SoC02 Kilimo cha Pilipili Kichaa (Dhahabu nyekundu) kinavyonipa pesa bila kutarajia

Stories of Change - 2022 Competition

the_diplomat

Member
Joined
Sep 1, 2022
Posts
81
Reaction score
75
Baada ya kuhitimu Shahada ya Sanaa (BA)2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), nilitafuta kazi bila mafanikio. Nikaona nisome Stashahada ya Uzamili katika Elimu nikamaliza 2014 ili nipate ajira ya ualimu, sikufanikiwa kuipata. Mwaka 2016 nikaanza kusoma Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tazania nikiwa na malengo ya kujiaandaa kuwa mwanasheria wa kujitegemea na kuhitimu 2020.

Nikiwa natafakari jinsi yakupata pesa kwenda Shule ya Sheria (Law School of Tanzania) mwaka, nikasikia watu wanaongelea habari ya kilimo cha pilipili kichaa (DHAHABU NYEKUNDU). Nikaona nitafute habari kamili ya kilimo hiki.

Nikatafuta tovuti mbalimbali na kwenye mitandao ya kijamii hususani Facebook nikaona kuna wakulima wengi ambao wanatoa ushuhuda wa kilimo hiki cha pilipili kichaa (DHAHABU NYEKUNDU). Lakini pia nikaona nchi kama Kenya na Uganda ni nchi ambazo pilipili kichaa hulimwa kwa wingi. Pia nikatafuta taarifa za masoko, nikaona masoko yake makuu ni nchi za bara la Asia na Ulaya. Hii ilinipa ‘moto mkuu’ usiozimika kuingia shambani na kuanza kazi ya kuandaa shamba.

Nikiwa na Kiasi cha 1,900,000/- ikiwa ndio akiba pekee. Sikujali nikaamua ‘ku-take risk’. Nikaamua kwenda inapolimwa pilipili Mkoa wa Kigoma , Uvinza na kuweka kambi ya kazi. Niliandaa shamba la ekari 2, gharama ya kukodi shamba 50,000/ ekari kwa mwaka.​

KAMBI YA KAZI.PNG

MAANDALIZI YA MBEGU

Nilitafuta mbegu aina ya African Bird’s Eye Chilli (ABE), hii ni aina ya mbegu ya pilipili yenye matunda kama macho ya ndege pori wengi wanaopatika Afrika. Aina hii ya pilipili huzaa sana na hususani ikipata maji ya kutosha. Nilichukua gramu 100 kwa 100,000/-, kwani hutosha la ekari 2 , kila ekari huchukua mimea 4500 hadi 5000.
MBEGU.PNG

MAANDALIZI YA VITALU
Nilitafuta maeneo yaliyo karibu na mto nikaandaa maeoneo ya vitalu 3 kwa ajili ya kusia mbegu. Niliweka mbolea ya samadi ya kutosha kiasi cha debe 3 kwa kila kitalu kulingana na ukubwa wa kitalu, nikaweka majani makavu kuhifadhi unyevu kwenye udongo (kama vinavyoonekana kwenye picha). Huchukua muda wa wiki 3 mbegu zote kuwa zimeota vizuri, katika picha kuna miche mikubwa ambayo niliitolea kivuli na midogo ambayo bado ilihitaji kivuli kwakuwa ilichelewa kuota, ingawa ilipandwa pamoja.
KITALU.PNG

KITALU 2.PNG

UPANDIKIZAJI WA MICHE
Shamba lililimwa kwa jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau) ili kulainisha shamba. Baadaye nilitafuta vijana 3 niliingia nao makubaliano kunitengezea matuta shambani, shughuli za kutengeneza matuta kama vile kuchimba mashimo, kuweka mbolea na kupandikiza miche kwa TZS 600,000/-. Kita tuta lilikuwa na mita 3.5, na kuchimba mashimo kwenye kila tuta, umbali wa sentimita 90 shimo hadi shimo, mita 1 msitari hadi msitari, na kila shimo liliwekewa mbolea ya samadi kilo 1 na hapa nilitumia vikombe viwili vya nusu lita.

