Haijarishi ni mkoa gani unaishi ila kuna miezi nyanya zinakuwa adimu kiasi cha kuuziwa nyanya moja sh 200. Uzoefu nilionao mimi miezi ya nov-april soko la nyanya ni zuri sana karibu maeneo mengi nchini.
Usilogwe kukutanisha mavuno na nyanya za magole/mateteni morogoro, debe wanauza sh1000. Hii ni miezi ya july,aug na sep. Wanauza kwa bei ya kutupa coz uzalishaji wao hauna gharama. Hawamwagilii maji na hutumia kiasi kidogo cha dawa na mbolea.
Nashauri mkulima survey hali soko kabla hujalima na kawaida nyanya huchukua miezi 4 kuanzi kitaruni mpaka kuvuna.