Kilimo cha Maharage: Mbinu za kulima, Ushauri na Masoko yake

Kilimo cha Maharage: Mbinu za kulima, Ushauri na Masoko yake

Gharama zake za ulimaji bila kujali eneo zimekaaje na misimu ya ulimaji wake?
Mkuu kuhusu kulima ni bora uchek sehemu unayolima maana kuna wengine wanalima kwa tractor wengine mkono. So bei zina vary kwahilo ungeuliza wenyeji sehemu unayolima 2. Msimu wa kulima ni mwezi wa 3 mwishoni mpaka wa nne mwanzoni na miezi ya 10 kipindi cha mvua za vuli.
 
Mbegu nzuri ya maharage inategemeana na eneo

Ila Rozi koko au njano ni Bora zaidi Na zina Bei sana,pia soko linategemeana Na eneo husika mfano si huku Huwa tunauza nchi jirani ya Uganda Kwa kuwa Wanabei nzuri Sana
 
1) Natumia 6ltr@acre
2) kawaida namwagilia mara 10 mpaka kuvuna maharage kulingana na hali ya hewa.(6ltr*10=2500*6*10=>150,000/-)
3) natumia mbolea ya CAN Kg50@are=>Tsh90000
4)Tsh200,000 kulima na kuchora muelekeo wa utiririkaji wa maji.
5)booster 2ltr@6000=>12,000
6)fungicide=>40,000
7)insecticide=>48,000
8)mbolea supergro tsh 250,000.
9)palizi nafanya mwenyewe
10) navuna na kupokea mkwanja nikiwa shamba. Siku hiyo lazima nichinje jogoo kwajili ya mteja!

Karibuni sana shamba.
Ukiamua kuchagua upande huu utakuwa njia sahihi.
Usimtegemee mwajiri wako maana anakutumia kwa ujira finyu na ukizeeka hatakuhitaji kamwe.
Janjaruka mwanangu usiwe poyoyo!!
Mkuu kisima
 
Ndiyo mkuu!
Shida yangu ipo kwenye huo mchanganuo hapo Juu Kuna sehemu unasema kuwa Kuna baadhi ya vitu unafanya mwenyewe.

Na nakumbuka niliwahi kuku-quote kuhusu kuweka Msimamizi ukasema sio vizuri sasa tatizo mimi hata niwe hapo field bado kulima hiyo heka tu mtihani.

Sasa naomba gharama za watu kulima hata kama nitakua hapo eneo husika?

Maana kila mikipiga gharama bado nakwama sehemu hiyo.

Shukrani
 
Shida yangu ipo kwenye huo mchanganuo hapo Juu Kuna sehemu unasema kuwa Kuna baadhi ya vitu unafanya mwenyewe.

Na nakumbuka niliwahi kuku-quote kuhusu kuweka Msimamizi ukasema sio vizuri sasa tatizo mimi hata niwe hapo field bado kulima hiyo heka tu mtihani.
Sasa naomba gharama za watu kulima hata kama nitakua hapo eneo husika?
Maana kila mikipiga gharama bado nakwama sehemu hiyo.

Shukrani
Ok mkuu!
Mara nyingi bei huwa ni maelewano.

Kwa wewe usietaka kushika jembe gharama zitakuwa juu kiasi.
Kuna kulima shamba kwa ng'ombe au trekta sh45000@acre

Kuna kudraft shamba kwa kuchorea mifereji,kusawazisha level na kutengeneza majaruba sh150000-200000

Kuna palizi sh40000@acre

Kuna kumwagilia sh 10000@acre siku ya kumwagilia na sh 10000@acre kupiga dawa.

Gharama nyingine ni wakati wa kuvuna na kupiga.
 
Ndiyo mkuu!
Bwana kisima nataka fanya hichi kilimo.mwaka huu nipo, morogoro, kilosa kijiji kimoja kina itwa Rudewa..

Sorry napenda kuuliza kwa haraka harakamakadirio ya china kabisa Heka moja ina weza kutoa kilo.ngap za.maharage au gunia ngap!??
 
Bwana kisima nataka fanya hichi kilimo.mwaka huu nipo, morogoro, kilosa kijiji kimoja kina itwa Rudewa..

Sorry napenda kuuliza kwa haraka harakamakadirio ya china kabisa Heka moja ina weza kutoa kilo.ngap za.maharage au gunia ngap!??
Mkuu pitia post zote kuna uzi tayari nimejibu haya uliyouliza.
 
Mkuu pitia post zote kuna uzi tayari nimejibu haya uliyouliza.