KITALU3.PNG

Upandikizaji wa mimea hufanyika siku 45 tangu mbegu kuwekwa kitaluni. Kwa kipindi cha siku hizo mimea huwa na uwezo wa kustahimili hali ya ukame kidogo hata kama mvua isiponyesha wiki moja bado unauwezo wa kuendelea na uhai wake.
KITALU 4.PNG

UTUNZAJI NA UKUAJI WA MICHE/MIMEA YA PILIPILI SHAMBANI
1. Mbolea:

Niliweka mbolea ya Samadi ya kutosha kuanzia kitaluni hadi shambani. Mbolea ya Samadi sikununua kwa kuwa wafugaji ni wengimaeneo haya, niliwaomba nao wakanipatia bure, gharama ilikuwa ni kwenye kusomba mbolea hiyo. Nilitumia mkokoteni wa kukokotwa na ng’ombe, mbapo ilinigharimu 140,000/- kusomba mbolea ya kutosha shamba zima la ekari 2.​

KWAMA 22.PNG

Pia nilitafuta lita mbili za mbolea ya Organic inayotoka kampuni ya MOKUSAKU inayoitwa MOKUSAKU Cal-Phos na NPK PLUS kwa kuongeza virutubisho kwenye mimea na kuhifadhi maua yasidondoke. Kila lita ni 30,000/- hivyo kwa lita 4 ilinigharimu 120,000/-​

MOKUSAKU BN.PNG

PILIPILI MOKU.PNG

2. Palizi
Palizi ya kwanza ni baada ya wiki ya 3 mimea ikiwa shambani. Niliendelea kupalilia magugu yanapoota. Palizi lilinigharimu kiasi cha 200,000 mpaka mimea ilipokuwa na matawi na majani mengi na kuzuia magugu kuota kwa wingi.
MIMEA SHAMBA.PNG

pilipili new.PNG

CHANGAMOTO ZA UKUAJI WA MICHE YA PILIPILI
1. Magonjwa

Pilipili hukabiliwa na ugonjwa wa ukungu, usipodhibiti mapema majani hujikunja (kama inavyoonekana katika picha za mimes aliyaanza kuugua) na mmea kupukutisha majani yote. Nilitumia dawa ya Innovex 360 SC kudhibiti ugonjwa huu, gharama 80,000/-
UKUNGU.PNG

2. Mchwa na Panzi
Mchwa wanakata mashina chini kwenye udongo na panzi wanakula majani sana. Nilitumia dawa ya NINJA kuzuia panzi , na TERMITE KILLER kwa ajili ya mchwa , gharama 50,000/-.

UVUNAJI NA UKAUSHAJI

Kuanza kuweka mimea shambani mpaka kuanza kuvuna ni miezi 3, ongeza siku 45 za miche kitaluni. Uvunaji hufanyika kwa kuchuma pilipili iliyoiva na nyekundu kama nyanya. Uvunaji huwa ni kazi kwelikweli, ndoo ndogo ya lita kumi (ambayo ni 3.5-4 kg za pilipili) huvunwa kwa 3000/- hadi 3500/- (hapa ndipo gharama kubwa huitajika na ndio ilitumia kiasi kilichobakia). Na pilipili iliyoiva hutoka kwenye kikonyo chake kwa haraka. Pilipili iliyovunwa huwekwa juani kwa muda wa siku 3 baada ya hapo inakuwa imekauka, itunze ndani sehemu kavu yenye hewa na mwanga . Jambo la kupendeza katika katika MGODI HUU WA DHAHABU NYEKUNDU ni kwamba pilipili iliyo tayari inaingia sokoni na hivyo kukusaidia kupata pesa ya kuendesha uvunaji, hiki ndio kitu cha pekee katika zao hili. Nimeanza kuvuna Mei mpaka sasa naendelea kuvuna, uvunaji natarajia kuisha Septemba
stiveppp.PNG
kausha 2.PNG

KUCHAMBUA
Kabla ya kuuza pilipili uichambue iwe safi, usiweke iliyoharibika . Zitenge hizo zilizoharibika usizitupe nazo zinauzika pia.

chambua 2.PNG

UUZAJI
Masoko ya Pilipili kichaa yapo na unatakiwa kuwa makini na madalali wa pilipili, wengi wao ni matapeli. Mimi nawauzia kampuni ya TAZAMA ambayo inachukua mzigo na kupeleka Kenya, hii kampuni ni ya uhakika na wanatoa pesa yote kwa mkulima.​
MAUZO.PNG

Na uuzaji hufanyika kila baada ya wiki mbili. Hata sasa ninavyomalizia kuandika Habari(Story) TAZAMA wamenitumia pesa ya awali kwa mzigo ulisafiri wiki hii.​
muamala.PNG

