsusi na utakaguliwa na wakaguzi na wadhibiti mambo ya elimu shuleni. Usione tunatumia maneno na sentensi za ajabu humu ukajua ndio tulivyo. Hapa ni jukwaa huru, kuna uhuru wa kutumia lugha na maneno upendavyo ila si kutweza utu wa mtu na matusi. unajua maneno kama uroda, mbunye, hogo, mkuyenge, kibamia, kunyandua na mengine mengi yasiyokuwepo kwenye kiswahili sanifu au kiingereza sanifu? haya maneno tunayatumia kwa mukhtadha wa majadiliano fulani kukwepa kuandika maneno makali tunatumia tafsida kuficha neno halisi ikiwa kuliandika ni aibu si vema! Humu hatuandiki sentensi/maneno ya lugha fulani kwa kukurupuka huwa tunajua usahihi wa maneno hayoUmesema wewe ni mwalimu wa English!!!!!! Hii ni hatari zaidi ya danger.
Exactly,huwa hawapendi mtu ajifanye kidume mbele yao au kuwavimbia huwa wanapatwa na kinyongo fulani sasa hapo ndio wataanza kudili na wewe halafu kumbuka wenyewe wanakuwaga na muda mwingi sana wa kushinda nyumbani na familia biashara zao ni simpo tu za kuangua nazi na kuuza kwenye genge so hautaweza kushindana naohawanaga shida wale kama huwaoneshi dharau ila ukiwa unakulakula wake zao hovyohovyo watakushughulikia kwa njia yoyote wanayoona inafaa ikiwa ni pamoja na ushirikina
offering?? Ndio imekushangaza na kuona upeo wangu umeishia hapo? naona una bold maneno yangu kwa rangi nyekundu kuwa nimeandika kimakosa huku mimi ni mwalimu wa lugha hiyo! Hapa niko huru kuandika nitakacho ikiwa tu sivunji terms and ruleles za humu. Sifundishi lugha sahihi ya kuandika humu. Humu huwa tunatumia maneno na sentensi za ajabu ajabu mradi tu zinaeleweka kwa unaojadili mada na wao, hatuangalii makosa ya sarufi na miundo ya sentensi iwe kiswahili sanifu au kiingereza, tunachosoma ni mukhtadha wa mada tuUmesema wewe ni mwalimu wa English!!!!!! Hii ni hatari zaidi ya danger.
Hii ni hatar sana Kwa usalama wa taifaHuko huko Kilimanjaro vipo vijiji vina wakazi wake ni dini fulani wazazi hupenda zaidi watoto wao wafundishwe walimu wa dini yao. Sipati picha huko Pangani, Kilwa, Mafia, Mkuranga hali ikoje kwa mwalimu asiye wa dini ya wenyeji kufundisha watoto wao. Maeneo mengine ya nchi hali ni shwari hakuna ukabila wala udini, walimu ni changanyikeni
kuna maeneo nchi hii ukipangiwa kufundisha huko unakuta wanafunzi ni wa dini fulani, watoto wana dharau balaa wanaona wanafundishwa na kafiri, hawazingatii unachowafundishaHii ni hatar sana Kwa usalama wa taifa
Wewe ni mental case kusema ukweli.sasa kama mtoto ni mzembe asichapwe? Nitamchapa mpaka akili zimkae sawa
Exactly,usiowaonyeshe kwamba unajiona matawi ya juu na kuwafanya mademu wao ni wachafu au hutaki kujumuika kwenye shughuli mbalimbali kama harusi na misiba hapo watakuonesha.Hili la kukomeshwa na kufanyiwa jeuri ikiwemo vitendo vya kishirikina baada ya wenyeji kuona una dharau lipo sana tu huko vijijini. Wenyeji hawataki udharau mazingira yao. vyakula vyao, maji yao na hata mademu wao, watapenda ushiriki vitu vyao na upate demu wao kabisa watafurahi kuwa unawathamini
we mama vipi? Unajua maana ya motisha na aina zake au umeamua tu kuni crash?Wewe ni mental case kusema ukweli.
Yaani unapenda matumizi ya mabavu kuliko akili.