Boss kuna mdau kauliza kuhusu mbegu, je zinapatikana wapi.? Au ni maharagwe hayohayo uliyovuna unatenga mengine ya mbegu, Na ni mbegu kiasi gani zinatosha kwa hekari.?
Pia ni maeneo yenye hali ya hewa ipi yanafaa kwa kilimo hiki.?
Na vipi ni majira gani ya mwaka yanafaa kuanza kilimo hiki.?
 
Je,maeneo ya milimani huku Same, Kilimanjaro zao linaweza kustawi kwa kutegemea mvua za msimu mfano vuli?
 
Je,maeneo ya milimani huku Same, Kilimanjaro zao linaweza kustawi kwa kutegemea mvua za msimu mfano vuli?
Ndiyo mkuu huko ndipo penyewe haswaa.
Angalizo kuu, maharage hayahitaji mvua nyingi na ukungu huathiri zaidi.
Ni mhimu kilimo hiki ukakifanya kwa mfumo wa bustani ukiwa umejiandaa na mbolea na viuatirifu vitatikanavyo.
 
Boss kuna mdau kauliza kuhusu mbegu, je zinapatikana wapi.? Au ni maharagwe hayohayo uliyovuna unatenga mengine ya mbegu, Na ni mbegu kiasi gani zinatosha kwa hekari.?
Pia ni maeneo yenye hali ya hewa ipi yanafaa kwa kilimo hiki.?
Na vipi ni majira gani ya mwaka yanafaa kuanza kilimo hiki.?
Awali nilichukua mbegu nanenane baadae nikawa naandaa mwenyewe.

Kama ni kilimo cha kutegemea mvua, tegesha mvua za mwishoni ukiwa umejiandaa dawa ya ukungu na wadudu.

Udongo mweusi wa mabondeni unafaa zaidi kwa kilimo hiki.

Ukanda wa baridi ndo mahala pake kwa kilimo cha maharage.

Andaa debe moja la maharage kwajili ya mbegu ya ekari moja.
 
Mbeya wanalima maharage wanapandia DAP tu mpk wanavuna hamna mbolea nyingine na madawa pekee. Palizi mara 1 au 2 tu...ila maharage sio zaid ya 10 mavuno.
 
KILIMO BORA CHA MAHARAGE (Phaseolus vulgaris)

UTANGULIZI
Maharage ni zao jamii ya mikunde ambalo hulimwa kwa ajili ya kuliwa kama mboga au futari.linaweza kama maharage mabichi au maharage makavu.Pia majani yake mni chakula cha mifugo na yanatumika pia kama mboga kwa binadamu.katika ekari moja unaweza kupata Kg 600 hadi 1200 za maharage.

HALI YA HEWA IFAAYO
Hustawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 1000 hadi 2000 kutoka katika usawa wa bahari .Pia yanaweza kulimwa pungufu ya mita 1000 au zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari.Maharage huitaji mvua ya kutosha kipindi cha kabla ya uwekaji maua na kipindi cha ukuaji wa vitumba vya maharage.Huitaji unyevu kidogo kipindi cha kuweka maua na ukavu kipindi cha kukomaa na kukauka vitumba.Maharage hulimwa kwa wingi MBEYA,IRINGA,KIGOMA,ARUSHA,MOSHI,morogoro n.k

UDONGO
Hustawi vizuri katika udongo usiotuamisha maji na ambao ni mfinyanzi kichanga ambao una mboji ya kutosha wenye pH 5.5 - 7.Pia unaweza kulima katika udongo wa aina tofauti tofauti.

MBEGU BORA ZA MAHARAGE
Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za maharage kama vile canadian wonder,Tengeru,Uyole,SUA,Ilonga na Lyamungo.

UPANDAJI
Maharage hupandwa mwishoni mwa msimu wa www.kilimofaida.blogspot.commvua kuepusha kunyeshewa kipindi cha uekaji maua.Yanawezwa kupandwa mwezi Februari,machi,aprili inategemea mvua katika eneo lako zinaisha mwezi gani,hivyo hakikisha angalau yanapata mwezi mmoja wa mvua ya kutosha.Fukia mbegu zako katika kona cha sm2.5 hadi 4 katika ardhi kutegemea na aina ya udongo shambani kwako.

Maharage hupandwa kwa kutumia mbegu ambazo ni safi na hazijaharibika kwa kuvunjika au kuliwa na wadudu.Kabla ya kupanda maharage yako unaweza kuyatibu kwa kutumia Rhizobia bacteria ambapo itakupunguzia matumizi makubwa ya mbolea za nitrojeni.

NAFASI YA UPANDAJI

Maharage yapandwe kwa nafasi ya sentimeta 40-60 mstari hadi mstari na sentimeta 8 -15 shina hadi shina.