FAIDA
Faida ya zao hili, kuna mimea 9400 shambani. Nilijiwekea mmea mmoja utoe robo kilo, naelekea kuvuka malengo ya robo kilo kwa mmea, kuna mimea inatoa mpaka robo tatu ya kilo 3/4 . Na kila kilo bei yake ni TZS. 5000/- Lakini pia zile zilizoharibika bei yake ni TZS 1000/ kwa kilo moja. Na zao hili nitaendelea kuvuna kwa miaka mingine mitatu. MUNGU NI MWEMA, SANA KARIBU MGODINI​
 
Attachments

  • ukaushaji.PNG
    ukaushaji.PNG
    129.6 KB · Views: 181
Upvote 93
Baada ya kuhitimu Shahada ya Sanaa (BA)2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), nilitafuta kazi bila mafanikio. Nikaona nisome Stashahada ya Uzamili katika Elimu nikamaliza 2014 ili nipate ajira ya ualimu, sikufanikiwa kuipata. Mwaka 2016 nikaanza kusoma Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tazania nikiwa na malengo ya kujiaandaa kuwa mwanasheria wa kujitegemea na kuhitimu 2020.

Nikiwa natafakari jinsi yakupata pesa kwenda Shule ya Sheria (Law School of Tanzania) mwaka, nikasikia watu wanaongelea habari ya kilimo cha pilipili kichaa (DHAHABU NYEKUNDU). Nikaona nitafute habari kamili ya kilimo hiki.

Nikatafuta tovuti mbalimbali na kwenye mitandao ya kijamii hususani Facebook nikaona kuna wakulima wengi ambao wanatoa ushuhuda wa kilimo hiki cha pilipili kichaa (DHAHABU NYEKUNDU). Lakini pia nikaona nchi kama Kenya na Uganda ni nchi ambazo pilipili kichaa hulimwa kwa wingi. Pia nikatafuta taarifa za masoko, nikaona masoko yake makuu ni nchi za bara la Asia na Ulaya. Hii ilinipa ‘moto mkuu’ usiozimika kuingia shambani na kuanza kazi ya kuandaa shamba.

Nikiwa na Kiasi cha 1,900,000/- ikiwa ndio akiba pekee. Sikujali nikaamua ‘ku-take risk’. Nikaamua kwenda inapolimwa pilipili Mkoa wa Kigoma , Uvinza na kuweka kambi ya kazi. Niliandaa shamba la ekari 2, gharama ya kukodi shamba 50,000/ ekari kwa mwaka.​

Kambi ya Kazi ikiwa inajengwa
View attachment 2342130

MAANDALIZI YA MBEGU

Nilitafuta mbegu aina ya African Bird’s Eye Chilli (ABE), hii ni aina ya mbegu ya pilipili yenye matunda kama macho ya ndege pori wengi wanaopatika Afrika. Aina hii ya pilipili huzaa sana na hususani ikipata maji ya kutosha. Nilichukua gramu 100 kwa 100,000/-, kwani hutosha la ekari 2 , kila ekari huchukua mimea 4500 hadi 5000.
Mbegu za Pipipili aina ya ABE zikiwa zimewekwa tayari udongoni
View attachment 2342266

MAANDALIZI YA VITALU
Nilitafuta maeneo yaliyo karibu na mto nikaandaa maeoneo ya vitalu 3 kwa ajili ya kusia mbegu. Niliweka mbolea ya samadi ya kutosha kiasi cha debe 3 kwa kila kitalu kulingana na ukubwa wa kitalu, nikaweka majani makavu kuhifadhi unyevu kwenye udongo (kama vinavyoonekana kwenye picha). Huchukua muda wa wiki 3 mbegu zote kuwa zimeota vizuri, katika picha kuna miche mikubwa ambayo niliitolea kivuli na midogo ambayo bado ilihitaji kivuli kwakuwa ilichelewa kuota, ingawa ilipandwa pamoja. (PICHA[emoji116])
Kitalu 1: Majani kuhifadhi unyevu
View attachment 2342095

Kitalu 2 Mimea iliyoota mapema na iliyochelewa kuota

View attachment 2342096

UPANDIKIZAJI WA MICHE
Shamba lililimwa kwa jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau) ili kulainisha shamba. Baadaye nilitafuta vijana 3 niliingia nao makubaliano kunitengezea matuta shambani, shughuli za kutengeneza matuta kama vile kuchimba mashimo, kuweka mbolea na kupandikiza miche kwa TZS 600,000/-. Kita tuta lilikuwa na mita 3.5, na kuchimba mashimo kwenye kila tuta, umbali wa sentimita 90 shimo hadi shimo, mita 1 msitari hadi msitari, na kila shimo liliwekewa mbolea ya samadi kilo 1 na hapa nilitumia vikombe viwili vya nusu lita . ( PICHA[emoji116]).

