Kilimo cha Parachichi kinahitaji kufuga Mbwa wengi kuepuka maparachichi kukosa walaji

Kilimo cha Parachichi kinahitaji kufuga Mbwa wengi kuepuka maparachichi kukosa walaji

Sioni tishio la kukosa soko la parachichi aina ya hass.

Sioni serikali yoyote ile kuvuruga mfumo tulivu wa soko uliopo labda kama haijitaki.

Utanishangaa lakini ukweli ni kwamba tulio wekeza na wanao endelea kuwekeza katika zao la parachichi ni watu wanao jielewa.

Kufanya jambo lolote la kuharibu utajiri tunao ufanyia kazi kwa jasho na damu ni kujitafutia balaa halina kipimo.

Nawahimiza wote wanao taka kuwekeza katika sekta ya kilimo cha parachihi wasitishwe au kukatishwa tamaa.

Kama tunathubutu kuwekeza bila shaka tutathubutu kujitetea pia. Parachichi zitaliwa na watu sio mbwa.
Hahaha kumbe umewekeza ndio maana huwezi kuwa impartial.

Nilikuwa natoa angalizo ila muda utaongea
 
Avocado by nature is a perishable crop hivyo basi uingiliaji wowote utasababisha matunda kuoza tofauti na mkonge,kahawa,nuts nk. ambavyo vinaweza kudumu walau kwenye maghala hata miezi sita.

Biashara ya parachichi ina mfumo tofauti na korosho, kahawa nk.
Kingine avocado ni matunda hivyo basi yanaweza kuuzwa kienyeji kama tuuzavyo maembe , machu gwa, ndimu, ndizi nk.
Hata soko la kimataifa likifa tutauziana humu humu kama machungwa na maisha yataendelea tofauti na kahawa, pamba nk vikibuma unatelekeza shambani.

Zingatia watanzania wameanza kuamka ktk sekta ya usindikaji wa jwisi hivyo basi avocado ina advantage ya kuto dorola kama mazao mengine ya biashara.
Kinachoua huwa Ni matozo
 
Nikisikia mtu amekosa soko la parachichi huwa sielewi tatizo la nchi yetu Ni Nini?
Nilikuwa Burundi nikakuta wanasafirisha parachichi kuja Tanzania wanafaulishia kabanga border pale.
Serikali yetu inafail wapi? Badala ya kutangaza mazao yanyopatikana nchin mwetu wawavutia wanunuzi wao wanaenda kukopa vijisenti
 
Hapo tunarudi kule kule

~poor storage facilities

~poor government policy

~Fluctuation of price at the market and absence of permanent market

~poor technology

~poor transportation network.

~lack of enough skills.

NIPE POINTI MAELEZO NITAJIJUA
Lack of knowledge
Iddi amin war
 
Hahaha kumbe umewekeza ndio maana huwezi kuwa impartial.

Nilikuwa natoa angalizo ila muda utaongea
Nimependa, umewekeza wapi na upo hatua gani.
Changamoto ya parachichi ni barafu kali inayounguza miche midogo na matunda.Una kabiliana vipi?
Mi naona ni bora tupambane kuhakikisha mti wa parachi chi haufi badala ya soko, maana soko huwa lina badirikabadirika kwa kila kitu duniani ila miti ikifa hio ni hasara ya kudumu
 
Nimepanda parachichi miaka kadhaa iliyopita huko kwetu Kusini, soko ikaporomoka parachichi zikaoza nikakosa pa kuzipeleka nikatamani nifuge Mbwa wanisaidie kula yanapoanguka lakini too late

Najuta kuacha kulima miti ya mbao nikadamganyika na faida ya parachichi bila kujiuliza Kuna viwanda nchini vya kununua parachichi au Hadi south?

Tumelima wengi lakini sioni juhudi za kufunguliwa kiwanda Tanzania, tutapata hasara tena na ten hasa kipindi hiki Cha COVID. Serikali mpo tayari tufuge Mbwa?

Je, wakinenepa tutawauza wapi?
Hatua ya kwanza ulishafanikisha, nenda hatua ya pili kwa kujenga kiwanda
 
Milioni 70?au milioni 700
Watu wanapiga pesa hatari...kuna mama wakichaga ni mjane sasa yupo Tukuyu mjini kwenye mashamba ya marehemu mumewe mchaga pia kapiga 700 Million Tzs juzijuzi tu na tunafahamu hawa sababu tupo nao kwenye AMCOS sasa huyu mleta uzi ni ile jamii ya wachawi!!
 
Acha kudanganya watu hakuna mkulima tena tukuyu wa kupata hiyo hela,
Watu wanapiga pesa hatari...kuna mama wakichaga ni mjane sasa yupo Tukuyu mjini kwenye mashamba ya marehemu mumewe mchaga pia kapiga 700 Million Tzs juzijuzi tu na tunafahamu hawa sababu tupo nao kwenye AMCOS sasa huyu mleta uzi ni ile jamii ya wachawi!!
 
Hamna hata moja ulilopatia yote ni kinyume!nenda eneo husika kuko shwari kabisa.
Hapo tunarudi kule kule

~poor storage facilities

~poor government policy

~Fluctuation of price at the market and absence of permanent market

~poor technology

~poor transportation network.

~lack of enough skills.