MBOLEA
Unaweza kupanda katika shamba lililotawanywa mbolea ya samadi.
Pia uanweza kwa uzuri zaidi kupandia mbolea za viwandani kama vile TSP au MInjingu mazao au minjingu kwa kiasi cha kg 50 -100 kwa ekari.

Wakati wa mmea kuanza kuweka maua unaweza kutumia mbolea ya N.P.K au SA au Kwa Kiasi Kidogo CAN au UREA Angalizo Mbolea hizi zikizidi maharage huwa na majani mengi kuliko maua na kusababisha mavuno kuwa machache.

UPALILIAJI
Upaliliaji inabidi ufanyike mapema mara tuu maharage yanapoota na kshamba kuwa na magugu.Palizi ya kwanza inaweza kufanyika Kati ya siku 8-12 baada ya mmea kuota na yapili ifanyike siku ya 20- 30 baada ya palizi ya kwanza.ILi kuyarinda maua ya maharage yako yasipukutike wakati wa palizi hakikisha unaepuka palizi kipindi cha uwekaji maua.

WADUDU
Funza wa maharage ni wadudu wanaoshambulia mimea michanga ya maharage. Funza wa maharage hawa huweza kusababisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100 kufuatana na hali ya hewa-unyevu kidogo, rutuba kidogo, kuwepo kwa maotea ya aina ya maharage na magonjwa kwenye udongo, kurudia kupanda zao la maharage kila msimu na aina ya naharage.

Njia nzuri ya kudhibiti funza wa maharage ni:-
1. Kupanda mapema
2. Kupakaza mbegu dawa kama endosufan, Acephate, Murtano (mchanganyiko wa dawa ya fungas na wadudu) nasaidia kuzuia funza wa maharage na visababishi vya kuozesha mizizi.
TAHADHALI: Dawa ya Murtano ni sumu kali hivyo mbegu zenye dawa hii zisitumike kwa chakula.
3. Kunyunyizia dawa mfano DUDUBA au DUDUALL Karate 5EC au Actellic 50EC ndani ya siku 4 hadi 5 baada ya maharage kuota.
4. Kupanda mbegu zenye afya kwenye udongo wenye rutuba.
5. Kupanda mbegu zenye ukinzani wa funza wa maharage.
6. Kuweka matandazo kama pumba ya mpunga husaidia kuotesha mizizi mipya n kurudisha afya ya mmea wa maharage

Pia maharage yanaweza kushambuliwa na wadudu mbalimbali kama vile nzi weupe wa maharage na wengineo ambao wanweza kuzuiwa kwa kutumia dawa mbalimbali za wadudu.

MAGONJWA

Magonjwa maarufu ni ndui ya maharage, madoa pembe, kutu, magonjwa yanayosababishwa na bacteria na virusi. Mbegu iliyoambukizwa, udongo na takataka za maharage ni vyanzo vikubwa vya uambukizaji kwa magonjwa yote isipokuwa ugonjwa wa kutu ya majani.
1. Punguza athari kwa kupanda mbegu safi, zenye afya zisizo na vidonda/ magonjwa, aina zinazovumilia na kutunza shamba.
2. Panda kwa mzunguko wa mazao ya jamii nyingine.
3. Ondoa na kuchoma yaliyougua.
4. Tumia dawa zilizopendekezwa kama Kocide, Funguran, Bayleton n.k kwa kuzuia magonjwa yanayosababishwa na ukungu na bacteria.

UVUNAJI

Maharage huvunwa mara tuu yanaponza kukauka na kabla vitumba havijapasuka.Ng'oa mashina ya maharage na na upigepige kuyaondoa katika vitumba vyake.

KUHIFADHI

Baada ya kuyapiga na kupeta kuondoa uchafu yaanike juani kwa siku kazaa kuhakikisha yamekauka na hayana unyevu unaoweza kusababisha yapate fangasi.yahifadhi katika magunia,kama yatakaa muda mrefu bila kuliwa basi hakikisha unayahifadhi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu kama vile Shumba, Kama vile ACTELLIC DUST au MALATHION. au Tumia mifuko maalum ya kuhifadhia nafaka.
 
Awali nilichukua mbegu nanenane baadae nikawa naandaa mwenyewe.

Kama ni kilimo cha kutegemea mvua, tegesha mvua za mwishoni ukiwa umejiandaa dawa ya ukungu na wadudu.

Udongo mweusi wa mabondeni unafaa zaidi kwa kilimo hiki.

Ukanda wa baridi ndo mahala pake kwa kilimo cha maharage.

Andaa debe moja la maharage kwajili ya mbegu ya ekari moja.
Habari mkuu?naomba nikutembelee hapo Moro nijifunze kitu kuhusu kilimo hiko cha maharagwe ya njano,namba zangu ni 0783724242/0713724242
 
Back
Top Bottom