View attachment 2342103

Upandikizaji wa mimea hufanyika siku 45 tangu mbegu kuwekwa kitaluni. Kwa kipindi cha siku hizo mimea huwa na uwezo wa kustahimili hali ya ukame kidogo hata kama mvua isiponyesha wiki moja bado unauwezo wa kuendelea na uhai wake. (PICHA[emoji116])​
View attachment 2342106

UTUNZAJI NA UKUAJI WA MICHE/MIMEA YA PILIPILI SHAMBANI
1. Mbolea:

Niliweka mbolea ya Samadi ya kutosha kuanzia kitaluni hadi shambani. Mbolea ya Samadi sikununua kwa kuwa wafugaji ni wengimaeneo haya, niliwaomba nao wakanipatia bure, gharama ilikuwa ni kwenye kusomba mbolea hiyo. Nilitumia mkokoteni wa kukokotwa na ng’ombe, mbapo ilinigharimu 140,000/- kusomba mbolea ya kutosha shamba zima la ekari 2.​

Picha kutoka : http://photos1.blogger.com/blogger/5177/2506/1600/DSCF0587.jpg
View attachment 2342137

Pia nilitafuta lita mbili za mbolea ya Organic inayotoka kampuni ya MOKUSAKU inayoitwa MOKUSAKU Cal-Phos na NPK PLUS kwa kuongeza virutubisho kwenye mimea na kuhifadhi maua yasidondoke. Kila lita ni 30,000/- hivyo kwa lita 4 ilinigharimu 120,000/-​
Picha kwa hisani ya : https://mokusaku.com/
View attachment 2342126

Picha za miche ya pilipili yenye mbolea ya Samadi na MOKUSAKU Cal-Phos na NPK Plus
View attachment 2342151

2. Palizi
Palizi ya kwanza ni baada ya wiki ya 3 mimea ikiwa shambani. Niliendelea kupalilia magugu yanapoota. Palizi lilinigharimu kiasi cha 200,000 mpaka mimea ilipokuwa na matawi na majani mengi na kuzuia magugu kuota kwa wingi.
(PICHA[emoji116])
View attachment 2342164

CHANGAMOTO ZA UKUAJI WA MICHE YA PILIPILI
1. Magonjwa

Pilipili hukabiliwa na ugonjwa wa ukungu, usipodhibiti mapema majani hujikunja (kama inavyoonekana katika picha za mimes aliyaanza kuugua) na mmea kupukutisha majani yote. Nilitumia dawa ya Innovex 360 SC kudhibiti ugonjwa huu, gharama 80,000/-
(PICHA [emoji116])
View attachment 2342184

2. Mchwa na Panzi
Mchwa wanakata mashina chini kwenye udongo na panzi wanakula majani sana. Nilitumia dawa ya NINJA kuzuia panzi , na TERMITE KILLER kwa ajili ya mchwa , gharama 50,000/-.

UVUNAJI NA UKAUSHAJI

Kuanza kuweka mimea shambani mpaka kuanza kuvuna ni miezi 3, ongeza siku 45 za miche kitaluni. Uvunaji hufanyika kwa kuchuma pilipili iliyoiva na nyekundu kama nyanya. Uvunaji huwa ni kazi kwelikweli, ndoo ndogo ya lita kumi (ambayo ni 3.5-4 kg za pilipili) huvunwa kwa 3000/- hadi 3500/- (hapa ndipo gharama kubwa huitajika na ndio ilitumia kiasi kilichobakia). Na pilipili iliyoiva hutoka kwenye kikonyo chake kwa haraka. Pilipili iliyovunwa huwekwa juani kwa muda wa siku 3 baada ya hapo inakuwa imekauka, itunze ndani sehemu kavu yenye hewa na mwanga . Jambo la kupendeza katika katika MGODI HUU WA DHAHABU NYEKUNDU ni kwamba pilipili iliyo tayari inaingia sokoni na hivyo kukusaidia kupata pesa ya kuendesha uvunaji, hiki ndio kitu cha pekee katika zao hili. Nimeanza kuvuna mwezi wa tano (Mei) mpaka sasa naendelea kuvuna, uvunaji natarajia kuisha mwezi wa tisa (Septemba).
(PICHA[emoji116] Uvunaji)
View attachment 2342205

(Picha[emoji116] ukaushaji)
View attachment 2342210

KUCHAMBUA
Kabla ya kuuza pilipili uichambue iwe safi, usiweke iliyoharibika . Zitenge hizo zilizoharibika usizitupe nazo zinauzika pia.