NIPE POINTI MAELEZO NITAJIJUA
 
Hebu jaribu kutofautisha matumizi ya hayo mazao,kahawa,parachichi,korosho utagundua parachichi ndo yenyewe mkuu ni sawasawa na useme ugali utakosa soko!
Watanzania huwa hamsomi na hamfuatilii hata takwimu za National Bureau of statistics. Korosho ni zao linaloongoza kwa kuchangia Pato la Taifa na kwa mujibu Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) katika msimu wa 2017/2018 mapato ya zao hilo yalifikia Sh1.08 trilioni. Lete takwimu za zao la parachichi walau kwa mwaka mmoja katika kuchangia Pato la taifa.

Stop kulinganisha Korosho na vitu vya ajabu. Point yangu ni moja kuwa mnaolima parachichi kuweni makini Sana siku serikali ikitia mguu mtatafutana, tumeyaona kwenye mazao ya Korosho na kahawa baada ya serikali kuingia.

Eti unasema parachichi Ina miaka 10 ebooo, Sasa kahawa na Korosho si kuanzia uhuru na Hadi Zina Bodi kabisa. Umewahi kusikia bodi ya parachichi?
 
zama hizo na sasa ni tofauti angalia zones zilizoua hayo mazao na ufananishe na zones zinazolima parachichi utagundua asili ya watu wa mahala husika ni issue pia....Lindi, Mtwara, Tanga VS Kilimanjaro, Njombe na Mbeya. Kama huwa unaelewa haraka umenielewa namaanisha nini Avocado ipo sana yaani hizi bad omens zako hazitafanya kazi...mikoa yote inayolima avocado ina watu wanajitambua sana unlike huko zinakolimwa korosho, na mkonge
Mkuu unanitia mashaka na HOJA zako

Kahawa inalimwa kwa wingi Moshi na Bukoba vipi inaendeleaje?

Pamba je?

Tatizo sio zones mkuu
Subiri serikali ione kuna hela huko iwatengenezee na bodi ya parachichi muanze kupangiwa bei, masoko, mjaziwe makodi na makato na madalali “rasmi” wakiingia pale kati mtajuta kuzaliwa
 
Hebu jaribu kutofautisha matumizi ya hayo mazao,kahawa,parachichi,korosho utagundua parachichi ndo yenyewe mkuu ni sawasawa na useme ugali utakosa soko!
Peleka ugali wako Zanzibar uone Kama utauza.

Unaongea vitu hata hujui
 
Watu wanapiga pesa hatari...kuna mama wakichaga ni mjane sasa yupo Tukuyu mjini kwenye mashamba ya marehemu mumewe mchaga pia kapiga 700 Million Tzs juzijuzi tu na tunafahamu hawa sababu tupo nao kwenye AMCOS sasa huyu mleta uzi ni ile jamii ya wachawi!!
Mkuu unajua milioni 700 ni sawa na maparachichi mangapi na yatachukua ukubwa wa shamba kiasi gani?
Acha stori za kwenye gahawa hapa
 
Peleka ugali wako Zanzibar uone Kama utauza.

Unaongea vitu hata hujui
Wewe ndio hujui bora ungenyamaza ,maana hiyo ya maparachichi ni dili tena kubwa sana,demand yake imeongezeka sana baada ya nchi zilizokuwa zinazalisha kwa wingi kushindwa kutosheleza soko la ulaya na Asia kutokana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.Na msimu tunaovuna sisi wao wanakuwa hawana ,hivyo ni fursa kwetu!acha kubisha kitu hujui bora unyamaze au ujifunze kuliko hivi unavyojidai mjuaji kama chakubanga na polo.
 
Nimepanda parachichi miaka kadhaa iliyopita huko kwetu Kusini, soko ikaporomoka parachichi zikaoza nikakosa pa kuzipeleka nikatamani nifuge Mbwa wanisaidie kula yanapoanguka lakini too late

Najuta kuacha kulima miti ya mbao nikadamganyika na faida ya parachichi bila kujiuliza Kuna viwanda nchini vya kununua parachichi au Hadi south?

Tumelima wengi lakini sioni juhudi za kufunguliwa kiwanda Tanzania, tutapata hasara tena na ten hasa kipindi hiki Cha COVID. Serikali mpo tayari tufuge Mbwa?

Je, wakinenepa tutawauza wapi?
Upo maeneo gani mzee??,Umelima aina gani ya Parachichi??.
 
Hass Avocado inawalipa wakulima Njombe watu wameacha kulima miti ya pine wanalima Hass Avocado na wanakuwa mamilionea...soko la uhakika lipo na kuna kampuni lukuki huko zimewekeza ukusanyaji na ukulima wa Hass avocado...mleta mada ni jamaa asiechangamsha akili analeta mada ya kuwa discourage prospective farmers wengine...

Avocado siyo ya kuifananisha na kilimo cha matikiti au sijui mananasi...Avocado ina soko la uhakika abroad including China na watu wanatajirika sana hasa Njombe.

Huyu mleta uzi nadiriki kusema ni FAILURE na APUUZWE.
Naunga mkono hoja.
 
Watu wanapiga pesa hatari...kuna mama wakichaga ni mjane sasa yupo Tukuyu mjini kwenye mashamba ya marehemu mumewe mchaga pia kapiga 700 Million Tzs juzijuzi tu na tunafahamu hawa sababu tupo nao kwenye AMCOS sasa huyu mleta uzi ni ile jamii ya wachawi!!
Ukute hata shamba la parachichi hana,lengo lake ni kuwakatisha tamaa wanaotaka kulima parachichi.
 
Nakushangaa sana unaposema Umekosa soko la parachichi kwanza utujibu umelima hela ngapi? parachichi zipi?? kama ni Hass hata za Kawaida hukosi soko.
acha Uongo mzee
 
Back
Top Bottom