Kilimo cha Kisasa cha Mahindi: Mbegu bora, Mbolea bora na magonjwa

Kilimo cha Kisasa cha Mahindi: Mbegu bora, Mbolea bora na magonjwa

Kwa kawaida mbolea ya kupandia ni mfuko 1.kwa eka.
 
Mbegu ziko nyingi ila Mimi Niko kanda ya kati natumia Zamseed kwa eka 3 ni kg 6 yaani pakti 3 za kilo mbilimbili
 
Kuna mbegu ya DK 80 - 53 pia inafanya vizuri maeneo mengi nchini na pia inavumilia mabadiliko ya Tabia ya nchi yaani hata kukiwa na mvua nyingi utavuna na kukiwa na mvua chache utavuna
 
SOURCE: Kilimo cha Kisasa cha Mahindi | Mogriculture Tz

Mbegu Bora za mahindi
Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:
  • Mbegu za asili: Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo
  • Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile zilizoboreshwa kutoka mbegu za asili. Kundi hili linagawanywa kwenye makundi mawili – composite varieties na mbegu chotara (Hybrids).

Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa sababu ya:
  • Mwinuko kutoka usawa wa bahari
  • Kiasi cha mvua katika eneo husika
  • Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa

Mbegu za mahindi zilizoboreshwa ni kama TMV1, TAN 250, TAN 254, Staha, Situka na zingine zote zinazoanza na herufi “H” kama vile H 250, H 251 na H 615. Pia mbegu mpya zilizotangawa na Kamati ya Taifa ya Mbegu mwaka huu ni WE4102, WE4106, WE4110, WE4114, WE4115 kutoka ARI ILONGA.

Jinsi Ya Kuweka Mbolea Za Kupandia
Mbolea hizi zinawekwa shambani kabla ya kupanda/kusia mbegu. Zinawekwa kwa njia mbalimbali kama vile kusambaza kwenye eneo husika na kuchanganya na udongo, au kuweka kwenye mistari au mashimo ya kupandia. Ni bora zaidi kuchanganya mbolea za Minjigu Phosphate au Minjingu Mazao na udongo kuliko kutia kwenye shimo la kupandia. Pia kuchanganya mbolea na udongo huondoa athari za mbolea kwenye uotaji wa mbegu, hasa kama kuna uhaba wa unyevunyevu.

Viwango Vya Mbolea Za Kupandia mahindi
Kiwango cha mbolea za kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 fosfati (P) kwa hektari ambayo ni sawasawa na kiasi cha mifuko 2 ya DAP (= mfuko mmoja kwa ekari). Ikiwa mbolea ya minjingu phosphate itatumika basi mifuko mitatu itatosa kwa hekta (= mfuko mmoja na nusu kwa ekari). Na endapo utaamua kuitumia mbolea ya minjingu mazao basi tumia mifuko minne na nusu kwenye hekta moja au mifuko miwili kwa ekari moja.

Upandaji wa mahindi
Muda wa kupanda:
Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzonimwa mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to 15th day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti mwanzoni. Katika msimu huu utayarishaji wa shamba hufanyika mwezi wa pili mwanzoni.

Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na majira ya mvua. Kwa mfano katika wilaya ya Morogoro tarehe za kupanda ni kuanzia februari 15 hadi Machi 15. Mkulima anashauriwa afuate kalenda ya muda wa kupanda kama anavyoshauriwa na bwana shamba wake.

Nafasi ya kupandia mahindi
Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za kilimo inayomwezesha mkulima kupata mazao bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupanda kwa mistari na kufuata nafasi zinazoshauriwa na wataalamu wa kilimo. Zifuatazo ni nafasi za kupanda mahindi na idadi ya mbegu kwa kila shimo na kiasi cha mbolea (kwa vizibo vya soda) inayotakiwa kuwekwa kwa shimo:
  • Kwa nafasi ya 90 sm X 30 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea
  • Kwa nafasi ya 90 sm X 25 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea
  • Kwa nafasi ya 90 sm X 50 sm, panda mbegu mbili na uweke vizibo viwili vya mbolea

Kupalilia
Ni muhimu shamba lipaliliwe baada ya mimea kuota ili kuondoa magugu. Magugu ni mimea hivyo hushindana na mimea iliyopandwa na mkulima kwa kunyonya virutubisho ardhini. Magugu yanaweza pia kuhifadhi wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo kupunguza mavuno. Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono (yaani) kung’olea (ikiwa magugu yapo mbali mbali sana) au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (herbicides) hasa 2-4D.