View attachment 2342213

UUZAJI
Masoko ya Pilipili kichaa yapo na unatakiwa kuwa makini na madalali wa pilipili, wengi wao ni matapeli. Mimi nawauzia kampuni ya TAZAMA ambayo inachukua mzigo na kupeleka Kenya, hii kampuni ni ya uhakika na wanatoa pesa yote kwa mkulima.​
(PICHA[emoji116] nikiwa napima mzigo wa pilipili kichaa mwezi wa Agust 28, 2022)
View attachment 2342224
Na uuzaji hufanyika kila baada ya wiki mbili. Hata sasa ninavyomalizia kuandika Habari(Story) TAZAMA wamenitumia pesa ya awali kwa mzigo ulisafiri wiki hii.​
(PICHA[emoji116] Angalia tarehe na muda wa tukio: 01.09.2022 muda saa 18:02)
View attachment 2342239

FAIDA
Faida ya zao hili, kuna mimea 9400 shambani. Nilijiwekea mmea mmoja utoe robo kilo, naelekea kuvuka malengo ya robo kilo kwa mmea, kuna mimea inatoa mpaka robo tatu ya kilo 3/4 . Na kila kilo bei yake ni TZS. 5000/- Lakini pia zile zilizoharibika bei yake ni TZS 1000/ kwa kilo moja. Na zao hili nitaendelea kuvuna kwa miaka mingine mitatu. MUNGU NI MWEMA, SANA KARIBU MGODINI​
Naomba kuuliza hio Robo kilo unaipata ktk mchumo wa mwanzo au ni ndani ya miaka hio ni miaka 3.
 
Katika mchumo wa kwanza, pilipili huzaa sana.....ikipata maji unachuma zilizoiva na huku zikiendelea kuweka maua mengine, naomba na kura yako pia
 
Attachments

  • IMG_20220508_111112_783.jpg
    IMG_20220508_111112_783.jpg
    1.9 MB · Views: 43
  • IMG_20220508_111255_579.jpg
    IMG_20220508_111255_579.jpg
    2 MB · Views: 46
VETESSE, BLUE BEAM, VEGRAB, DATA TRIP, SUNSHINE, hawa wote ni madalali achana nao
Kaka hiyo namba uliyoweka(0759526397) nimepiga muda huu,aliyepokea kwanza alitaka kujua nimeipata wapi namba nilipomwambia jf akakata simu. Nikampigia tena akesema imekatika kwa bahati mbaya
akasema ngoja nikuunganishe na mhusika mwenye uwezo wa kujibu maswali akakata simu tena,wakati mimi mpigaji sina haraka,
na mimi niliuliza ofisi zenu ziko wapi? hilo tu limemtoa jasho.
Kwa ufupi naungana na wanaoona ni kama kuna mchongo fulani.

Kusema ukweli kwa hali tuliyonayo,ongeza na tozo si rahisi kupiga hela kirahisi rahisi.
tuendelee kutafakari
 
pole sana mkuu, nakukaribisha shambani ujionee mwenyewe na ukifika najua utasema huu sio mchongo fulani, au kama una mtu yuko kigoma mwambie aje mashambani Uvinza ajionee kazi inavyoenda
 
Kaka hiyo namba uliyoweka (0759526397) nimepiga muda huu,aliyepokea kwanza alitaka kujua nimeipata wapi namba nilipomwambia jf akakata simu. Nikampigia tena akesema imekatika kwa bahati mbaya
akasema ngoja nikuunganishe na mhusika mwenye uwezo wa kujibu maswali akakata simu tena,wakati mimi mpigaji sina haraka,
na mimi niliuliza ofisi zenu ziko wapi? hilo tu limemtoa jasho.
Kwa ufupi naungana na wanaoona ni kama kuna mchongo fulani.

