Humble African
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 4,781
- 14,415
Aswaa kwa greenhouse nadhani itakulipa zaidi mkuu!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wapendwa naomba mwenye ujuzi juu ya hilo zao naomba tushee ujuzi, pia mwenye mchanganuo kuanzia kulima, mbegu bora hadi kuvuna,nataka nilime nyanya kwaajili ya kuuza, asanten sana kwa michango yenu.
Na Ukitaka Mbolea nzuri na yenye kukuletea faida ya mazao yako ya nyanya bonyeza hapa.Wadau naomba mwenye uzoefu wa kilimo hiki hasa kipindi cha masika. Nataka nianze mwezi wa kumi ili nivune kama mwezi wa kwanza kipindi mvua inapokuwa kali na nyanya kuwa adimu.
Shamba lipo Mbeya ukubwa wa hekari mbili. Mtaji nataka niweke maximum wa 3mil kwa hekari zote mbili.
Naomba mnisaidie challenge nitakazokutana nazo mbegu nitatumia anna f1.
cc: malila
Wadau naomba mwenye uzoefu wa kilimo hiki hasa kipindi cha masika. Nataka nianze mwezi wa kumi ili nivune kama mwezi wa kwanza kipindi mvua inapokuwa kali na nyanya kuwa adimu.
Shamba lipo Mbeya ukubwa wa hekari mbili. Mtaji nataka niweke maximum wa 3mil kwa hekari zote mbili.
Naomba mnisaidie challenge nitakazokutana nazo mbegu nitatumia anna f1.
cc: malila
Mkuu Shanty F1 unaweza kulima nje (siyo kwenye green house) wakati wa masika? mavuno yake yakoje kwa mche au Kwa ekari moja?Habari JF Senior, nimeona ujumbe wako kuhusu ushauri wa kilimo, sisi Balton Tanzania ltd tunatoa huduma zifuatazo;
mbegu bora za nyanya inaitwa shanty F1,ina ngozi ngumu ambayo inaweza kukaa kwa mda mrefu baada ya kuvuna (shelf life). Pili kilimo unachotaka kufanya anza mwezi 8 au 9 ili uvune mwezi wa 11-3 kwa mbegu ya shanty F1, lakini ukitaka kilimo chenye tija zaidi nakushauri utumie drip irrigation ili ikusaidie wakat wa kipindi cha kiangazi (off season), nazo tunatoa kwanzia 250sqm mpaka 4000sqm(1acre) na bei zetu ni nafuu, kwa mazungumzo zaidi tuwasiliane kwa 0714 919019
Asante sana hizi info za Moro ndo nilikuwa nahitaji maana ni washindani wakuu. Ningependa kuanza na eka chache Pwani nitapanda kwenye September au October ili nipishane nao. Thanks and blessings
Nikipata e mail yako nitakutumia brochure ya nyanya aina ya Anna F1, Assila F1 na Aden F1
Baadhi ya vijiji wanaziita moyo,
Ni nzuri kama ulivyosema, ni tamu sana hata kwa kuzila mbichi!!!!!! na zinazaa sana,zenyewe hazihitaji miti ya kuegeshea kwenda juu kama money maker na marglobe, zinakuwa chini chini hivi. Go for garden man.
Mkuu mi nipo iringa(kilolo) kuna baridi sana eneo hili.. 1.Je nyanya zitakubali?
2. Mbegu gani nitumie?
3. Mbolea aina gani?
4. Ni dawa aina gani muhim kuwa nazo ktk shughuli hii?
Pia naomba ufafanuzi wa vitu vyote muhim maana nataka niazime kwa Mara moja niwe navyo store tu
Bahati nzuri Kilolo naifahamu kwa sehemu, Kilolo ambayo hutapata shida kama utataka kulima nyanya ni Ilula ( pande za Lyasa, Image,Namba saba,nane na namba tisa,Kitonga areas), Ruaha Mbuyuni( hapa pana wajanja kidogo be careful), Pawaga ( mashamba ni ya kukodi, hapa sio Kilolo), pia vijiji vya Ndiwili/Ihimbo/Itimbo/Pomern.
Vile vijiji vya ndani sana kama Kising`a hakufai,sababu gharama za usafirishaji. Kama utakuwa tayari, nitakuunganisha na jamaa yangu pale Ilula ili akusaidie kwa usalama zaidi.
"Shikamoo Malila!",wee jamaa ni noma aisee pawaga ni kwetu kbs eneo ninalotaka kulima ni kihesa mgagao jiran sana pomerin.
Mbegu na madawa ambayo ni lazima niwe nayo ni yapi mkuu maana nahitaji kukopa hayo madawa hvyo nataka nikachukue vyote kwa pamoja. NtakuPM namba zangu mkuu au nitumie nikupgie
Hapo Mgagao nina mashamba ya misitu, anza kulima july ili upishane na ukungu/theruji. Juzi nilipita hapo, kile kipande cha Magereza kulikuwa na ukungu ile mbaya.
Mbona unateseka na nyanya, lima njegere kule bonde la mtitu au mwombe baba Win akupe kinyungu ulime karoti. Halafu makabichi hapo Mgagao yanamea sana, mbona usilime? Kama una bonde zuri, lima kiazi cha kiangazi ili ukitoe october/november kinalipa sana.