Mbolea za kukuzia mahindi
Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha naitrojeni. zifuatazo ni mbolea za kukuzia na kiwango chake cha naitrojeni:
  • UREA: 46% N
  • Calcium Ammonium Nitrate, CAN: 23% N
  • Sulphate of Ammonia, SA: 21%

Urea inakirutubisho cha naitrojeni (N) kwa kiwango kikubwa na watu wengi wanauzoefu nayo. Vilevile bei yake ni nafuu ikilinganishwa na mbolea zingine za kukuzia. Mbolea hii iko katika hali ya chengachenga za mviringo (granules) za rangi nyeupe. Kiwango cha urea ni nusu kizibo cha soda kwa kila shina. Mbolea hizi hazidumu kwenye udongo kwa muda mrefu kwa hiyo huwekwa shambani wakati mimea inapokuwa na mahitaji makubwa ya kirutubisho cha naitrojeni na wakati udongo una unyevunyevu na shamba halina magugu.

Pia wakulima hutumia mbolea za kukuzia zinazopatikana kwa bei nafuu kama vile BOOSTER (foliage nitrogeneous fertilizers) ambayo hupigwa kwa kunyunyizia katika majani ya mmea kila baada ya wiki 3, kwa mara 2-3 mpaka mahindi kuvunwa. Kiwango cha kupiga ni mchanganyo wa mls 50-80 ktk lita 15 za maji. Mbolea za kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la mimea au pande mbili au tatu au nne za kila shina. Cha muhimu ni kwamba mbolea isirundikwe sehemu mmoja. Minjingu Mazao (kg 50/ekari = gramu 10kwa shimo) pia yaweza tumika kwa kukuzia, hivyo mkulima yko huru kuchagua kulingana na uwezo na upatikanaji wake.

Viwango Vya Mbolea Za Kukuzia Vinavyoshauriwa

Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi cha mifuko miwili ikiwa utatumia UREA. Hata hivyo mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. Hivyo basi utumie mifuko mitatu kwa hekta ambayo ni sawa na mfuko mmoja kwa ekari. CAN inaweza kutumika kama kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium na endapo utaitumia basi mifuko minne na nusu itatosha kwa hekta, ambapo kwa ekari moja utatumia mifuko miwili tu.

Kwenye mahindi mbolea ya kukuzia inawekwa baada ya palizi ya kwanza ambayo ni kama wiki tatu mpaka wiki nne baada ya kupanda. Kwa kila mmea mmoja weka kiasi hiki cha mbolea:
  • UREA: kizibo kimoja cha soda
  • CAN: vizibo viwili vya soda, na
  • SA: kizibo kimoja cha soda

Mambo Muhimu Ya Kuzingatia
Kuweka mbolea:
Sehemu za nchi ambazo muda wa kukua mahindi ni mrefu (zaidi ya miezi mitatu), ni vyema kuweka mbolea za kukuzia mara mbili, yaani nusu ya kiwango kinachopendekezwa baada ya mwezi mmoja, na kurudia tena (kutumia nusu iliyosalia) baada ya wiki tatu.

Kupalilia: Katika kilimo cha mahindi, ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda. Wataalamu wanashauri kwamba katika kilimo cha mahindi, shamba lipaliliwe mara 2-3, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.

– Utafiti unaonyesha kwamba, shamba la mahindi ambalo halijapaliliwa linaweza kupunguza mavuno kwa asilimia 60 hadi 100 ya mavuno yanayotarajiwa. Hata kama mkulima atatumia mbegu bora, aina na kiasi cha mbolea zinazoshauriwa, kupanda kwa mstari pamoja na mbinu nyingine bora zinazoshauriwa, bila kupalilia hali hii itaathiri mavuno yake.