Kusema ukweli kwa hali tuliyonayo,ongeza na tozo si rahisi kupiga hela kirahisi rahisi.
tuendelee kutafakari
pole ungemwambia nimepewa na mkulima wa pilipili kutoka Uvinza, Kigoma....wanapatikana Arusha, Jengo la Moleli
 
Mkuu hawa wote umewajuaje kwa mda mfupi?

Kwanini una force watu wakuamini na unaweka namba za hio kampuni ya mnunuzi?

Ingekuwa ni vyema uwache members waulize namba mnunuzi kwanza wenyewe...

Kilimo cha kwanza uko na uzoefu kama mkulima mbobezi.
Uzi wako nimeutilia walakini...

Kama kuna mtu yuko kigoma atufanyie uchunguzi kabla hatujatumbukia humo.
Ni ajabu mpaka sasa hivi watu hawajui ''dalili'' za tapeli. Tanzania hii hii na raia hawa hawa, eti atokee raia mmoja aone ''huruma'' kiasi cha kuanika siri za kuingiza fedha kirahisi na tena atumie nguvu kubwa ''kutafadhalisha'' watu wamwamini. Maweeee!. Huyu jamaa amejaa dalili zote za utapeli. Kama alivyosema jamaa mmoja ni kuwa jamaa anatega mingo ili apige watu kwa kuwauzia mbegu. Utapeli wa aina hii ndiyo umeshika kasi sana siku hizi i.e. Create demand ya uongo ya bidhaa fulani, wajinga wanapokuwa wanapapatika, wauzie ile bidhaa. Utapeli kama huu atawapata watu wasio na exposure lakini siyo mimi. Mimi najua jinsi nchi za Asia zinavyozalisha pilipili kichaa kwa wingi na mpaka Europe wanapeleka tena kwa bei ndogo kabisa.
NB: Hizi namba anazoweka ni za washirika wake na ukijaribu kupiga watakupa maneno mazuri ya kufurahisha ili uingie kingi. Nimeamuuliza asema mahali ofisi zilipo lakini jamaa anaishia kutoa namba tu.
 
Baada ya kuhitimu Shahada ya Sanaa (BA)2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), nilitafuta kazi bila mafanikio. Nikaona nisome Stashahada ya Uzamili katika Elimu nikamaliza 2014 ili nipate ajira ya ualimu, sikufanikiwa kuipata. Mwaka 2016 nikaanza kusoma Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tazania nikiwa na malengo ya kujiaandaa kuwa mwanasheria wa kujitegemea na kuhitimu 2020.

Nikiwa natafakari jinsi yakupata pesa kwenda Shule ya Sheria (Law School of Tanzania) mwaka, nikasikia watu wanaongelea habari ya kilimo cha pilipili kichaa (DHAHABU NYEKUNDU). Nikaona nitafute habari kamili ya kilimo hiki.

Nikatafuta tovuti mbalimbali na kwenye mitandao ya kijamii hususani Facebook nikaona kuna wakulima wengi ambao wanatoa ushuhuda wa kilimo hiki cha pilipili kichaa (DHAHABU NYEKUNDU). Lakini pia nikaona nchi kama Kenya na Uganda ni nchi ambazo pilipili kichaa hulimwa kwa wingi. Pia nikatafuta taarifa za masoko, nikaona masoko yake makuu ni nchi za bara la Asia na Ulaya. Hii ilinipa ‘moto mkuu’ usiozimika kuingia shambani na kuanza kazi ya kuandaa shamba.

Nikiwa na Kiasi cha 1,900,000/- ikiwa ndio akiba pekee. Sikujali nikaamua ‘ku-take risk’. Nikaamua kwenda inapolimwa pilipili Mkoa wa Kigoma , Uvinza na kuweka kambi ya kazi. Niliandaa shamba la ekari 2, gharama ya kukodi shamba 50,000/ ekari kwa mwaka.​

Kambi ya Kazi ikiwa inajengwa
View attachment 2342130

MAANDALIZI YA MBEGU

Nilitafuta mbegu aina ya African Bird’s Eye Chilli (ABE), hii ni aina ya mbegu ya pilipili yenye matunda kama macho ya ndege pori wengi wanaopatika Afrika. Aina hii ya pilipili huzaa sana na hususani ikipata maji ya kutosha. Nilichukua gramu 100 kwa 100,000/-, kwani hutosha la ekari 2 , kila ekari huchukua mimea 4500 hadi 5000.
Mbegu za Pipipili aina ya ABE zikiwa zimewekwa tayari udongoni
View attachment 2342266