Kitu cha kutumia akili wewe unatumia mabavu halafu eti ulipitia chuo cha ualimu ukafundishwa code of conduct and ethics zinazohusiana na ualimu.
Ndiyo maana kuna haja ya walimu kupitishwa japo short course ya sheria kadhaa kama sheria ya elimu, sheria ya mtoto na sheria chache zinazohusiana na watoto kidogo ingesaidia kuwatoa ujinga walioujaza vichwani mwao.
Mkuu kuna walimu walipaswa kutibiwa kwanza changamoto ya akili pale Mirembe ndiyo wapewe kibarua cha ualimu.Ila walimu nao hupenda sana kujitaftia matatzo wao wenyew sasa mtoto kusahau bag na kumkabidhi ni kitu cha kumchapa kweli mbna walimu wa tz wanapenda kuhamisha stress zao kwa wanafunzi me naona yote wanayapitia sawa tu Mungu nae anaamua kuwaadhibu kwa namna anayojua yeye
Eti maana ya motisha?😆we mama vipi? Unajua maana ya motisha na aina zake au umeamua tu kuni crash?
Unazidi kudhihirisha ulivyo kilaz,a kuliko hata tunavyodhani.Kuchapwa watoto wataendelea kuchapwa sana tu. Nani ambaye hajui haki za watoto na matamko ya kimataifa juu ya haki za watoto? Watanyukwa sana tu
Eti maana ya motisha?
Kamwe sitalea ujinga shuleni, nidhamu kwanza ndiyo huduma itolewe. kama mnalea watoto wenu vibaya shuleni watanyooshwaUnazidi kudhihirisha ulivyo kilaz,a kuliko hata tunavyodhani.
Yaani unajikuta mjanja kuchapa mtoto asiye na uwezo wa kukabiliana na wewe huku ukijiona mshindi.
Nikuhakikishie una mwisho mbaya sana kama hutobadili mindset za kijima maana jela ipo jirani na wewe.
Najua kwasasa utaona kama jambo lisilowezekana ila ni suala la muda tu zamu yako itafika na utakuja kukumbuka haya ninayoyasema humu kila mara wakati huo ni too late.
Yupo mwalimu mmoja mkoani Njombe tulienda kwa ziara maalum ya kutembelea shule mbalimbali tukaambiwa tabia za yule mwalimu tukakaa naye pamoja na walimu wengine tukaelimishana lakini baadae tulivyoondoka alikaza fuvu.
Kilichomtokea alimuadhibu mtoto akamsababishia ulemavu wa kudumu hivi tunavyoongea ana mvua zake kadhaa anatumikia.
Kujionea ni kuamini. Kila la heri kwenye matumizi ya mabavu.
Tamaduni za kasikazini nitoka nyakati hizo za Baba wa Taifa hivyo gusa unase .. endKuna shule moja huko moshi vijijini kata ya Arusha Chini/TPC Mkoani Kilimanjaro mi na mwenzangu kutoka Lushoto mkoani Tanga, mwenzangu huyo ni msambaa tulipangiwa shule tukakuta walimu ni wachaga watupu wa Kibosho na Uru tu, Tulitishika kidogo ila tulipata moyo kwa kuwa hata hao walimu si wazawa wa kijiji hicho kilichopo ukanda wa Moshi Chini, kule ni waarusha chini na wamasai nako jamii ya pale ilitamani sana kupata walimu wazawa wa eneo hilo. Baadaye mwenzangu alirudi kwao kwa uhamisho wa kubadilishana wilaya nikabaki peke yangu katikati ya wachaga, Bahati nzuri staff iligawanyika pande mbili hasimu mi nikawa neutral katikati ya walimu wachaga sikuogopa kutengwa na kubaguliwa sababu nilikuwa mkali mno kwenye ubaguzi wa kikabila kwa hoja kuwa mi ni mtanzania napangwa kazi mahali popote Tanzania. Kule Kilimanjaro kuna shule utakuta walimu ni wachaga tu au wapare tu. Akitokea ofisa elimu ni mchaga walimu wachaga hufurahia hali kadhalika akiwa mpare walimu wapare hufurahia wanaona watasikilizwa shida zao