KUVUNA, KUKAUSHA, KUSAFISHA NA KUHIFADIHI

Kuvuna
Mahindi yako tayari kuvuna wakati kikonyo kimekuwa dhaifu na mahindi yanaangalia chini. Mahindi yakishakauka vizuri yanatenganishwa na bua halafu majani ya mhindi kutolewa.

Kukausha
Kama mahindi hayajakauka vizuri hukaushwa zaidi katika juani siku 3-4 ili kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni muhimu mahindi yakauke vizuri ili yasioze yakiwekwa ghalani. Ili kujua kama mahindi yamekauka vizuri, tia mahindi kadhaa kwenye chupa ya soda iliyokauka na uongeze kiganja kimoja cha chumvi. Tingisha chupa halafu uwache itulie kwa dakika tatu. Chumvi ikikwama kando ya chupa, basi mahindi hayajakauka vizuri.

Kusafisha
Mahindi yaliyokauka vizuri hupepetwa na vilevile mahindi mabovu huondolewa.

Kuhifadhi
Mahindi huhifadhiwa ghalani baada ya kuwekwa viatilifu vya kuzuia bungua wa mahindi Njia za kisasa za uhifadhi hutumiwa kama vile matumiz ya ACTELLIC SUPER DUST katika uwiano wa 1kg kwa gunia 5-10 za ujazo wa 100kg. Kiatilifu kingine ni actellic solution katika rate ya 5mls katika gunia moja la kg 100. Njia nyingine ya kienyeji katika kuhifadhi mahindi ni kuweka juu ya ghala ambalo chini yake kuna jiko la kupikia ambalo hutoa moshi unaotumika kufukuza na kuua wadudu.

SOURCE: Kilimo cha Kisasa cha Mahindi | Mogriculture Tz

Karibu kwa majadiliano...
Mpaka sasa mkulima aliyefanikiwa ni yule aliyekamata Bombadia kule canada, ukulima ni tusi (we mshamba nini?)
 
Labda uweke stoo usubiri njaa ianze ndio uuze
 
Habari wataalam,

Kwa mara ya kwanza nimefika katika ardhi isemekanayo kutukuka kwa rutba na mvua za kutusha kwa kilimo cha mahindi kiukweli nimeshawishika sana kuingia katika kilimo cha mahindi japo kilimo cha kutegemea mvua ya mungu kupata ni majaliwa ya Mola lakini mimi nitarisk na nimeplan kuanza na heka kumi (10) kulingana na uchumi wangu.

Nilichokipenda zaidi huku kulimo sio gharama sana gharama kubwa ni yakukodi shamba na kulima kwa trekta basi habari za mbolea hamna kabisa inasemekana ardhi hii inarutba ya kutosha kabisa kustawisha mazao bila kutegemea mbolea.

Kwa hesabu zangu za kawaida gharama ya kulima ekta 10 ni sawa mchanganuo huu chini..

Kukodi shamba 1kt = 30,000/- @10 (300,000/-)
Kulima kwa trekta 1kt = 30,000/- @10 (300,000/-)
Kupanda 1kt = 10,000/- @10 (100,000/)
Palizi 1kt =10,000/ @10x2 ( 200,000/-)
mbegu (200,000/-)

JUMLA. 1,100,000/-
Tuweke laki tano ya dharura ikitokea labda wadudu kununua dawa au kubadilika kwa bei ya vitu vingine
Jumla kuu itakuwa 1,600,0000/-

Sasa basi kwa kawaida kabisa kilimo kikitiki kwa ekta moja kupata gunia 7 ni kawaida kabisa sasa tuchukulie kiwango hichi cha chini kwa gunia7 kwa ekta kwaiyo sasa 7x 10 = 70 na kwa kawaida kabisa gunia moja kuuzwa elfu60 ni bei ya chini hivyo basi 70 x 60,000/- =( 4,200,000/)

Ukitoa hela niliowekeza (4,200,000/-1,600,000 =2,600,000/- ) napiga bingo la 2.6M kwa kipindi cha miezi 3 tu.

Naomba kuwasilisha nakaribisha mawazo na ushauri kutoka kwa wadau wa kilimo hasa kama umewai kulima kiteto.
Yaani ardhi ina rutuba afu unasema Hekari moja itoe gunia 7 sasa hapo rutuba iko wapi!
 