MAANDALIZI YA VITALU
Nilitafuta maeneo yaliyo karibu na mto nikaandaa maeoneo ya vitalu 3 kwa ajili ya kusia mbegu. Niliweka mbolea ya samadi ya kutosha kiasi cha debe 3 kwa kila kitalu kulingana na ukubwa wa kitalu, nikaweka majani makavu kuhifadhi unyevu kwenye udongo (kama vinavyoonekana kwenye picha). Huchukua muda wa wiki 3 mbegu zote kuwa zimeota vizuri, katika picha kuna miche mikubwa ambayo niliitolea kivuli na midogo ambayo bado ilihitaji kivuli kwakuwa ilichelewa kuota, ingawa ilipandwa pamoja. (PICHA👇)

Kitalu 1: Majani kuhifadhi unyevu
View attachment 2342095

Kitalu 2 Mimea iliyoota mapema na iliyochelewa kuota

View attachment 2342096

UPANDIKIZAJI WA MICHE
Shamba lililimwa kwa jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau) ili kulainisha shamba. Baadaye nilitafuta vijana 3 niliingia nao makubaliano kunitengezea matuta shambani, shughuli za kutengeneza matuta kama vile kuchimba mashimo, kuweka mbolea na kupandikiza miche kwa TZS 600,000/-. Kita tuta lilikuwa na mita 3.5, na kuchimba mashimo kwenye kila tuta, umbali wa sentimita 90 shimo hadi shimo, mita 1 msitari hadi msitari, na kila shimo liliwekewa mbolea ya samadi kilo 1 na hapa nilitumia vikombe viwili vya nusu lita . ( PICHA👇).

View attachment 2342103

Upandikizaji wa mimea hufanyika siku 45 tangu mbegu kuwekwa kitaluni. Kwa kipindi cha siku hizo mimea huwa na uwezo wa kustahimili hali ya ukame kidogo hata kama mvua isiponyesha wiki moja bado unauwezo wa kuendelea na uhai wake. (PICHA👇)​
View attachment 2342106

UTUNZAJI NA UKUAJI WA MICHE/MIMEA YA PILIPILI SHAMBANI
1. Mbolea:

Niliweka mbolea ya Samadi ya kutosha kuanzia kitaluni hadi shambani. Mbolea ya Samadi sikununua kwa kuwa wafugaji ni wengimaeneo haya, niliwaomba nao wakanipatia bure, gharama ilikuwa ni kwenye kusomba mbolea hiyo. Nilitumia mkokoteni wa kukokotwa na ng’ombe, mbapo ilinigharimu 140,000/- kusomba mbolea ya kutosha shamba zima la ekari 2.​

Picha kutoka : http://photos1.blogger.com/blogger/5177/2506/1600/DSCF0587.jpg
View attachment 2342137

Pia nilitafuta lita mbili za mbolea ya Organic inayotoka kampuni ya MOKUSAKU inayoitwa MOKUSAKU Cal-Phos na NPK PLUS kwa kuongeza virutubisho kwenye mimea na kuhifadhi maua yasidondoke. Kila lita ni 30,000/- hivyo kwa lita 4 ilinigharimu 120,000/-​
Picha kwa hisani ya : https://mokusaku.com/
View attachment 2342126

Picha za miche ya pilipili yenye mbolea ya Samadi na MOKUSAKU Cal-Phos na NPK Plus
View attachment 2342151

2. Palizi
Palizi ya kwanza ni baada ya wiki ya 3 mimea ikiwa shambani. Niliendelea kupalilia magugu yanapoota. Palizi lilinigharimu kiasi cha 200,000 mpaka mimea ilipokuwa na matawi na majani mengi na kuzuia magugu kuota kwa wingi.
(PICHA👇)
View attachment 2342164

CHANGAMOTO ZA UKUAJI WA MICHE YA PILIPILI
1. Magonjwa

Pilipili hukabiliwa na ugonjwa wa ukungu, usipodhibiti mapema majani hujikunja (kama inavyoonekana katika picha za mimes aliyaanza kuugua) na mmea kupukutisha majani yote. Nilitumia dawa ya Innovex 360 SC kudhibiti ugonjwa huu, gharama 80,000/-
(PICHA 👇)
View attachment 2342184

2. Mchwa na Panzi
Mchwa wanakata mashina chini kwenye udongo na panzi wanakula majani sana. Nilitumia dawa ya NINJA kuzuia panzi , na TERMITE KILLER kwa ajili ya mchwa , gharama 50,000/-.

