Habari wataalam,
kwa mara ya kwanza nimefika katika ardhi isemekanayo kutukuka kwa rutba na mvua za kutusha kwa kilimo cha mahindi kiukweli nimeshawishika sana kuingia katika kilimo cha mahindi japo kilimo cha kutegemea mvua ya mungu kupata ni majaliwa ya mola lakini mimi nitarisk na nimeplan kuanza na heka kumi (10) kulingana na uchumi wangu.
Nilichokipenda zaidi huku kulimo sio gharama sana gharama kubwa ni yakukodi shamba na kulima kwa trekta basi habari za mbolea hamna kabisa inasemekana ardhi hii inarutba ya kutosha kabisa kustawisha mazao bila kutegemea mbolea.
Kwa hesabu zangu za kawaida gharama ya kulima ekta 10 ni sawa mchanganuo huu chini..
Kukodi chamba 1kt = 30,000/- @10 (300,000/-)
Kulima kwa trekta 1kt = 30,000/- @10 (300,000/-)
Kupanda 1kt = 10,000/- @10 (100,000/)
Palizi 1kt =10,000/ @10x2 ( 200,000/-)
mbegu (200,000/-)
JUMLA. 1,100,000/-
Tuweke laki5 ya dharura ikitokea labda wadudu kununua dawa au kubadilika kwa bei ya vitu vingine
Jumla kuu itakua 1,600,0000/-
Sasa basi kwa kawaida kabisa kilimo kikitiki kwa ekta moja kupata gunia 7 ni kawaida kabisa sasa tuchukulie kiwango hichi cha chini kwa gunia7 kwa ekta kwaiyo sasa 7x 10 = 70 na kwa kawaida kabisa gunia moja kuuzwa elfu60 ni bei ya chini hivyo basi 70 x 60,000/- =( 4,200,000/)
Ukitoa hela niliowekeza (4,200,000/-1,600,000 =2,600,000/- ) napiga bingo la 2.6M kwa kipindi cha miezi 3 tu.
Naomba kuwasilisha nakaribisha mawazo na ushauri kutoka kwa wadau wa kilimo hasa kama umewai kulima kiteto.