Nimepanga kulima maeneo ya kijingu mkuu pia kuna shamba jingine nimepata maeneo ya lantomoni ila bado sijafanya maamuzi yakulichukua.
nilijaribu heka kumi na hesabu zilikua kama zako nilipata 482,000 sema sijui dogo alinipiga ngoja mkuu nijipange nitakutafuta maana nataka nisimamie mwenyewe kabisa
 
Ukiona mwaka kiteto wamevuna mahindi kwa wingi jua gunia itakuwa elf25 nawewe utauza kwa bei iyo,huwezi pata elf60 kwa miezi mitatu labda baada ya miezi 7 kuelekea mwaka unaofuata,sisi ndo ma-settler wa kiteto tuulize,kwanza kwenye mchanganuo wako sijaona gharama ya kupukuchua,makuli,usafiri,stoo.nk. vip unalima kiteto maeneo gani tufahamiane
Salamu Settler 900 ....vipi nikitaka kufanya Biashara mkishavuna nije nifanye Biashara gani kwenu walowezi na wapagazi wa Kiteto!
 
Habari wataalam,

Kwa mara ya kwanza nimefika katika ardhi isemekanayo kutukuka kwa rutba na mvua za kutusha kwa kilimo cha mahindi kiukweli nimeshawishika sana kuingia katika kilimo cha mahindi japo kilimo cha kutegemea mvua ya mungu kupata ni majaliwa ya Mola lakini mimi nitarisk na nimeplan kuanza na heka kumi (10) kulingana na uchumi wangu.

Nilichokipenda zaidi huku kulimo sio gharama sana gharama kubwa ni yakukodi shamba na kulima kwa trekta basi habari za mbolea hamna kabisa inasemekana ardhi hii inarutba ya kutosha kabisa kustawisha mazao bila kutegemea mbolea.

Kwa hesabu zangu za kawaida gharama ya kulima ekta 10 ni sawa mchanganuo huu chini..

Kukodi shamba 1kt = 30,000/- @10 (300,000/-)
Kulima kwa trekta 1kt = 30,000/- @10 (300,000/-)
Kupanda 1kt = 10,000/- @10 (100,000/)
Palizi 1kt =10,000/ @10x2 ( 200,000/-)
mbegu (200,000/-)

JUMLA. 1,100,000/-
Tuweke laki tano ya dharura ikitokea labda wadudu kununua dawa au kubadilika kwa bei ya vitu vingine
Jumla kuu itakuwa 1,600,0000/-

Sasa basi kwa kawaida kabisa kilimo kikitiki kwa ekta moja kupata gunia 7 ni kawaida kabisa sasa tuchukulie kiwango hichi cha chini kwa gunia7 kwa ekta kwaiyo sasa 7x 10 = 70 na kwa kawaida kabisa gunia moja kuuzwa elfu60 ni bei ya chini hivyo basi 70 x 60,000/- =( 4,200,000/)

Ukitoa hela niliowekeza (4,200,000/-1,600,000 =2,600,000/- ) napiga bingo la 2.6M kwa kipindi cha miezi 3 tu.

Naomba kuwasilisha nakaribisha mawazo na ushauri kutoka kwa wadau wa kilimo hasa kama umewai kulima kiteto.
Duh aisee mtu anapalilia ekari mzima kwa elf 10? Jipange kukabiliana na changamoto zaidi ya hizi
1. Usimamizi hakikisha 95% unasimamia ww mwenyewe front shamba
2. Kukutana na bei za uzalishaji tofauti na hizo ulizoziandika
3. Kutowapata vibarua kwa wakati, waaminifu na wavumilivu
 
Kongolee
Ila mimi nahitaji mbegu chotara ya maharage ya njano , soya au meupe niko Pwani naipata wapi?
 
Binadamu wasikuvunje moyo maana Kama wanasema ( wanaume wa dar) na huku wanaamini ili ufanikiwe lazima uje dar inakuaje
Mpaka sasa mkulima aliyefanikiwa ni yule aliyekamata Bombadia kule canada, ukulima ni tusi (we mshamba nini?)
 
Back
Top Bottom