UVUNAJI NA UKAUSHAJI

Kuanza kuweka mimea shambani mpaka kuanza kuvuna ni miezi 3, ongeza siku 45 za miche kitaluni. Uvunaji hufanyika kwa kuchuma pilipili iliyoiva na nyekundu kama nyanya. Uvunaji huwa ni kazi kwelikweli, ndoo ndogo ya lita kumi (ambayo ni 3.5-4 kg za pilipili) huvunwa kwa 3000/- hadi 3500/- (hapa ndipo gharama kubwa huitajika na ndio ilitumia kiasi kilichobakia). Na pilipili iliyoiva hutoka kwenye kikonyo chake kwa haraka. Pilipili iliyovunwa huwekwa juani kwa muda wa siku 3 baada ya hapo inakuwa imekauka, itunze ndani sehemu kavu yenye hewa na mwanga . Jambo la kupendeza katika katika MGODI HUU WA DHAHABU NYEKUNDU ni kwamba pilipili iliyo tayari inaingia sokoni na hivyo kukusaidia kupata pesa ya kuendesha uvunaji, hiki ndio kitu cha pekee katika zao hili. Nimeanza kuvuna mwezi wa tano (Mei) mpaka sasa naendelea kuvuna, uvunaji natarajia kuisha mwezi wa tisa (Septemba).
(PICHA👇 Uvunaji)
View attachment 2342205

(Picha👇 ukaushaji)
View attachment 2342210

KUCHAMBUA
Kabla ya kuuza pilipili uichambue iwe safi, usiweke iliyoharibika . Zitenge hizo zilizoharibika usizitupe nazo zinauzika pia.

View attachment 2342213

UUZAJI
Masoko ya Pilipili kichaa yapo na unatakiwa kuwa makini na madalali wa pilipili, wengi wao ni matapeli. Mimi nawauzia kampuni ya TAZAMA ambayo inachukua mzigo na kupeleka Kenya, hii kampuni ni ya uhakika na wanatoa pesa yote kwa mkulima.​
(PICHA👇 nikiwa napima mzigo wa pilipili kichaa mwezi wa Agust 28, 2022)
View attachment 2342224
Na uuzaji hufanyika kila baada ya wiki mbili. Hata sasa ninavyomalizia kuandika Habari(Story) TAZAMA wamenitumia pesa ya awali kwa mzigo ulisafiri wiki hii.​
(PICHA👇 Angalia tarehe na muda wa tukio: 01.09.2022 muda saa 18:02)
View attachment 2342239

FAIDA
Faida ya zao hili, kuna mimea 9400 shambani. Nilijiwekea mmea mmoja utoe robo kilo, naelekea kuvuka malengo ya robo kilo kwa mmea, kuna mimea inatoa mpaka robo tatu ya kilo 3/4 . Na kila kilo bei yake ni TZS. 5000/- Lakini pia zile zilizoharibika bei yake ni TZS 1000/ kwa kilo moja. Na zao hili nitaendelea kuvuna kwa miaka mingine mitatu. MUNGU NI MWEMA, SANA KARIBU MGODINI​
hongera
 
Kaka hiyo namba uliyoweka(0759526397) nimepiga muda huu,aliyepokea kwanza alitaka kujua nimeipata wapi namba nilipomwambia jf akakata simu. Nikampigia tena akesema imekatika kwa bahati mbaya
akasema ngoja nikuunganishe na mhusika mwenye uwezo wa kujibu maswali akakata simu tena,wakati mimi mpigaji sina haraka,
na mimi niliuliza ofisi zenu ziko wapi? hilo tu limemtoa jasho.
Kwa ufupi naungana na wanaoona ni kama kuna mchongo fulani.

Kusema ukweli kwa hali tuliyonayo,ongeza na tozo si rahisi kupiga hela kirahisi rahisi.
tuendelee kutafakari
Kwa hiyo kwa akili yako ukaona kabisa hapa kuna hela? Ukahangaika na kupiga simu?

Hivi wabongo hamuoni au shida ni nini. Elimu kazi yake nini sasa
 
Back
Top Bottom