Kilimo cha Maharage: Mbinu za kulima, Ushauri na Masoko yake

Unaweza kulima kwa greenhouse na makisio ya gharama ya greenhouse ya hekari 2 ni tshs ngapi na unaweza kupata ngunia ngapi kipindi cha mavuno?
 
Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi mzuri,, nna swali dogo tu kwako. Maharage tunalima kwa wingi sana hapa TZ ( wa kwanza kiafrika ) Na nadhani zaid ya 100% yanatumika kwa kula.

Nnavojua moja ya sifa ya maharage ukila wee itakua ni kujamba tu cku nzima hata kama umekula mlo mmoja tu na ndo mana hua silagi hizi mbegu kwa sbb hiyo tu. Sasa najiuliza nimimi tu au? Kama ni kwa wote huko makazini mnakaaje asee?
 
Asante kwa elimu, nafikir maharage ni sawa mazao mengine, kwan kuna aina hustawi vizur sehem ya barid na mengine ukanda wa joto, naomba kufaham ni aina ipi ya mbegu hustawi vizur ukanda wa joto na ipi ukanda wa baridi
 
Mbegu nzuri ya maharage inategemeana Na eneo
Ila Rozi koko au njano ni Bora zaidi Na zina Bei sana,pia soko linategemeana Na eneo husika mfano si huku Huwa tunauza nchi jirani ya Uganda Kwa kuwa Wanabei nzuri Sana
Upo wapi?
 
mi pia nimelima mwaka huu ila nilichopata hakiridhishi ni kama nimerudisha mbegu tu.
 
mi pia nimelima mwaka huu ila nilichopata hakiridhishi ni kama nimerudisha mbegu tu.

uskate tamaa mdau. uvumilivu ni kitu cha kuwa nacho kwa % kubwa sana. ikiwezekana fuatilia mbinu ulizotumia pengine ndio ziliku-letdown lkn ni vema sana ukalima tena tena maana kama ukifuata taratibu zote hakina jembe halimtupi mtu mkuu..
 


Daaah mkuu Kisima uko vizuri thanks kwa kuwa wazi pia mkuu mimi ni mkulima pia ntakucheki kwa maongezi fulani mkuu.
 

Hekari moja ya maharage inagharimu kipimo cha ndoo ambacho kwa mikoa yetu ni kama debe moja. Mbegu nzuri kwa sasa ni kipapi or kibranketi zamani maharage ya Mbeya, ila kluna mbegu inaitwa DRK ya UYOLE inahimili hali zote za hewa. Maharage yanachukua miezi mitatu mpaka yavunwe. Kwa upandaji wa kisasa hekari moja inaweza kutoa mpaka madebe 32, zaidi ya gunia tano.

Kwa maharage ya kipapi ambayo ndiyo marketable kwa sasa bei yake ni 30000 mpaka 40000 kwa debe.

Sitakuwa mwingi wa busara nisipoeleza msala ulionipata mwaka huu. Nililima maharage mapema sana mwezi Desember mvua ilipiga kidogo baada ya hapo ilikata shamba zima lilikauka. Nikapanda tena hali kadharika mvua haikuwa vyema ikawa yenye kunyesha mno na kukata ni maeneo ya mbalizi nikavuna kiasi ambacho mtu mzima hawezi kukiandika hapa katika shamba langu la maharage.

Awamu ya pili baada ya kuvuna nimepanda tena ila safari hii mvua imekata maharage ndo kwanza yanatokeza katika mmea na wala sio mimi tu, ila wanakijiji wote sehemu niliyolima.

Nitoe unabii bei ya maharage kuwa ya kushangaza mwaka huu, ila ni hali ya hewa tu mwakani nitaingia shambani nikiwa na morali zaidi
 
Je, ili yazae vema, yahitaji kufanya nini?
mfano kwa mbeya upandio mbolea hasa ya DAP then piga busta baada ya kama wiki moja zisizidi wiki mbili, usikose kupiga dawa ya wadudu na ukungu mwisho yanapotoa maua rudia tene busta na ya ukungu.... space is the matter of at most importance harage kwa harage sm 5 na mstari kwa mstari sm40 Nonchalant Alejandroz
 
Ndugu kisima naomba unisaidie kwa hili Kilimo mseto yaani maharage na mahindi na maharage pekee vip katika mavuno kuna utofauti sana
 
Mkuu kwa hali ya hewa y mbozi mbeya vipi yanastawi mana kuna kaubaridi zaidi

Pia soko kwa maeneo ya nyanda za juu kusini vipi una uzoefu nalo

Na la mwisho nikupongeze sana kwa ushauri nzuri.

Nitakuja kukitrmbelea kabla sijaanza mana natarajia kuanza kilimo wakani mwezi wa kwanza hasa maeneo ya mbeya nataka niteke mkoa kwa kilimo cha maharage aina yote hope utakua mentor wangu mkuu mungu akubaliki sana.
 
Mkuu Kisima mimi ni mkulima nalima Mahindi, sijawahi kulima maharage, booster ni kitu gani?
 
Mkuu Kisima mimi ni mkulima nalima Mahindi, sijawahi kulima maharage, booster ni kitu gani?
Booster ni kirutubisho cha mimea.

Kipo katika mfumo wa kimiminika.

Mara nyingi husaidia kustawisha maua na kuboresha matunda.

Booster yenye viambata vya Zinc na Boron ni nzuri sana ikatumika kipindi cha maua na matunda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…